Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Makocha 5 bora wasio na kazi na klabu zinazowafaa

4 Makocha 5 bora wasio na kazi na klabu zinazowafaa

Mon, 18 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KUWA kocha ni moja ya kazi ngumu katika soka. Kuwasimamia wachezaji wenye tabia tofauti na kujaribu kuhakikisha unapata kilichobora kutoka kwao mara zote si kazi rahisi. Ongeza hilo na presha kutoka kwa wamiliki wa klabu, pamoja vyombo vya habari visivyosamehe, kwa hakika ni kazi ngumu.

Kocha anahitaji kuipa klabu utambulisho. Wakati tunapofikiria kuhusu Pep Guardiola, tunafikiria kuhusu staili ya soka la tiki-taka. Jurgen Kloop anajulikana kwa staili ya soka la kusukumiza mashabulizi mbele, na Sir Alex Ferguson anatukumbusha soka la kushambulia kwa haraka na mashambulizi ya kushitukiza.

Zamani, alitakiwa kufanya kila kitu, kuanzia kufanya skauti ya wachezaji, usajili na udhamini. Yaani klabu ilikuwa inaendeshwa na kocha. Leo hii kazi ya kocha mkuu inahusika tu kwa kile kinachotokea uwanjani.

Hapa tunawaangalia makocha bora watano ambao kwa sasa hawana kazi na klabu bora zinazowafaa, twende sasa...

#5. Laurent Blanc

Umekuwa ni muda mrefu sasa tangu Laurent Blanc alipokuwa kocha wa Klabu. Mara ya mwisho alionekana kama kocha wa PSG, na kuwaongoza kwenye mataji matatu mfululizo ya Ligi Kuu, Blanc ni gwiji wa soka la Ufaransa, kwa pamoja kama mchezaji na kocha. Wakati muda mwingi alikuwa PSG, awali pia aliwahi kuinoa Bourdeaux. Aliongoza timu yake kutwaa mataji matatu mwaka 2008, na akapewa kazi ya kuinoa timu ya Taifa ya Ufaransa.

Msimu wake wa mwisho haukuwa mzuri kwa mujibu wa rais wa klabu, alishindwa kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Na tangu hapo hakuna kocha yeyote aliyeiwezesha PSG kusonga mbele ya hatua hiyo katika mashindano hayo.

Yeye ni aina ya kocha ambaye anaweza kuja kwenye kikosi ambacho kipo tayari kushindana kwenye mashindano makubwa, lakini bado hajakuwa hapo.

Klabu inayomfaa: Olympique Lyon

Wakati Lyon inawachezaji nyota wa kuinyanyua kama Memphis Depay, Moussa Dembele na Houssem Aouar, bado wamemaliza nafasi ya saba, na wanataka mtu atakayeweza kuwarudisha kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Blanc, kwa ujuzi wake na kulielewa soka la Ufaransa, ni mtu anayewafaa.

#4. Marcelinho

Marcelinho ni mmoja wa makocha wachache duniani ambaye anaweza zaidi kuutumia mfumo wa 4-4-2 na kupata mafanikio.

Alikuwa kwenye kiwango cha juu wakati wake pale Villareal ambapo aliwachukua kutoka ligi daraja la pili hadi kwenye nusu fainali ya Ligi ya Europa.

Pia ana jicho la kuona vipaji.Aliwauza wachezaji kama Bailly, Vietto, na Pato kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Ni kocha mwenye ujuzi, anajua namna ya kuwapata wachezaji. Msimu wake wa mwisho na Valencia, alishinda Kombe la Mfalme ['Copa del Rey'], akiifunga Barcelona kwenye fainali. Kwa mshangao, alifukuzwa baada ya mechi tatu tu msimu huu.

Uwezo wake wa kufanya kazi kwa bajeti ndogo unamfanya kuwa na uwezo mzuri wa kufundisha klabu zilizopo katikati ya msimu kuanzia 5-bora.

Klabu inayomfaa: West Ham

West Ham tayari wana kikosi kizuri kwenye karatasi. Haller, Anderson, Diop na Fornals- wote wapo tayari kusukumwa, angalau kwenye Ligi ya Europa. Pamoja na heshima zote kwa David Moyes, yeye si mtu anayeweza kufanya hivyo. Marcelinho anaweza kuwa mtu atakayeisaidia klabu hiyo kufika sehemu inayotakiwa kuwapo.

#3. Unai Emery

Kabla ya kukutana na wakati mgumu pale Arsenal, Unai Emery alikuwa na CV nzuri. Mataji matatu mfululizo kwenye Ligi ya Europa akiwa na Sevilla na mataji saba akiwa pale PSG yalitosha kuwashawishi 'Washikabunduki' kwamba alikuwa mtu sahihi kuwaongoza.

