Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mchukie Kipanya, heshimu hustles zake!

FB IMG  Kipanya He Mchukie Kipanya, heshimu hustles zake!

Sun, 23 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ally Masoud 'Kipanya', naweza kuwa simpendi na sidaiwi kumpenda. Jambo moja ni uhakika, naheshimu akili yake na uwezo ambao ameudhihirisha kwenye jamii. Miongo mitatu sasa.

Wajiji husema "you don't respect me, respect my hustles" - "huniheshimu mimi, heshimu mitikasi yangu."

Unanipata mwana? Naweza kuwa simheshimu Kipanya, ila naheshimu mitikasi yake.

Hiyo ndio ari ambayo mtu yeyote timamu anapaswa kuwa nayo. Maisha ni rahisi mno kama utajifunza na kujizoesha kuheshimu mitikasi ya wengine.

Aprili 2022, Kipanya alifanya kile ambacho Mohammad Ali alikiita "to shock the world". Alizindua gari alilobuni na kuliunda mwenyewe.

Kipanya, mwanahabari, cartoonist unaweza kumwita, sio mhandisi, ila utundu na uthubutu wake viliwezesha aunde gari lenye kutumia umeme. Nchi iliduwaa.

Ni vile Tanzania, watu wake wengi hawakujaliwa nidhamu ya kuthamini na kushukuru, vinginevyo Kipanya angebebwa na kunadiwa kama superhero wa ubunifu Afrika Mashariki.

Vijiweni na mitandaoni kuhusu ubunifu wa Kipanya: "kagari gani kale? Nani atanunua? Niache kununua kirikuu kutoka Japan ninunue kagari ka Kipanya nina wazimu? Kipanya kasomea uinjia wapi na lini?"

Kali zaidi, ndani ya vikao vya uamuzi serikalini, imevuja sauti. Bosi mmoja anasema gari la Kipanya lilinunuliwa dola 600 China (Sh1.4 million). Kipanya akawadanganya Watanzania kuwa ameunda gari. Bosi huyo akasema Kipanya ni mhuni tu!

Hao ndio binadamu. Wivu, inda, unafiki, husuda, vijicho ni matawi ya roho mbaya.

Waza, Kipanya akipata mtaji mkubwa na teknolojia bora ataunda gari lipi? Ikiwa kwa kuungaunga ameshatoa kitu.

Unga mkono juhudi za kibunifu ili wabunifu wengi wajitokeze. Nchi ipendeze. Uchumi ukue. Sio kuwakaba wabunifu au kuhamisha goli wasifunge.

Ubunifu ni sanaa. Engineering ni taaluma. Unaweza kuwa na weledi mkubwa kiuhandisi, ukakosa sanaa. Kipanya ni msanii.

Badala ya wahandisi kumchukia Kipanya, ni fursa ya kushirikiana.

Ninyi wataalamu, ingizeni utaalamu kwenye ubunifu wa Kipanya ili KP Motors izalishe magari bora na yenye kuvutia zaidi. Sio kukandia. Roho mbaya ni kirusi.

Huingii gharama yoyote kuheshimu mitikasi ya kibunifu ya Kipanya.

Ndimi Luqman MALOTO

Columnist: www.tanzaniaweb.live