Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mmemsikia Kaze..! kwa mafundi hawa kazi mnayo

Kazee Pic Data Mmemsikia Kaze..! kwa mafundi hawa kazi mnayo

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelMore by this Author HUKO mtaani mashabiki wa soka hasa wa Simba na Yanga wamekuwa wakitaniana wakitambia safu yao na mabenchi ya ufundi, Simba ikitambia ujio wa Didier Gomes na Milton Nienov, lakini watani wao wakiwacheka wamejaa wazee tofauti na wao.

Yanga wanasema hivyo baada ya Kocha Cedric Kaze kuwa na umri wa miaka 41 tu, lakini akiwa amezungumzwa na wasaidizi vijana akiwamo Msaidizi wake Nizar Khalfan, Vladimir Niyonkuru anayenoa makipa na Edem Mortotsi aliyetua kikosini sambamba na Nizar.

Kumbe kuundwa kwa benchi hilo la mayanki kimemkuna mpaka Kaze mwenyewe aliyeamua kufunguka na kudai benchi lao lililojaa mafundi litongeza chachu kwa kikosi chao na kuwapa shida sana wapinzani wao katika mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho (ASFC).

Kaze alisema amefurahishwa na klabu hiyo kuwaajiri kwa Nizar na Mortotsi akisema kuna manufaa makubwa kwa benchi la ufundi na Yanga itakuwa ikiupiga mpira mwingi wa kisasa kuliko awali kwa kwa soka kisasa linahitaji makocha vijana wanaoenda na kasi ya mabadiliko ya kisayansi.

Nizar aliyekuwa African Lyon ameongezwa benchi la ufundi kutumikia nafasi ya kocha msaidizi kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyejiweka kando kwa matatizo ya kiafya, huku Mortotsi, raia wa Ghana, akiajiriwa kama kocha wa viungo kuziba nafasi ya Riedoh Bardien kutoka Afrika Kusini aliyetimka zake klabuni hapo kimyakimya.

Columnist: mwanaspoti.co.tz