Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

MPAPASO WA MASAU BWIRE: Jaribio la kuokoa maisha ya staa lilivyokumbana na vikwazo

Ally Mtoni Sonsooo Ally Mtoni "Sonso"

Sun, 24 Apr 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Wiki iliyopita katika safu hii ya Mpapaso nilielezea namna klabu mbalimbali za mpira wa miguu nchini zinavyoamini na kudhani ushirikina na uchawi ni moja ya njia na mbinu za kuwapatia ushindi na kuwafikisha katika mafanikio.

Nilieleza namna klabu hizo zinavyolazimika kuvunja sheria na kanuni zilizowekwa kuhakikisha wanatimiza matakwa na maelekezo ya kishirikina na uchawi waliyopewa na ‘mtaalamu’ wao wa uganga huo wa kienyeji ili wapate ushindi.

Tuliona namna ambavyo baadhi ya klabu hizo za soka, zikiwemo zile kubwa zinazoshiriki Ligi Kuu Bara wanavyofanya hadharani vitendo vya kishirikina na uchawi kwa kunyunyiza, kumwaga, kutupa na kufukia dawa viwanjani ili kuwaroga wapinzani wao na kuwawezesha wao kupata ushindi.

Wakati mwingine wanafanya uharibifu wa miundombinu ya viwanja kusudi tu watimize masharti ya kishirikina na uchawi, wanaruka ukuta, wanavunja mageti uwanjani, wakikwepa kupitia mlango ulio rasmi wakihisi kwamba timu pinzani imeweka uchawi katika lango la kuingilia na kwamba, kama wakiingia kwa kutumia lango hilo ambalo ni rasmi, watafungwa.

Hali hiyo ya ushirikina na uchawi imekuwa changamoto kubwa katika soka letu inayoidhalilisha ligi yetu, klabu na hata wachezaji wenyewe mbali na kuwepo kwa kanuni zinazokataza matendo hayo ya kishirikina na uchawi, adhabu kali kwa yeyote atakayebainika bado watu wanafanya wakiamini bila hivyo, ushindi haupatikani.

Katika mpapaso wa leo, najaribu kuonyesha namna ambavyo imani hizi za kishirikina na uchawi zimewakaa baadhi ya wachezaji, kiasi kwamba bila kuzishiriki, hawaamini kama watafanya vizuri na watafanikiwa kupitia soka. Kwa kuwa ushirikina na uchawi ndivyo vimekuwa dira kwa wachezaji wengi kwamba ndicho chanzo chao kuonekana bora kiuchezaji na kuwafikisha kwenye mafanikio, wanapoumia mchezoni au mazoezini huamini kwamba wamerogwa.

Columnist: Mwanaspoti