Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Magufuli taa ya Afrika iliyozima ghafla

171325ea38f412aa5ac8d7e592ca0bf9 Magufuli taa ya Afrika iliyozima ghafla

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TAREHE 17 Machi, 2021 haitosahaulika vichwani mwa watanzania wote hasa wale maskini na wafanyabiashara ndogo ndogo ambao imani yao kubwa ilijengwa dhidi ya mwamajumui huyu aliyefariki gafl a bila hata kuwaaga Watanzania.

Ni siku ambayo wanamajumui wa Afrika pia hawataisahau kwa kupoteza kiongozi mwenye maono na mapenzi mema na bara la Afrika tangu baada ya Hayati Baba wa Taifa.

Kimsingi Hayati Dk Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli na mwenye mapenzi ya dhati na bara la Afrika na nchi yetu ya Tanzania. Vilio vilivyotanda taifa zima na Bara la Afrika vilidhihirisha kabisa aina ya kiongozi aliyepotea.

Ni mara chache sana kupata viongozi wenye kariba yake. Aliwaaminisha watanzania ya kwamba wao ndiyo wamiliki wa nchi na kwamba watembee vifua mbele bila woga kwa kuwa yeye atasimama kuwapigania na kulinda rasilimai zao pasipo kificho na kamwe hatofumbia macho uonevu dhidi ya watanzania wote.

Ni wazi kwamba aliyoyatenda katika bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla wake ni mengi sana. Lakini kama wahenga wasemavyo ‘vizuri havidumu’.

Kauli hii imezidi kuthibitika katika kipindi hiki. Lakini kifo chake kinaacha maswali mengi kwa watanzania walio wengi ya kwamba inawezekanaje Rais aliye madarakani na matabibu wa kila aina afe kwa ughafla huu?

Jitihada gani zilifanyika ili kunusuru uhai wake? Au ndo ile tunaishia kusema bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe?

Je, inawezekana kuna aliyehusika hasa ukizingatia kuna walioanza kumzushia kifo hata kabla ya kifo chake kutangazwa?

Lakini pengine tunajiuliza ni nani atawatetea wanyonge tena? Je, huu ndiyo mwisho wa heshima katika utumishi wa umma? Na miradi yote aliyoanzisha je, iatendelezwa?

Wafanya biashara ndogo ndogo waliachwa huru kujitafutia kipato bila bughudha yoyote watabaki salama?

Inawezekana maswali haya yanatokana na kwamba hatujawahi kuona Rais akipoteza uhai wakati bado yuko madarakani nchini mwetu.

Tena akiwa na umri mdogo vile! Pengine ni ngumu kuamini kwamba Mheshimiwa Magufuli katutoka na hatutamwona tena! Kweli iauma sana. Wakati naandika makala haya nikakumbuka hotuba zake ambazo mara nyingi aliwaomba watanzannia wazidi kumwombea kwa kuwa vita vilivyokuwa mbele yake, hususani vita vya uchumi ni vikali.

Na hapa nikajiuliza swali, vita hivi vilikuwa dhidi ya nani? Je, ni mabeberu ambao hawakupenda na kamwe hawatapenda maendeleo ya Tanzania na Afrika kwa ujumla?

Je, kama ni mabeberu wamewatumia watanzania wenzetu wenye kupigania matumbo yao wenyewe? Kimsingi siyo jambo jepesi kwamba viongozi kadhaa wa kitaifa wafariki dunia tena kwa kufatana pasipokuwa na sababu ya msingi.

Sipendi nizungumze sana hilo bali niishie tu kusema pengine ni mapenzi ya Mungu na kuna mafunzo Mwenyezi Mungu anatupa. Niliwahi kutazama filamu moja ya Kikorea inayoitwa “tree with deep roots”; maudhui yake yanaendana pengine na kile ninachokiona sasa kwenye Taifa letu.

Ni wazi kwamba Rais wetu pendwa alikuwa na maadui wengi ambao kimsingi ni mabeberu wasiopenda kuona watanzania wakivuka hatua ya umasikini na kuelekea maisha yaliyobora.

Katika filamu hii niliyotaja, inaonyesha hata pale ambapo mfalme wa Korea alianzisha herufi ambazo zilikuwa rahisi kila mkorea kusoma bado maadui zake walimchukia na kutaka kumuua mfalme huyo.

