Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Magufuli alipigania viwanja vya kisasa

Viwanja Pic Data Magufuli alipigania viwanja vya kisasa

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

SHUJAA ameumaliza mwendo. Mwanamichezo ameondoka. Taifa linaomboleza kifo cha Rais wa Jumhuri wa Mungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki dunia Jumatano ya tarehe 17, Machi kwa maradhi ya moyo akiwa na umri wa miaka 61, kifo chake kilitokea akiwa kwenye matibau Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam.

Magufuli aliyekuwa mstari wa mbele kupigania maendeleo ya sekta ya michezo nchini, alikuwa bega kwa bega na wanamichezo kuhakikisha Tanzania inakuwa tishio Afrika na sio kichwa cha mwenda wazimu kama usemi huo ulivyokuwa ukitumika pindi mambo yanapokuwa ndivyo sivyo.

Wakati wa uhai wake, Magufuli aliwahi kueleza anataka kuuona ubingwa wa Afrika siku moja ukija Afrika, hiyo inaonyesha ni jinsi gani alitamani kuona Tanzania ikiwa tishio, sio kwa ngazi ya klabu tu hata upande wa taifa ndio maana alikuwa akitoa sapoti yake.

Makala haya yanakuletea namna rais huyo wa awamu ya tano atakavyokumbukwa kwa kuhusika kwenye mchakato wa kuubadili jina la Uwanja wa Taifa na kuwa kumbukumbu ya Rais wa awamu ya tatu, Hayati Benjamin Mkapa aliyefariki dunia wakati taifa la Tanzania lilipokuwa likielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka jana.

Pia atakumbukwa kwa kuanzisha mchakato wa ujenzi wa uwanja mkubwa wa kisasa utakaojengwa Dodoma na chini ya utawala wake kumefanywa rasmi kuwa makao makuu ya nchi huku baadhi ya ofisi zikihamishiwa huko.

TAIFA HADI MKAPA

Julai mwaka jana katika siku ya kitaifa ya kumuaga Hayati Benjamin Mkapa aliyezikwa Lupaso mkoani Mtwara, Magufuli alitangaza rasmi uwanja huo ambao ulikuwa ukifahamika kama uwanja wa Taifa kuitwa Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Magufuli alisema hali mbali na Hayati Mkapa kujenga uwanja huo, amepokea maombi mengi ya watu kutaka uwanja huo, uitwe kwa jina lake ingawa yeye (Mkapa) alipokuwa hai hakupenda hilo.

“Amejenga uwanja, tunaouona mbele yetu, napokea meseji nyingi wanataka uitwe uwanja wa Mkapa nafahamu hakupenda sana vitu viitwe kwa jina lake, amelala, hawezi kuniadhibu. Natamka rasmi uwanja wa Taifa sasa utaitwa Mkapa Stadium,” alisema na kushangiliwa kwa kupigiwa makofi na umati wa watu waliojitokeza.

Akiwa madarakani Hayati Mkapa alipigania vyema sekta ya michezo nchini na kufanikisha kujenga Uwanja wa Taifa. Baada ya kifo chake yaliibuka maoni kutoka kwa watu na taasisi mbalimbali kuhusu uwezekano wa kubadili jina la uwanja huo na kwa kuwa lilikuwa wazo zuri, Magufuli aliafiki na shughuli ya kubadili jina ikaanza mara moja.

UWANJA WA DODOMA

Uwanja wa Mkapa uliopo Temeke jijini Dar es Salaam, ndio Uwanja mkubwa zaidi kwa sasa nchini ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki waliokaa kwenye viti 60,000 kwa wakati mmoja.

Awali uwanja huo ulikuwa unaitwa Uwanja wa Taifa kabla ya kuitwa Uwanja wa Mkapa, lakini Dodoma ambayo ndio makao makuu ya nchi, ndipo uwanja mpya wa Taifa utakapokuwa endapo ujenzi wa uwanja unaotarajiwa kujengwa utakamilika.

Uwanja huo unaotarajiwa kujengwa eneo la Nzuguni (Nanenane) lililopo nje kidogo ya jiji la Dodoma, barabara ya Morogoro, ukikamilika utakuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki wasiopungua 80,000.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Katibu mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Hassan Abbasi aliyewahi kuzungumza na gazeti hili kwa kusema;

“Hapa Dodoma kuna kitu kinakuja, wakati uliokuwa uwanja wa Taifa kupitia Magufuli aliposema uitwe jina la Mkapa unaoingiza mashabiki 60,000 lakini huu utakaojengwa hapa Dodoma hautapungua watu 80,000,” alisema Dk. Abbasi.

Dk. Abbasi alisema kulingana na ahadi ya Rais atatekeleza ujenzi wa uwanja huo na taratibu zote zimekamilika ikiwa ni pamoja na kuwasilishwa serikalini, kinachosubiriwa ni fedha zake ili itangazwe tenda ya kuanza kwa ujenzi huo.

Mbali na uwanja huo utaokuwa mkubwa zaidi nchini endapo utakamilika, Dk. Abbasi aliongeza Serikali pia iliongea na wamiliki wa uwanja wa Jamhuri (Chama cha Mapinduzi) kuuboresha uwanja huo ikiwemo kuwapatia wataalam wa kusaidia uboreshaji huo.

Uwanja wa Jamhuri utatumika kwenye mechi za Ligi Kuu na timu za Dodoma Jiji pamoja na JKT Tanzania, Baobab Queens ya Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL), Fountain Gate upande wa Daraja la Kwanza (FDL) na Area C United ya Daraja la Pili (SDL).

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz