Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Mambo saba kumfanya Mbappe kuwa staa

Mbappe 2 Goals.jpeg Kylian Mbappe

Fri, 9 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Supastaa fowadi wa Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe anatajwa kuwa mchezaji bora kabisa duniani kwa sasa na mengi yanasemwa kuhusu namna gani England itaweza kumdhibiti kwenye mchezo wa robo fainali wa Kombe la Dunia 2022 huko Qatar, keshokutwa Jumamosi.

Wakati ukiwa unawaza itakuwaje kwenye mechi hiyo, haya hapa mambo saba yanayoonyesha namna Mbappe alivyokuwa kwenye soka hadi kuwa supastaa.

1. Mchezaji ghali namba mbili

Mwaka 2017, Mbappe alijiunga na PSG, kwa mkopo kutokea Monaco kabla ya dili hilo kuwa la jumla kwa ada ya Pauni 166 milioni. Hilo limemfanya kuwa mchezaji ghali namba mbili duniani baada ya Neymar, aliyenaswa kwa Pauni 200 milioni na PSG akitokea Barcelona mwaka huohuo. Amefunga mabao 190 katika mechi 237 alizocheza PSG.

2. Ushindi kawaida yake

Katika miaka saba ya kuwa kwenye soka la kulipwa, Mbappe ameshinda Kombe la Dunia (2018), Uefa Nations League (2021), mataji matatu ya Ligue 1 (matatu PSG, moja Monaco), Kombe la Ufaransa mara tatu, Kombe la Ligi mara mbili huku akishinda pia tuzo binafsi kama Golden Boy, Mchezaji Bora Ligue 1 na Mchezaji Kijana wa mwaka mara tatu.

3. Amezoea kufunika Kombe la Dunia

Mbappe alikuwa na umri wa miaka 19 tu wakati alipoisaidia Ufaransa kushinda Kombe la Dunia 2018 huko Russia, ambapo alifunga mabao manne. Alifunga pia kwenye ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Croatia kwenye fainali na kuwa mchezaji namba mbili mwenye umri mdogo kufunga fainali kama ambavyo alifanya Pele mwaka 1958. Kwenye fainali hizi za huko Qatar, Mbappe tayari ana mabao matano.

4. Dogo mvunja rekodi

Mbappe, aliyezaliwa Paris alianza kuichezea Timu ya Mtaa AS Bondy, kabla yay a kwenda kukipiga Monaco, Desemba 2015. Akiwa na umri wa miaka 16 na siku 347, alikuwa mchezaji mdogo zaidi kwenye klabu hiyo, akivunja rekodi ya Ufaransa iliyokuwa ikishikiliwa na Mfaransa, Thierry Henry.

5. Kasi yake ni tishio

Wakati Ufaransa inashinda 3-1 kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya Poland, Mbappe alikimbia kwa 35.3 km/s. Kuna wachezaji wachache sana walioonyesha kasi hiyo ya kukimbia kwenye fainali za Kombe la Dunia. Septemba mwaka huu, aliweka rekodi kwenye Ligue 1, alipokuwa mchezaji mwenye kasi zaidi msimu huu, alipokimbia kwa 36km/s. Wakati Usain Bolt anavunja rekodi ya dunia kwenye mita 100, alikimbia kwa kasi ya 37.58km/s.

6. Aigomea Real Madrid

Baada ya kufuatwa na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez na kufikia makubaliano ya mkwanja mrefu wa kwenda kujiunga na miamba hiyo ya La Liga, Mbappe aligomea na kuamua kubaki zake Paris, akisaini dili jipya la miaka mitatu. Kwa mujibu wa Guillem Balague, mwandishi maarufu wa soka la Hispania, alisema Los Blancos ilikuwa tayari kumpa Mbappe Pauni 127 milioni kama ada ya saini yake.

7. Tajiri mtulivu

Oktoba, Mbappe alikuwa namba moja na Forbes kuwa mwanasoka anayevuna mkwanja mrefu zaidi kuliko Lionel Messi na Cristiano Ronaldo. Staa huyo mwaka huu ameweka kibindoni Pauni 115.2 milioni. Mbappe pia ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii, akiwa na jumla ya wafuasi 100 milioni kwenye Facebook, Instagram na Twitter.

Columnist: Mwanaspoti