Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Migogoro ZFF inaathiri utendaji wa Bodi

09927ec0166b4f5c4301e5a33c128b4b Migogoro ZFF inaathiri utendaji wa Bodi

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

IMEELEZWA kuwa kuendelea kwa mgogoro ndani ya Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) kunachangia kuathiri utendaji wa Bodi ya Ligi Zanzibar.

Hayo yalisemwa na Mjumbe wa Bodi hiyo, Mohammed Masoud alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za ZFF Amaan mjini hapa jana. Alisema mgogoro huo umekuwa ukiwaathiri sana hali ambayo inawapa shida katika upatikanaji wa fedha kwa bodi hiyo.

“Jamii inapaswa kujua msuguano ambao upo kwa muda mrefu unasababishwa na kamati ya utendaji ambayo inaonekana bado haijawa tayari kumaliza migogoro yao.”

“Sisi Bodi hatutakiwi kuingilia lakini tulitakiwa kujua kwa sababu sisi ndio wenye dhamana ya mpira na wengine wana dhamana ya uongozi, hivyo sisi katika kipindi hiki tumefikia dirisha dogo lakini upande mmoja hakuna ligi iliyoendelea,” alisema.

Alisema pamoja na kuwa bodi inafanya kazi vizuri lakini inaongoza ligi upande mmoja ambao sio sahihi kwani upande mwengine imesimama lakini hakuna hatua ambazo zimechukuliwa. Masoud alisema kila mmoja ni shahidi kuwa ligi katika kisiwa cha Unguja inaendelea, lakini kwa upande wa Pemba hata usajili haujafanyika.

Aliitaka Kamati ya Utendaji iwajibike na kujiuliza kwanini ligi inachezwa upande mmoja na upande mwengine haichezwi wakati kanuni za mashindano na ratiba zote ni moja na hakuna ligi mbili katika nchi moja hasa ligi kuu.

Columnist: habarileo.co.tz