Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Madeni ya Waamuzi usipime!-3

Waamuzi TFF Madeni ya Waamuzi usipime!-3

Sat, 7 Jan 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Katika mfululizo wa Ripoti Maalumu juu ya Waamuzi wa Tanzania, jana tuliona naona malipo yao yalivyo, ikielezwa wanalipwa kiwango kisichozidi Sh 300,000 kama posho, lakini wengi wao wakiwa wanakopwa zaidi.

Pia ilielezwa namna ambavyo waamuzi wamekuwa wakitaabika kulipwa posho hizo, kiasi cha kutengeneza mazingira yanayowaweka kwenye hali mbaya.

Leo tunaendelea kuona namna malimbikizo ya waamuzi hao yalivyo na jinsi wanavyopata ugumu kukumbushia, kwani mamlaka zimekuwa zikiwaopiga mkwara na hata kuwachukulia hatua za juu kwa juu ikiwamo kuwaondoa kwenye orodha hata kama wana uwezo mzuri. Endelea...

UKIDAI MSALA

Kuhusu waamuzi kudai posho zao Bilasho alisema:“ Nawajua waamuzi wanaodai hakuna mwamuzi wa ligi kuu ambaye hadai, mwaka jana wanadai, ligi ya wanawake wanadai hiyo ndio hawajawahi kulipwa hata 100 ligi zote za wanaume wanadai,”alisema mwamuzi huyo

Alisema wanaohusika na mpira wameamua kuuendesha mpira kwa njia ambayo wanaitaka wao.

Akisimulia zaidi Bilasho alisema baada ya kuona hapati haki yake alienda Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ambako walimsaidia kupata deni lake.

“Nadai mpaka sasa shilingi laki mbili kabla nilikuwa nadai millioni moja kama na elfu hamsini hivi walizipunguza baada ya kupigizana kelele na kufikishana mpaka Takukuru,”alisema Bilasho.

WENGI WAO WAOGA

Bilasho alisema waamuzi wengi sasa wanaogopa kusema kwamba wanadai kwa kuona hawatapangwa katika mechi zinazofuata.

“Wanaogopa kusema lakini kusema kweli uamuzi wa sasa hivi ni kama utumwa vile kwamba mwenye mamlaka ndio anaekuweka na anaekutoa,”alisema

Alisema wanapoelekea kwa sasa hali ndio itakuwa mbaya zaidi kwani hawalipwi bali hupokelewa na timu mwenyeji.

MADENI YAO

Msimu wa 2018/19, ligi haikuwa na mdhamini mkuu waamuzi wengi walifanya kazi kwa kujitolea wakiahidiwa mambo yatakapokuwa sawa basi watalipwa stahiki zao.

Msimu uliofuata neema ikaanguka kwa kupatikana wadhamini walioweka donge nono. Kilio cha waamuzi kikaongezeka kwani kati ya waamuzi waliochezesha msimu huo hadi sasa kwenye Ligi Kuu wamebaki wawili.

Anoldo Bugando na Charles Simon (Dodoma) tena walikuwa wanastahili kupewa beji ya Fifa lakini wakaondolewa kwenye ile orodha ndio pona yao na wengine wakashushwa madaraja na wengine kuwekwa kando kabisa na hakuna aliyelipwa.

Mfano msimu huo alikuwa, Alex Mahagi, Abdalah Kambuzi, Jimmy Fanuel, Gasper Ketto, Abdalah Uhako, Athuman Senkala, Jacob Adongo na Agness Pantaleo leo hii anza kufuatilia wanafanya nini au uliza kwanini walitoka kwenye reli msimu uliofuata utaambiwa utovu wa nidhamu. Hebu jiulize inakuaje asilimia 95 ya waamuzi wawe na utovu wa nidhamu.

"Hapa nilipo ninadai zaidi ya Sh7 milioni ambazo nilipangwa katika michezo 12 na kuna michezo minne nilipewa baada ya waamuzi kuchomoa dakika za mwisho yaani piga Sh520,000 mara 12 hapo sijaweka michezo ya FA.

"Tunaambiwa waamuzi ni wengi anayejisikia kubaki abaki anayetaka kuondoka anaweza kuondoka, hivyo ukihoji tu jiandae kuondoka yaani kama huna mtetezi jiandae kuondoka. Hivi umejiuliza kwanini Mwandembwa (Emmanuel) sahivi hana beji ya Fifa?

Mwandembwa ni mmoja ya waamuzi walitarajiwa kufika mbali sababu, uzuri wa jamaa lugha inapanda vyema na enzi zake waliokuwa na beji ya Fifa waamuzi wa kati ni pamoja na Florentina Zabron, Mwandembwa, Elly Sasii, Martin Saanya na Jonesia Rukyaa.

