Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Miaka 60 ya TANESCO ya kuliangaza Taifa

Tanesco Iii Tanesco: Miaka 60 ya kuliangazia Taifa

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: mwananchidigital

Septemba 25, 2021 kulijitokeza mabadiliko makubwa katika shirika hilo, si tu katika usimamizi wa juu bali pia katika idara kuu za Wizara ya Nishati.

Rais Samia Hassan Suluhu alimteua Omari Issa kuchukua nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo. Alimteua pia Maharage Chande kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanesco, akichukua nafasi ya Tito Mwinuka.

Wiki mbili kabla ya uteuzi huo, Rais Samia alikuwa amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ambalo alimteua January Makamba kuwa Waziri wa Nishati. Baada ya uteuzi wake waliteuliwa wajumbe wapya wa bodi ya wakurugenzi ya Tanesco kutoka sekta binafsi.

Alipokuwa akihutubia wafanyakazi waandamizi wa Tanesco wakati alipowasilisha bodi mpya na menejimenti Septemba 26, 2021, Makamba hakumumunya maneno pale alipoitaka Tanesco kuzaliwa upya.

Makamba pia aliwaambia mameneja wakuu kuwa ni wakati wa Tanesco kufanya biashara kwa ufanisi ili kuongeza mchango wake kwa uchumi wa kitaifa.

Watoa maoni na wanamtandao walitikisa ndimi zao kuitikia mabadiliko ya Tanesco. Ingawa kulikuwa na wasiwasi wa kweli katika maoni yaliyotolewa katika mitandao ya kijamii kuhusu kama timu mpya itaweza kubadilisha kile kinachoonekana kuwa ni kupotea njia, na upotevu mkubwa wa kifedha wa Tanesco unaweza kudhibitiwa (kulikuwa na hasara ya Sh112.5 bilioni katika mwaka ulioishia Juni 2018), na wengine walidai kuwa mabadiliko hayo yalichochewa sababu za kisiasa.

Baadhi ya waliotoa maoni waligundua athari za maneno ya Makamba juu ya iwapo uteuzi wa timu inayomaliza muda wake iliyoteuliwa na mtangulizi wa Rais Samia ulikuwa wa kisiasa. Na bado matumaini ya waliotoa maoni yalidai kwamba mabadiliko hayo yanaweza kuwa ni njama za kurudi kwa mafisadi ambao walisababisha hasara kubwa kwa Tanesco siku za nyuma.

Licha ya kuwapo kwa maoni tofauti kuhusu ‘mabadiliko mapya’ ya Tanesco ni busara kubeba kauli ya Makamba. Angalau ahadi zake za kuondoa siasa katika shirika hilo zinalingana na uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji na bodi ya wakurugenzi. Karibu wote ni kutoka sekta binafsi; wachache miongoni mwao wana uzoefu mbalimbali katika sekta binafsi na za umma.

Kuhusu Omari Issa, wasifu mmoja unasema mwenyekiti mpya wa Tanesco: “Ana uzoefu mkubwa wa kibiashara wa kiwango cha juu zaidi katika sekta za umma na za kibinafsi, kwa sababu amefanya kazi Afrika, Asia, Ulaya na Amerika Kusini.”

Issa alifanya kazi kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji wa Hali ya Hewa kwa Afrika (ICF) na kama mkurugenzi mtendaji na afisa mkuu wa uendeshaji wa Celtel International, ambayo baadaye ilibadilisha umiliki na majina na kwa sasa inajulikana kama Airtel.

Lakini Issa pia ana uzoefu mkubwa na mashirika ya kimataifa kwa sababu alifanya kazi kwa miaka 20 na Benki ya Dunia, miaka 14 na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) na miaka sita na Benki ya Dunia.

Wachunguzi wengine wanasema kuwa ni jambo la kushangaza kwamba miaka 60 baada ya uhuru Serikali bado inatafuta kufanya mabadiliko ya kimsingi kwa shirika ambalo mchango wake kwa uhai wa nchi hauelezeki.