Soka la kushambulia kwa kasi ndio kitu kilichotengeneza jina la Emery. Hata pale Arsenal, kulikuwa na ishara ya hilo, lakini kutokana na safu mbovu ya ulinzi kazi ikawa ngumu kwake. Klabu ambayo ipo tayari kuamini uwezo wake itakuwa sahihi kwake.

Klabu inayomfaa: Napoli

Napoli imekuwa na msimu mbaya, huku Rais wa Klabu, Aurelio de Laurentiis akiwa ameonyesha hadharani kutoelewana na wachezaji. Wachezaji wengi muhimu kama Koulibaly na Allan wanatarajia kuuzwa kipindi cha majira ya joto kinachokuja. Wana kocha mzuri Gattuso, lakini Napoli inahitaji kocha wa daraja la juu mwenye uwezo wa kuleta ushindani kwenye Serie A kwa mara nyingine tena.

Emery anaweza kuwa kocha atakayefiti kwa klabu hiyo. Kama wakifanya usajili sahihi kuziba mapengo ya wachezaji wanaoondoka, Napoli inaweza kuwa kama Juventus, Inter Milan na Lazio endapo watatumia fedha zao.

#2. Massimiliano Allegri

Kwa kila kitu Max Allegri amefanikiwa, hapati heshima inayotakiwa. Huku akiwa na mataji sita ya Serie A, ya ligi manne na matatu ya Italian Supercups, pamoja na fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya, inatosha kusema ni kocha mwenye mafanikio sana.

Huku ikiwa inakaribia miezi 18 tangu awe hana klabu ya kuinoa, atakuwa tayari kupata kazi haraka. Timu ya Allegri inakuwa imejengwa na safu imara ya ulinzi. Wakati akiwa kocha wa Juventus, waliruhusu mabao 25 kwenye ligi kwa msimu. Wakati wake pia amewanoa wachezaji bora kama Buffon, Barzagli, Evra, Pirlo, Tevez na Dani Alves.

Klabu inayomfaa: Atletico Madrid

Inaweza kuonekana ni kitu kigumu kutokana na kile ambacho Diego Simeone amefanikiwa pale Atletico Madrid, lakini pengine inaweza kuwa ameshafikia kilele chake cha mafanikio. Ni wakati wake sasa kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine.

Ishara zinaonekana, kwa sasa wapo nafasi ya sita kwenye LaLiga, na wameiondoa Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Walipofika sasa, Simeone anatakiwa kuachia na Allegri anaweza kufiti kwenye kiti hicho.

#1. Mauricio Pochettino

Kuchomoza kwa Mauricio Pochettino katika soka la dunia hii ni kutokana na jitihada zake mwenyewe. Kuchomoza kwa Tottenham Hotspur kuwa moja ya vigogo kwenye Ligi Kuu ya England, ni kazi yake. Kwa kile alichofanikiwa Pochettino kwa klabu ambayo inachukuliwa kama haina vyanzo vingi vya fedha, kumemfanya kuwa na jina kubwa duniani.

Ingawa hajawahi kushinda taji lolote na klabu hiyo, ameichukua klabu hiyo kutoka katikati ya msimamo hadi kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Inakaribia miezi sita sasa tangu alipofukuzwa, na amekuwa akihusishwa na klabu nyingi duniani. Barcelona, Real Madrid, PSG na Newcastle, zote amekuwa akihusishwa nazo.

Tangu kuwapo na taarifa za Newcastle kununuliwa na matajiri wa Saudi Arabia, amekuwa akitajwa sana kama ndiye anayekwenda kuchukua mikoba ya kuinoa.

Klabu inayomfaa: Manchester United

Huku Pochettino akiwa anachukuliwa kama mmoja wa makocha watatu wa daraja la juu duniani, anafaa kuwa kwenye moja ya klabu bora. Ingawa Ole Gunnar Solskjaer amesaini mkataba mpya, United haijawa na matokeo ya kuridhisha tangu raia huyo wa Norway achukue kazi hiyo.

Pochettino ni aina ya mtu ambaye United inamhitaji ili kuirudisha kuwa klabu yenye kushinda katika kila mashindano. Tayari wana kikosi kizuri, na usajili wa wachezaji wengine utakuwa unahitajika. Pochettino anaweza kuwa mtu sahihi wa kufiti kwenye viatu vya Sir Alex Ferguson.

Columnist: www.tanzaniaweb.live