Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mipakani tusjisahau maambukizi ya corona

Fdf013d53a5fb29ad57f9674966f5108.png Mipakani tusjisahau maambukizi ya corona

Tue, 15 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHUGHULI zinaendelea kama kawaida katika eneo la Sirari lililoko mpakani mwa Tanzania na Kenya. Zamani, wananchi wa eneo hili wilayani Tarime mkoani Mara walikuwa wakitembeleani sana lakini sasa hali ni tofauti kutokana na janga la corona.

Takwimu za jana zilikuwa zinaonesha kwamba Kenya ilikuwa na matukio ya watu 91,526 walikwishapata maambukizi ya ugonjwa wa cororona (COVID-19).

Idadi ya watu walioaga dunia kutokana na janga hilo nchini humo hadi jana ilielezwa kwamba ni 1,586, huku ya wagonjwa waliopona ikifikia 72,596. Lakini Tanzania haina hata mgonjwa mmoja wa corona kwa sasa.

“Mimi ni mfayabaishara hapa mpakani. Kwa sisi watu wa mpakani ilikuwa ni kawaida kuvuka kwenda kule na wao kuja huku kwetu lakini kutokana na corona, hatuwezi tena kwenda kule. Lakini wakaidi wanapita pamoja na vikwazo vilivyowekwa ingawa si rahisi sana,” anasema Jacob Marwa, mfanyabiashara wa samaki Sirari.

Anasema kimsingi wananchi wa maeneo hayo mawili hawaaminiani kama zamani, kwa maana kwamba wale wa Kenya hawawaamini Watanzania kwamba ingawa wanadai kwamba hakuna Korona lakini wanaficha na Watanzania hawawamini Wakenya kwa vile nchi yao bado inasumbuliwa vikali na janga hilo.

“Pale Uhamiaji kuna madaktari wa kupima virusi. Wakenya wakija huku kimsingi wanapaswa kupima na sisi tunapaswa kupima na kupata kibali kuingia kule,” anasema.

Ukiacha mpaka wa Sirari, Mara wanasema kuna njia za panya kama Kumumwamu na Motemurabu ambako anasema jamii za nchi hizo mbili hupitia, ama kwa kibali au kwa ujanjaujanja.

Kuhusu wananchi wa mpakani upande wa Tanzania wanavyojilinda na corona, Marwa anasema kwa kweli wengi akiwemo yeye hawajali sana kuchukua hatua kama ilivyokuwa wakati ikisemwa kuna corona, lakini majirani zao wa mpakani ambao bado wanasumbuliwa na ugonjwa huo anasema wengi wanavaa corona na kunawa kila mara.

Anasema kuna Wakenya wanaokuja Tanzania kwa vibali maalumu, wanapovuka mpaka wanashangaa kuona Watanzania wanavyoendelea na maisha kama kawada, wakichanganyikana, kushiriki katika hafla mbalimbali zikiwemo harusi.

“Sisi Tanzania shule zilishafunguliwa siku nyingi na wanafunzi wanasoma, lakini ukivuka tu mpaka unakuta wenzetu wanafunzi wako majumbani, shule hazijafungiliwa,” anasema Marwa.

Katika mazingira kama hayo ni vyema Watanzania wa mipakani, wakazidisha umakini dhidi ya ugonjwa wa corona kwa kuchukua hatua zote madhubuti zinazosaidia kuzuia maambukizi mapya ya ugionjwa huo hatari unaondelea kutikisa dunia.

Ni vyema wananchi wa mipakani, hususani mashule tahadhari za kama kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni zikaendelea kuchukuliwa huku wanawanchi wakiepuka kuchanganyikana na wageni na hata kuvaa barokoa pale inapobidi.

Tusipuuze pia kujihadhari na corona tunapokutana na wageni katika viwanja vya ndege na kwenye mbuga za wanyama pamoja na Mwenyezi Mungu kuibariki nchi yetu dhidi ya ugionjwa huo hatari.

Columnist: habarileo.co.tz