Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Milima, mabonde mitandao ya kijamii

Simu Ni Hatari Kwenye Mapenzi, Ziepukeni Hivi . Milima, mabonde mitandao ya kijamii

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: mwanachidigital

Uvujishaji wa taarifa za watu upo zaidi nje mtandao kuliko mtandaoni, ikiwemo matokeo ya mtihani na majibu ya afya ambayo makaratasi yake yanafungiwa maandazi na chapati.

Majibu ya hospitalini yanatumika ndivyo sivyo watu wanakutana na karatasi za afya za watu huko mtaani, ukiangalia taarifa za mtu binafsi si nani anatembea na nani bali taarifa zinazolinda utu wake.

Hayo yamesemwa Desemba 13,2023 na Mkurugenzi wa Jamii Forum, Maxence Melo wakati akichangia mada kwenye Mwananchi Space iliyoandaliwa na Mwananchi Communications Limited (MCL) ikibebwa na mada isemayo ‘Nini mchango wa mitandao ya kijamii katika kufichua taarifa kwa umma.

"Nimekuwapo eneo hili kwa muda mrefu nadhani tangu mwaka 1999, nimeona mengi, tumepuuzwa sana mwanzoni, tulikuwa tukisema tuko mtandaoni tunajadiliana walikuwa wanaona kama tuko kwa ajili ya kutongozana," amesema Melo.

Amesema mwanzoni wakati wanaanza walipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa wamiliki wa vyombo vya habari walikuwa wakipinga, Serikali, wanasiasa walikuwa wanaona kinachokuja kitakuwa kigumu kwa sababu ni rahisi kwa wanasiasa wenye nguvu kifedha, watu watoa rushwa au wenye akili za kifedha kununua wanahabari au chombo cha habari.

Amesema ni rahisi kununua wanasiasa wa chama cha upinzani lakini fedha hizo haziwezi kununua wana mitandao wote kwahyo mitandao imekuja kubadilisha mambo.

Amesema uhuru wa mitandao ambao unaupimwa sasa hivi ndiyo ulioleta uwajibikaji ambao unaonekana lakini umekuja kwa baadhi ya watu kutoka jasho wengine damu.

"Mitandao ya kijamii na digitali kwa ujumla wake imetoka mbali imepitia milima, mabonde, kona kadhaa tumezikata, tumefanya vyema lakini tulipofika mitandao ina nguvu,"amesema.

Akitolea mfano Melo amesema kunguni waliokuwapo Chuo Kikuu cha Dodoma ingekuwa mwandishi ameenda kuhoji, stori ingeishia palepale lakini ilivyotolewa mitandaoni hatua zikachukuliwa.

Amesema ikumbukwe kama Azory Gwanda ambaye hadi sasa hajulikani alipo, ingawa kuna Waziri aliwahi kusema aliuwawa, pia kuna mwanahabari aliuwawa na askari polisi na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Iringa alisema waliofanya hivyo ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ndiyo walimuua kwa kitu chenye ncha kali.

Amesema bahati nzuri, picha ya tukio zima ilipigwa na kupandishwa Jamii Forum kupitia mtu wao wanayemuamini aliyehakikisha kuwa alikuwa eneo la tukio na ilisaidia hatua zichukuliwe, lakini upotoshaji ulikuwa umeshaanza na kwa sababu yeye ndiye mwenye mamlaka waandishi wengine wangelazimika kuandika kuwa wafuasi wa chadema wamemuua mwandishi wa habari kwa kitu cha ncha kali.

"Mitandao ya kijamii inatoa taarifa ila isipowalinda watoa taarifa hii inaweza kuwa nafasi hatarishi kwa wananchi pia inaweza kuwaumiza wengine,"amesema Melo.

Kwa upande wake, Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii, Faraja Kristomus amesema mitandao ya kijamii inaweza kutumika kama wafichua maovu, wakati mwingine kuna jambo nyeti na hatari kwa jamii linafanywa na kikundi fulani la waovu wana mipango ya kiovu inafanyika.

Amesema huenda wakubwa wa Serikali wasijue lakini mitandao ya kijamii inatoa nafasi ya kufichua ovu ambalo linapangwa kutendeka na likawa jambo zuri kwa Serikali na ustawi wa Taifa au manufaa kwa Taifa.

Mbali na kufichua maovu amesema kuna fursa zinapatikana huko, watu wengi wanaweza wasifikiwe lakini ikitangazwa mtandaoni mtu anaona kumbe anaweza kutumia fursa hiyo akabahatika kutuma zabuni akafanikiwa.

"Kwa jicho lingine mitandao ina matatizo yake kwa sasa hivi imekuwa kama tabia wanasiasa kuumizana mitandaoni ya kijamii, kwa ustawi wa siasa ni changamoto kwani si tu kufichua bali kuchafuana kwani imefika mahali si tu kufichua maovu kumbe tunatengeza maovu ya uongo yasiyo halisia," amesema Kristomus na kuongeza kuwa.

"Tunasema tunafichua maovu ya mtendaji fulani kumbe nyuma yake tunakuwa na ajenda ya kuharibiana tumeshuhudia hilo kwa wanasiasa kadhaa wakiwa wanachafuliwa kwa kusingizia kuwa wanaweka wazi maovu yao ila ukifuatilia si kweli."

Amesema hali hii kuelekea uchaguzi mkuu kuna hatari kubwa zaidi ya kufichua maovu ya wanasiasa kikawa kichaka cha kuharibiana kisiasa na kibiashara pia.

Mchangiaji, Clay Mwaifwani amesema shida kubwa ni wanaotakiwa kuwajibika hawawajibiki, wanaopaswa kuwawajibisha wasiowajibika hawawajibishi, kumekuwa na jitihada za dhati za kuibua taarifa lakini watu wanaotakiwa kushughulika na taarifa hizo wamekuwa wakitumia namna inayofanya taarifa hizo zionekane hazina maana.

Amesema wanawavunja moyo waleta taarifa, wanawatisha, ikumbukwe Bob Chacha wangwe baada ya kutoa maoni baada ya uchaguzi mkuu alifunguliwa kesi, mwaka 2018.

"Kama sikosei kuna wakati huo wakiwa chama cha upinzani kina Joshua Nassari na baadhi ya viongozi wa Chadema walikuwa na ushahidi wa matukio ya rushwa wanashawishiwa kwa vitendo ambavyo kwa mujibu wa vitendo vya kuzuia na kupambana na rushwa ni makosa,"amesema Mwaifani.

Amesema walirekodi vile kwa kutumiwa vifaa kwenye mashati, kalamu, walikuwa na ushahidi kuwa watumishi wa mamlaka za umma wamewashawishi kwa kuwaahisi kuwafanyia vitu ambavyo ni rushwa

Kwa mujibu wa Mwaifani amesema taarifa zile walipozipeleka Taasisi ya Kuzia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) na Mamlaka zingine wakaanza kuzizungumza na mitandaoni mamlaka za umma na Jeshi la Polisi wakasema waache kuongea ongea watashughulikia bila kuathiri ushahidi.

Mtu anaibua maovu makubwa ya rushwa ya maofisa wa juu ya watumishi wa umma mwisho wa siku wanapewa vitisho na hili linakatisha tamaa wengine kuibua vitu vya namna hii.

Columnist: mwanachidigital