Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mshahara wako unalipa kodi miezi sita?

IMG 4046.jpeg Mshahara wako unalipa kodi miezi sita?

Sat, 6 May 2023 Chanzo: Mwananchi

Ian ni mwajiriwa wa taasisi yaa umma. Mshahara wake ni wa kawaida ambao unaweza kumsaidia kulipa bili na matumizi yake ya kawaida.

Ian yupo kazini kwa kipindi cha miaka 12, lakini hali yake ya kifedha inazorota kila kukicha. Ian ana mikopo kutoka katika benki tofauti na taasisi nyingine za kifedha.

Kila apunguzapo madeni hayo, anachukua mkopo wa nyongeza ili kukidhi mahitaji yake. Ian amefika wakati ambao hakuna sehemu ya kukopa.

Mbaya zaidi ameingia katika madeni ambayo hayalipiki. Kila siku wadai wanagonga hodi kwake na kwa mwajiri wake kudai pesa zao. Ian anahangaika kujitoa katika madeni haya lakini anashindwa.

Kwa upande mwingine, Ian hakuwahi kuwa na imani na washauri wa masuala ya kifedha. Alikuwa anawabeza na kuwaona kama hawana msaada wowote katika ustawi wa uchumi wake. Lakini kwa hali aliyofika, akaamua kuwajaribu.

Akatafuta mtaalamu, akamlipa gharama ya ushauri kisha akamweleza hali yake ya madeni. Baada ya kujieleza kwa muda mrefu mshauri akamwambia, amuandikie mapato na matumizi yake yote ya mwezi. Ian alifanya hivyo na mshauri akaona kwenye upande wa mapato kuna mshahara pekee, lakini kwenye matumizi kuna vitu vingi sana.

Matumizi yalikuwa na vitu vya lazima na vingine visivyo vya lazima. Mshauri akavutiwa na kitu kimoja tu katika matumizi. Kodi ya nyumba.

Mshahara wa Ian ni milioni moja, lakini analipa kodi ya Sh400,000 kwa mwezi. Hii ina maana Ian analipa kodi ya Sh4.8 milioni kwa mwaka.

Mshauri akazungushia duara kwenye kodi ile. Akamwambia Ian kuwa tatizo limeanzia pale. Ian hakumwelewa mshauri.

Mshauri akamwambia, bila kubadilisha upande wa matumizi, hali yako itakuwa mbaya kuliko sasa. Pamoja na kwamba matumizi mengi siyo ya lazima, leo tutafanyia kazi matumizi ya kodi ya nyumba.

Ian akauliza kwa shauku, una maana kuwa matumizi haya ni makubwa? Sio makubwa tu bali ni makubwa sana, mshauri akamjibu. Gharama ya kodi kwa mwaka haipaswi kuzidi mshahara wako wa miezi miwili, mshauri akaongeza.

Ian akastaajabu kwa muda, kisha akamwambia mshauri kuwa hajamwelewa. Mshauri akamwambia, ili utoke katika changamoto za madeni unatakiwa kutumia mshahara wako wa mwezi mmoja kulipia kodi ya miezi sita ama zaidi.

Baada ya kumweleza hilo, akamwambia aende akafanyie kazi hilo. Kwa shingo upande Ian aliondoka na kuona kama pesa yake kwa ajili ya ushauri ameitoa bure.

Lakini kutokana na hali ya madeni aliyokuwa nayo, hakuwa na jinsi, akafanyia kazi. Ian akahama nyumba ya aliyokuwa anakaa na kuhamia ya Sh150,000.

Columnist: Mwananchi