Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mchambuzi Kimataifa: Tanzania ina mazingira bora ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

Add3b9be0abf329f5c6928431a2ebf0c Mchambuzi Kimataifa: Tanzania ina mazingira bora ya amani kuelekea Uchaguzi Mkuu Oktoba 28

Thu, 24 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MWANATAALUMA wa masuala ya usalama, Profesa Richard Andes, amesifu amani iliyopo nchini kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Prof Andes amesema hayo yamewezekana kutokana na kila chama kukubali na kusaini fomu za maadili zilizotolewa na Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) kuelekea uchaguzi huo, ikiwa inalenga kuwapo kwa amani kabla na baada ya upigaji wa kura.

Kila chama chenye usajili wa kudumu kilitia saini makubaliano hayo yanayolenga kipindi hiki chote cha kampeni pamoja na siku ya kupiga kura.

“ Ninafurahi kutambua kuwa kila chama na kila mgombea alisaini fomu za maadili. Ninafurahi kuona kuwa kampeni zinafanyika kwa utulivu na amani,” amesema.

NEC ilitoa fomu za maadili kwa lengo la kuhakikisha kuna usawa, maelewano, pamoja amani wakati wote mchakato wa uchaguzi mkuu ukiendelea.

Columnist: habarileo.co.tz