Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

MZEE WA UPUPU: Mbappe mwana Afrika mwenye rekodi zake Kombe la Dunia

Mbappe 2 Goals.jpeg Kylian Mbappe

Thu, 22 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kijana wa miaka 23, Kylian Mbappe amekuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.Mbappe ni Mfaransa mwenye asili ya Afrika, kwa baba na mama.

Mama yake mzazi, Fayza Lamari, ni mtu wa asili ya Algeria, kutoka eneo la Kaskazini zaidi la nchi hiyo linaloitwa Kabylie.

Hili ndiyo eneo ambalo Zinedine Zidane na Karim Benzema pia wana asili nalo.Baba yake mzazi, Wilfried Mbappe, ana asili ya Cameroon, nchi inayosifika kwa kuzalisha vipaji vya soka.

Ukoo wa kina Mbappe ni moja ya koo maarufu zaidi nchini humo kwa soka, likibebwa na Samuel Mbappe Leppe, anayetajwa kama mchezaji bora zaidi soka kuwahi kutokea nchini Cameroon.

Maisha yake yote alicheza soka lake nchini Cameroon akikataa ofa kadhaa kutoka klabu vya Ulaya.

Aliitumikia klabu ya Oryx Doula na kushinda mataji 5 ya Ligi Kuu, lakini kubwa zaidi yeye ndiye nahodha wa kwanza kubeba Kombe la Klabu Bingwa Afrika, mwaka 1965 mashindano haya yalipoanza.

Kwa heshima yake, tuzo ya mchezaji bora wa Cameroon inaitwa Mbappe Leppe award.Kwa hiyo damu yenye asili ya Kabylie wanakotoka kina Benzema na Zidane imechagangika na damu ya Cameroon wanakotoka kina Samuel Eto’o na Roger Milla na kutoa kipaji cha hali ya juu sana kinachoitwa Kylian Mbappe.

Akiwa na miaka 23, Mbappe anashikilia rekodi za ajabu kwenye Kombe la Dunia. Mwaka 2018 akiwa na miaka 18, alifunga mabao manne, moja la kwenye fainali dhidi ha Croatia.

Bao hilo likamfanya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye miaka chini ya 20 (teenager) kufunga kwenye fainali ya Kombe la Dunia tangu Pele afanye hivyo mwaka 1958 dhidi ya Sweden. Mwaka huu, 2022, akiwa na miaka 23, amefunga mabao 8.

Mabao haya siyo tu yanamfanya kuwa mfungaji bora wa Kombe la Dunia, bali kuwa mchezaji wa kwanza kufikisha idadi hiyo tangu Ronaldo de Lima mwaka 2002 kule Korea Kusini na Japan.

Amefunga mabao matatu (hat-trick) kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Argentina. Hii inamfanya kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo yangu mwaka 1966 pale George Hurst wa England alipofunga dhidi ya Ujerumani Magharibi.

Alifunga bao moja kwenye fainali ya 2018 na amefunga mabao matatu kwenye fainali ya mwaka 2022.

Jumla ana mabao manne kwenye fainali, yanayomfanya kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia.

Lakini pia kwa kufunga kwenye michezo miwili mfululizo ya fainali kunamfamya kuwa mchezaji wa kwanza kufanya hivyo.

Akiwa na miaka 23, Kylian Mbappe ana jumla ya mabao 12 kwenye Kombe la Dunia, baada ya kushiriki fainali mbili, za 2018 na 2022.

Lionel Messi anayetajwa kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea, ana mabao 13 kwenye Kombe la Dunia baada ya kushiriki fainali 5; 2006, 2010, 2014, 2018 na 2022.

Cristiano Ronaldo, ambaye naye yumo kwenye mjadala kama Messi, amefunga mabao 8 licha ya kushiriki fainali 5 naye; 2006, 2010, 2014, 2018 na 2022. Nadhani hapo unaweza kuona Mbappe ni hatari kiasi gani.

Wafuatao ni wafungaji wa mashindano ya Kombe la Dunia tangu kuanza kwake mwaka 1930.

2022 - Qatar

Kylian Mbappe - Ufaransa - Mabao 8

2018 - Urusi

Harry Kane - England - Mabao 6

2014 - Brazil

James Rodriguez - Colombia - mabao 6

2010 - Afrika Kusini

Thomas Mueller - Ujerumani - mabao 5

2006 - Ujerumani

Miroslav Klose - Ujerumani - mabao 5

2002 - Korea Kusini/ Japan

Ronaldo de Lima - Brazil - mabao 8

1998 - Ufaransa

Davor Suker - Croatia mabao 6

1994 - Marekani

Hristo Stoichkov (Bulgaria) na Oleg Salenko (Urusi) - mabao 6

1990 - Italia

Salvatore Schillaci - Italia - mabao 6

1986 - Mexico

Gary Lineker - England - mabao 6

1982 - Hispania

Paolo Rossi - Italia - mabao

1978 - Argentina

Mario Kempes - Argentina - mabao 6

1974 - Ujerumani Magharibi

Grzegorz Lato - Poland - mabao 7

1970 - Mexico

Gerd Muller - Ujerumani Magharibi - mabao 10

1966 - England

Eusebio - Ureno - mabao 9

1962 - Chile

Garricha (Brazil), Vava (Brazil), Florian Albert (Hungary, Valentin Ivanov (Urusi), Drazan Jerkovic (Yugoslavia) na Leonel Sanchez (Chile) - mabao 4

1958 - Sweden

Just Fountain - Ufaransa - mabao 13

1954 - Uswisi

Sandor Kocsis - Hungary - mabao 11

1950 - Brazil

Ademir - Brazil - mabao 8

1946 na 1942

Kombe la Dunia halikufanyika kutokana na vita vya pili vya Dunia.

1938 - Ufaransa

Leonidas - Brazil - mabao 7

1934 - Italia

Nejedly - Czechoslovakia - mabao 5

1930 - Uruguay

Guillermo Stabile - Argentina - mabao 8

Columnist: Mwanaspoti