Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mimba na ukatili ni mambo yaliyoshamiri kipindi corona

Mz.webp Mimba na ukatili ni mambo yaliyoshamiri kipindi corona

Thu, 18 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

• SAUT yabuni dawati; RC, wadau wanena

UGONJWA wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona ya (Covid -19), umetajwa kuwa changamoto kwa sekta ukatili wa kijinsia na hasa dhidi ya kinamama.

Kwanini? Jibu ni kwamba inatokana na wanafamilia kutumia muda mrefu wakiwa pamoja, ikitajwa inaibuka katika sura ya pili kuongezeka ukatili wa kijinsia.

Ni katika orodha hiyo kuwa changamoto ya ukatili wa kijinsia kingono na hasa mabinti, kutokana na ukweli kwamba hawapo shuleni kwa muda na wanatarajiwa kurejea masomoni siku 11 zijazo.

Hivyo, miezi mitatu ya maisha tofauti na waalivyozoea, imebainika kuwapo kundi la watoto waliojiingiza kwenye vitendo vya ngono tena ‘zembe’, jambo linalohatarisha kuongezeko mimba za utotoni na hata , magonjwa ya zinaa, ikiwamo Ukimwi.

MDAU ANAELEZA

Akizungumza na Nipashe ofisini kwake, katika Siku ya Maadhimisho ya Afya ya Wanawake Duniani Mei 28, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Kutetea Wanawake na Wasichana la Haki Zetu, Gervas Evodius, anaorodhesha changamoto za corona.

Pia, anasema watu wamejikita zaidi kupambana na ugonjwa huo, huku wakisahau upande mwingine wa afya, ama mimba za utotoni au zisizisotarajiwa zenye kawaida ya kuendana na matukio kama watoto kutupwa baadaye, pia ukatili wa kibinadamu.

Anasema wasichana na wavulana, wanahitaji usimamizi thabiti kutoka kwa wazazi wawili na jamii, pia ulinzi dhidi ya ukatili, ikiwa ni wakati muafaka wa kuzungumza nao njia bora za kujikinga na ngono mapema, wakipatiwa elimu zaidi ya afya ya uzazi na makuzi.

Evodoius anahimiza wakati ambao watoto hawapo shuleni, wazazi wanapaswa kutumia fursa ya ukaribu nao, wakijadili mabadiliko ya miili yao, hedhi salama ikaoanishwa na uelewa wa kuwapo Wiki ya Hedhi Salama, ambayo nayo imeshapita.

Katika hilo anasisitiza kinababa ambao baadhi yao ni adimu majumbani, wawe na muda wa kutosha kuongeza mapenzi kwa wenza wao na sio kuendeleza ukatili.

“Tunatakiwa kufahamu kwamba ukatili wa kijinsia unaathiri familia nzima na jamii nzima kwa ujumla, kwa hiyo ni vita ambayo sote tunatakiwa kushiriki katika kuvitokomeza,” anasema Evodius.

CHU0 KIKUU SAUT

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT), jijini Mwanza, Balozi Prof. Costa Ricky Mahalu, akifungua ‘Dawati la Changamoto za Kijamii’ chuoni hapo alikumbusha unyanyasaji wa aina yoyote.

Kwa mujibu wa Prof. Mahalu, ukiukwaji wa haki za binadamu ulishatamkwa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948, kwamba binadamu wote wamezaliwa wakiwa uhuru sawa, katika masuala ya utu na haki.

Mtaalamu huyo anasisitiza kukabili unyanyasaji na uhusiano wake na ulinzi wa haki za binadamu, jambo ambalo mataifa duniani yako mstari wa mbele kuyatatua, ili kuwaletea haki na usawa wananchi wote.

Uamuzi wa chuo kikuu hicho kuanzisha dawati, unaelezwa unalenga kugusa changamoto nyingi za kijamii. Hapo zinaorodheshwa;unyanyasaji kingono, mabavu, kisaikolojia na kijinsia .

RC & WADAU

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, anakiasa Chuo Kikuu cha SAUT litumie dawati kuleta amani na vitendo vya ukatili visitumike kama mahakama.

Pia, anazungumzia suala la afya, akifafanua kwamba wamekuwa wabia na taasisi anayoitaja ya Aga Khan Develop Network na kunafanikisha majengo 28 ya vituo vya afya sehemu mbalimbali nchini, kumhuduma mama na mtoto.

Mdau wa harakati hizo, Simoni Chemu, anasema ni wakati muafaka familia zikaungana kiimani, ili kupata uponyaji unaowapa mapungfu ya kijamii yaliyotajwa, pia kuwarejesha amani wawe nje ya maovu.

Ni mawazo yanayoungwa mkono na mdau mwenza, Husna Kambarage, anayesema, jamii inapaswa kuungana kupinga yanayovunja amani hasa katika malezi, ili kupata mbadala wa upendo unaoelimisha watoto afya ya kujitambua na kuwajengea maarifa .

MTAALAMU & MCHUNGAJI

Lugodisha George, Mtaalamu na Muwezeshaji wa Huduma za Afya ya Uzazi wa Kujitegemea, anautaja ukatili ulivvyo ni pale binti anapata ujauzito, fursa zake nyumbani zinapotea ana anangukia changamoto kama kufukuzwa shule na nyumbani.

Ni hali mtaalamu huyo anayoeleza inaendana na hali kama ya kukimbiwa na mwanaume aliyempatia ujauzito, jamii inamtenga, binti anahamia mtaani anakoshidwa kupahimili, akiangukia athari kama kujifungua mtaani, kutoa mimba au kuwa kahaba.

Anataja chanzo kikuu, ni kwamba kasoro ya wazazi wanaposhindwa kuwa karibu kuwaandaa watoto, hawawapi elimu sahihi kuhusu maisha, hawapunguzi kuwanyanyasa au kuwajengea uwezo wa kimaendeleo.

“Hakika afya ya uzazi imepunguza maambukizi ya magonjwa mbalimbali pamoja na kushamiri kwa utoaji wa mimba mitaani,” anasema George.

Mwenyekiti wa Umoja wa Makanisa Mwanza, ambaye ni Askofu wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (AICT), jijini Mwanza, Philipo Mafuja, anawaelekezea nasaha Watanzania kuomba waondolewe janga la kirusi Covid – 19, inayoendana na majanga kama kushuka uchumi na ukatili katika jamii.

Anakiri harakati za kujilinda na kujiepusha, kupitia imani za kidini umma unapaswa kubadilika na kuchukua tahadhari za kupambana.

Juzi katika hotuba ya kulivunja Bunge jijini Dodoma, Rais Dk. John Magufuli, alirejea kuwashukuru viongozi wa dini, kwa mchango wao wa kiimani, katika kupiga vita maradhi ya corona.

Columnist: www.tanzaniaweb.live