Wanasisitiza kuwa mabadiliko hayo, ingawa ni yamekuja wakati unaofaa na yanaonekana kuwa na nia njema kwa Tanesco, yalipaswa kufanyika miaka 30 iliyopita wakati nchi, ikiwa bado ndani ya mchakato wa ukombozi wa kiuchumi, ilizindua Sera ya Nishati ya kwanza kabisa au mwaka 2003 wakati Serikali ilipozindua Sera ya pili ya Nishati ambayo lengo lake lilikuwa ni kurekebisha soko la nishati na kuvutia ushiriki wa sekta binafsi katika sekta ya nishati. Sera ya 2003 ndiyo iliyoweka msimamo wa sera ya kuiajiri NETGroup Solutions (Pty) Ltd ya Afrika Kusini kuisimamia Tanesco tangu 2002 hadi 2006.

Mchambuzi aliyezungumza na gazeti la Mwananchi kwa masharti ya kutotajwa jina alisema wanaodhihaki au kuisema vibaya timu hiyo mpya hawaoni ukweli.

Alisema mabadiliko katika usimamizi yanafanikisha malengo ya baadaye ya shirika na, labda hata uhai wa CCM kama chama tawala. “Nakubali kuwa mabadiliko katika Tanesco ni hatua ya kusonga mbele ya ‘kuondoa siasa’ katika hili shirika la umeme, lakini tunachopaswa kuelewa ni kwamba uamuzi wenyewe wa kuondoa siasa katika uendeshaji wa Tanesco ni wa kisiasa,” mchambuzi huyo alisema.

Alisema kwa kuteua watu ambao wamefanikiwa sana katika sekta binafsi Serikali imeongeza matarajio kwa wadau ambao ni muhimu zaidi; sekta binafsi, washirika wa maendeleo na nia ya watumiaji binafsi wa huduma za Tanesco.

“Uhalisia wa uteuzi hautapimwa na CV za wajumbe wa timu mpya. Utapimwa na matokeo. Ikiwa Tanesco itaendelea kupata hasara au ikiwa inarudi katika kashfa kubwa za ufisadi, basi watu wataangalia nyuma na kuona nia mbaya katika uteuzi huo,” mchambuzi huyo alibaini.

“Kugawanya shirika la umeme katika vyombo vitatu (uzalishaji, usafirishaji na usambazaji) ni wazo ambalo lilielea muda mrefu uliopita. Kila mwangalizi makini wa masuala ya nishati anahisi kuwa huwezi kuanza kufikiria kuifufua Tanesco katika muundo wake wa sasa,” alisema.

Sera ya Kitaifa ya Nishati ya mwaka 1992 iliifungua sekta ya nishati kwa washiriki binafsi katika maeneo kama vile uzalishaji wa umeme. Sera hiyo iliruhusu kampuni za binafsi kushiriki katika usambazaji wa umeme tu katika maeneo ambayo Tanesco haikuanzisha mfumo wa usambazaji umeme.

Kudumaa?

Tanesco ni miongoni mwa taasisi kongwe nchini. Historia yake inaonyesha kuwa kazi zake zimekuwa zikifanyika kwa miaka 90 iliyopita kwani zilianza mwaka 1931, ikiwa ni miaka 30 kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Inaeleweka kwa kawaida kuwa wakoloni hawakuwa na mpango wa kuwafundisha Waafrika kubeba majukumu ya kitaalamu baada ya uhuru lakini kumbukumbu za taasisi tangu uhuru ilipaswa kuifanya Tanesco kuwa miongoni mwa watoa huduma bora zaidi barani Afrika. Tatizo pekee kama wachambuzi wanavyosema ni siasa na uwekezaji.

Suluhisho

_Uchambuzi wa Swoc wa Tanesco (uwezo, udhaifu, fursa, changamoto) unaonyesha kuwa suluhisho la matatizo ya Tanesco hayapaswi kutoka ndani bali kutoka nje.

Kuongezeka kwa ufanisi kutoka kwa timu bora ya usimamizi kutasaidia kuboresha na kupanua usambazaji wa umeme lakini haiwezi kumaliza ubora duni wa umeme unaosambazwa au hasara ya kila mwaka ya shirika.

Wakati suluhisho nyingine za nje kama ukosefu wa fedha za kuhudumia shughuli za utendaji na maendeleo ni rahisi kupata, nyingine ni ngumu sana. Inahitaji ujasiri wa ziada na dhamira ya kisiasa ya kushughulikia.

gharama kubwa za tozo za umeme katika makubaliano ya uzalishaji wa umeme na ufisadi, ambayo yameorodheshwa katika mpango wa ushirika wa Tanesco kama udhaifu na changamoto kwa shughuli zake.

Columnist: mwananchidigital