Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mo Dewji amewekeza Young African?

Yanga Mo Dewji Mo Dewji amewekeza Young African?

Thu, 29 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Binafsi navutiwa sana na sanaa ya uongeaji ya Ahmed Ally, amekuja kutupa ladha tofauti kutokana na kinywa chake katika vipaza sauti vya waandishi wa habari.

Kuna namna Ahmed kama Msemaji wa Taasisi kubwa ya kimpira Tanzania na Barani Afrika anaikosea heshima klabu yake kwa nini?

Binafsi nimeifuatilia press yake ambayo lengo lilikuwa ni kuzungumzia mchezo wa Simba vs Jwaneng Galaxy kwa Mkapa lakini cha kusikitisha maudhui karibia 80 yameizungumzia Yanga.

Kuna sehemu amesema mafanikio ya Yanga anayepaswa kupongezwa ni Mo Dewji hebu tujiulize kwa lipi?

1. Mo Dewji amesimamia mfumo wa Mabadiliko wa Young Africans? 2. Mo Dewji amewekeza Young African? 3. Mo Dewji amehusika katika kusajili Quality player na proper management?

Totally wrong, pengine alikuwa katika ku-set agenda ili kuhuisha nguvu na furaha ya Mashabiki wa Yanga baada ya kufuzu robo fainali.

Angetumia hata mitandao yake ya kijamii lakini cha ajabu na kusikitisha hizo pongezi zimewekwa mpaka katika ukurasa rasmi wa timu.

Unaweza usione madhara yake na ukachukulia utani ila unaendelea kumpa mileage mwenzako wakati wewe una Mambo ya Msingi ya Kufanya.

Simba ana mchezo muhimu wa kuamua hatma yake kimataifa kulikuwa na haja press kuzungumzia Yanga na kufuzu kwake?

Kuna la kulitafakari.

Columnist: www.tanzaniaweb.live