Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mbowe kaachiwa kwa kigezo kipi?

Mbowe Huruu Freeman Mbowe

Mon, 7 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKANGANYIKO; kila mtu anasema lake kuhusu mheshimiwa Freeman Mbowe kuachiwa huru kutokana na kesi ya ugaidi iliyokuwa ikimkabili.

Jambo la kuaminika kisheria ni kwamba, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) kwa mamlaka aliyopewa kisheria ndiye aliyeiondoa kesi ya Mbowe na wenzake watatu mahakamani kwa sababu ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.

Pamoja na ukweli huo ambao umetumika mara kadhaa kwa watuhumwa tofauti nchini, kuna baadhi ya watu wanatafsiri kwamba Mbowe ameshinda kesi.

Watu wengine kupita mitandao ya kijamii wanaeneza maneno kwamba, Mbowe amesamehewa na rais kupitia maombi yaliyoombwa na baadhi ya wanasiasa na viongozi wa dini kwamba mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ‘atumie busara’ kumnusuru Mbowe.

Akitoa neno lake la shukrani kanisani hapo jana, Mbowe alisema ‘nguvu ya umma’ ndiyo iliyomtoa gerezani.

Nauweka mjadala huu mezani tujaribu kuuangazia kwa mapana kwamba rais anaweza kumfutia kesi mtuhumiwa? Sheria inakataa.

Je, nguvu ya umma inaweza kumshinikiza DPP amfutie shtaka mtuhumiwa? Sheria pia inakataa.

Je, mtuhumiwa akiachiwa na DPP anakuwa ameshinda kesi au ni kama kapewa “fea” na DPP?

Karibuni wajuzi wa sheria na mambo ya kiutawala tuchangamshe fahamu zetu kwa kutoa hoja na kujibu hoja siyo povu na lugha za kukera.

Columnist: www.tanzaniaweb.live