Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mimba zakatisha masomo maelfu wanafunzi wa kike

58dc11180678fa6ecb5639b8949f6f14 Mimba zakatisha masomo maelfu wanafunzi wa kike

Wed, 10 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAELFU ya wanafunzi wa kike nchini wameshindwa kurejea shuleni baada ya kupata mimba au kuolewa wakati wa likizo iliyotokana na kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Wakati wanafunzi waliopo kwenye madarasa yanayokaribia kufanya mitihani ya taifa wakirejea shuleni huku waliobaki wakijindaa kuanza masomo, takwimu katika Jimbo la Kitgum zinaonesha kuwa, wasichana wenye umri wa miaka 14 hadi 16 wamepata ujauzito kati ya Machi na Oktoba, mwaka jana na kusitisha masomo.

Takwimu hizo zinaonesha kati ya wasichana hao, 780 ni kutoka wilaya ya Kitgum, 1,000 wilaya ya Lamwo, 730 wilaya ya Agago na 920 wilaya ya Pader.

Askofu wa Dayosisi ya Kitgum, Wilson Kitara wiki iliyopita alitoa onyo kwa wasichana wanaopata mimba za mapema kuwa wako katika hatari ya kupata matatizo mbalimbal ya kiafya wakati wa ujauzito na kujifungua.

Huko Kabale, Ofisa Mkuu wa Ustawi wa Jamii, Monica Nzeirwe alisema katika vituo mbalimbali vya afya katika wilaya hiyo wasichana wenye umri wa miaka 15 na 19 zaidi ya 1,014 wamebainika kuwa wajawazito kati ya Januari na Septemba, mwaka jana.

Alisema umasikini, wazazi kupunguzwa kazi kutokana na janga la corona, ni miongoni mwa sababu za wasichana hao kupa ujauzito na kuolewa katika umri mdogo.

“Karibu nusu ya wasichana wanaotakiwa kurejea shuleni hawataweza pale shule zitakapofunguliwa kutokana na kupata ujauzito na kuolewa,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Uganda (Unatu) wilaya ya Kibuku, Samuel Kyaide alisema wasichana 200 wanaotakiwa kurejea shule wamepata ujauzito katika wilaya hiyo wakati wa likizo hiyo, huku Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibuku akisema wasichana 20 katika shule hiyo wamepata ujauzito.

“Nimetaarifiwa kuwa wasichana 20 wana ujauzito hivyo hawataweza kurejea shule ingawa Wizara ya Elimu imeruhusu wanafunzi wajawazito kurejea shule na kuendelea na masomo,” alisem

Columnist: www.habarileo.co.tz