"Alipovuliwa ndio akapewa, Kayoko (Ramadhan) wakati jamaa alifika hadi hatua ya 'Elite B' yaani kiwango cha juu sana, alipovuliwa Jonesia akapewa Kassim Mwalogo, alipovuliwa Saanya akapewa mwamuzi flani hivi kutoka Zanzibar.

Mwamuzi mwingine anasema tatizo watu wanalaumu lakini hawajui nini kipo ndani yake, ukipewa maagizo unatakiwa kuyafuata, ukienda sivyo utatafutiwa kosa ufungiwe, wakati mtu anapaswa kushushwa daraja ili ajifunze na sio kufungiwa.

"Angalia maisha ya waamuzi nje ya uwanja yalivyo, kuna watu nakuambia hata wakifungiwa maisha lakini maisha yao yamekuwa mazuri kuliko uhalisia, watu wamepiga mzigo sana misimu hii miwili."

ZAIDI YA SH 10 MILIONI

“Maana nasikia kuna wengine wanadai mpaka milioni 10 sasa fikiria mpaka hapo huyo uwezo wa kwenda viwanjani alikuwa anautoa wapi, unaweza ukakuta wengine wanatemea rushwa ya kwenye vilabu.

“Mechi unalipwa 300,000 mechi 10 ni milioni 3 mpaka unafikisha milioni 10 maana yake zaidi ya mechi 30 wewe unaendaje huko kuna vitu vingi sana vimejificha lazima visemwe,”alisema Bilasho.

INAVYOKUWA

Alisema utaratibu ulivyo kwa mwamuzi ni kutumia fedha zake halafu baadae anakuja kulipwa ama baada ya mechi au katika kikao cha maandalizi ya mechi.

“Mfano kipindi cha Jamali Malinzi hela tulikuwa tunalipwa kwenye PM yaani unatoka Dodoma labda unaenda Mbeya nafika jioni kesho asubuhi tunakutana wote baada ya mechi kuna fomu ya madai tunaandika madai yetu yanasainiwa na kufafanua sababu za kutochezesha Ligi Kuu.

“Sikupewa mechi za ligi kuu kwa sababu mimi sio mtu wa kujipendekeza kwa mtu baadhi ndio zao,ninamaisha yangu nayamudu,”alisema Bilasho.

Mmoja wa waamuzi alisema hata vyombo vya habari vinachangia wao kupotea, kwani linapokuja suala la kuzungumziwa maslahi ya waamuzi, jambo hilo halipewi uzito wakiamini wapo waliozibwa midomo.

MALINZI ATAJWA

"Msidhani hata sisi tunapenda kuharibu mchezo, mtu katoka kwao na nauli ya mkopo na kupokelewa na mwenyeji (timu mwenyeji) napewa hoteli, usafiri, chakula na nauli pia narudishiwa tena mara tatu ya ile nitakayopewa na TFF, unatarajia nifanye nini.

"Nakumbuka enzi za Malinzi na Tenga madai hayakuwa namna hii, kipindi kile tulikuwa tunalipwa Sh220,000 hadi Sh250,000 yaani bora kidogo kuliko kikubwa ambacho huna uhakika nacho na ukiongea wataziba mipango yako.

"Enzi hizo ukifika tu kwenye 'Pre match meeting' napewa pesa yangu au ukimaliza mchezo tu kule vyumbani unakuta kila mtu bahasha yake na haki yake hivyo hakuna cha kusema kesho, yaani unatoka hapo na pesa yako yote.

"Alipoingia Karia wakaleta mfumo wao wa kuwekewa pesa kwenye akaunti za benki na hapo ndipo mikopo ilipoanza, sahivi unaeza ukachezesha michezo saba ukalipwa michezo miwili.

"Ninaweza nikawa na mpango wa kuja kuwa 'match commissioner' baadaye hivyo kutokana na uongeaji wangu sitapewa nafasi na wala ikitokea fursa yoyote ndani yake sitapewa ndio maana wengi wanaamua kukaa kimya.

Hebu angalia mfumo wa TFF anayeondoka ni Rais tu wengine wanaendelea kupeta na kuhama vitengo tu, leo hii nina miaka 16 kwenye uamuzi na nilimkuta, Israel Nkongo kama 'Physical Instructor', nikamkuta Soudy Abdi na Leslie Liunda 'Referees Facilitator', ukisema uovu wao wewe utotokea wapi?

Columnist: Mwanaspoti