Kwao hawakupenda wananchi wajue kusoma na kuandika kwa kuwa kufanya hivyo itaondoa tabaka la walio nacho na wasio nacho, sawa na kwetu baada ya Mzee Magufuli watanzania wanavyohamanika kuondoa matabaka haya.

Kwa nyakati tofauti aliwataka waandishi wa habari kuandika yaliyo mema ya Tanzania kutokana na kile alichoamini kwamba walitoa kipaumbele kwa mambo yasiyo ya msingi kwenye habari zao. Nanukuu: “Niwaombe waadishi wa habari muitangulize Tanzania kwanza.

Siku ikiharibiwa Tanzania na nyinyi mtakuwa mmeharibikiwa pamoja na wale waliowapanga kuandika yale mnayoyaandika. Matatizo yaliyotokea kwenye nchi fulani fulani yalianzia kwenye kalamu zenu.

Walianza wa mzaha mzaha hivi… Unaweza ukawa unamchukia mtu fulani lakini usiichukie Tanzania. Madhara yake ya kuendelea ni kubwa, na moto ukishawaka hamuwezi kuuzima… Huwezi kukuta waandishi wanaandika masuala ya maendeleo bali wanatafuta mahali penye migogoro ndo wanaipa kipaumbele…” Hotuba hii aliitoa kwa sauti na sura ya huzuni sana.

Je, alimaanisha kwamba mabeberu wanawatumia baadhi ya waandishi wa Habari? Pengine inawezekana maana hata kabla ya kifo chake baadhi ya vyombo vya habari vilimsingizia kuugua COVID-19 tofauti na kile kilichoelezwa na Rais Samia Suluhu Hassani wakati wa kutangaza kifo chake.

Maneno ya hayati Dk Magufuli wakati mwingine ni kama yalikuwa yanawaandaa watanzania juu ya kitakachotokea mbeleni. Wakati mwingine yalikuwa ya kinabii.

Moja ya kauli zake muhimu ni hii: ‘Siku moja mtanikumbuka. Na mimi ninajua mtanikumbuka kwa mazuri si kwa mabaya. Kwa sababu nime-sacrifice Maisha yangu kwa ajili ya watanzania maskini.

Kwa hiyo tusimame pamoja, tusibaguane kwa vyama, tusibaguane kwa ajili ya dini zetu, tusibaguane hata kwa makabila yetu. Sisi tuijege Tanzania.” Kila nikisikiliza maneno yake haya najiuliza je alijua atakufa kabla ya kumaliza muda wake wa utawala? Pengine je, aliposema aliyatoa mhanga maiasha yake kwa ajili ya watanzania maskini alimaanisha kuna genge la watu ambao hawakupenda awajali maskini na hivyo kwa hatua zake walikuwa wanapanga kumuua? Je, alimaanisha mtu anayetaka kuwakomboa watanzania awe tayari kufa kwa ajili yao?

Hili ni sawa na lile andiko la Yesu alipowaambia wafuasi wake kwamba mwenye kumfuata lazima aikane nafsi yake na kumfuata, na pengine kupoteza uhai wake?

Kama ndivyo inamaanisha Magufuli alikuwa na vita kubwa am- bayo watanzania ha- wakuiona kwa macho kwa kuwa aliwaatamia kama ndege anavyolinda vichanga vyake kwenye kiota?

Je, kama Magufuli asingejitoa mhanga kwa ajili ya maskini angekuwa hai leo hii? Kama ndivyo watanzania tunamuenzije? Kiukweli maswali ni mengi sana. Japokuwa maandiko yasema Musa alipokufa, Mungu alimuinua Joshua kuwaongoza wana wa Israel lakini je, pengo lake Mzee wetu huyu litazibika?

Kiukweli Magufuli ni chuma na mwamba wa Afrika. Kifo chake kimeshtua sana tulio wengi. Ni tumaini lililopotea wakati ambapo wahitaji wameongezeka. Ni taa iliyozima katikati ya giza totoro, hatuoni pa kwenda.

Mungu wetu asaidie katika hili. Kwa kuwa kila alipoongea alitutaka tumtangulize Mungu, basi na tuendelee kufanya hivyo na kuomba sana ili Mungu alilinde taifa letu dhidi ya genge la wanyang`anyi. Mwandishi wa makala haya ni mchangiaji wa gazeti hili.

Mawasiliano yake ni HYPERLINK “mailto:flugeiyamu@gmail. com” flugeiyamu@gmail. com; +255 7

Columnist: www.habarileo.co.tz