Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Magufuli alijiandaa kiroho kwa kifo

73ae3bb6e36bcf83b3b0790764e8d474 Magufuli alijiandaa kiroho kwa kifo

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

RAIS John Magufuli alijiandaa kiroho kabla ya kifo chake kwa kuongoza sala na nyimbo akiwa na madaktari na wauguzi waliokuwa wakimhudumia hospitalini.

Msemaji wa familia ya Magufuli, Ngusa Samike alisema hayo jana wakati wa Ibada ya kuaga mwili wa Rais Magufuli iliyofanyika kwenye Parokia ya St Peter Oysterbay Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Magufuli aliishuhudia imani yake, tunawashukuru kwa kushirikiana naye na kumjenga kiimani, kabla ya kifo chake aliongoza sala na wimbo akiwa na madaktari na wauguzi,” alisema msemaji huyo wa familia.

Alisema Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Paroko wa Parokia ya St. Peter, Padri Alister Makubi walimpatia huduma ya kiroho ya Mpako Mtakatifu.

Msemaji alisema pia Shehe Mkuu wa Tanzania, Mufti Abubakar Zubeir alimfanyia maombi kabla ya kifo chake.

Samike alishukuru Parokia ya St Peter kwa kumjenga Rais Magufuli kiimani.

“Tunakumbuka wiki tatu hivi zilizopita alishiriki nasi hapa na alipokuwa hapa alisema kila mtu atakufa, kwa wale ambao mnamfahamu marehemu hata kabla hajawa Rais wa Tanzania, mlipata fursa ya kushiriki naye,” alisema.

Columnist: www.habarileo.co.tz