Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

MAONI: Kazi na ziendelee, kasi ya michezo nayo iendelee

Yanga Kmc Pic Data MAONI: Kazi na ziendelee, kasi ya michezo nayo iendelee

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LIGI Kuu Bara tayari imerejea baada ya kusimama kwa muda kupisha mechi za Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) pamoja na msiba mzito ulilolikumba Taifa baada ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kufariki Dunia, Machi 17 na kuzikwa Machi 26.

Taifa lilikuwa kwenye maomboplezo ya siku 21 na Aprili 6 ndio ilikuwa siku ya mwisho ya maombolezo hayo ya kumwezi na kumkumbuka shujaa wa Taifa. Akapumzike kwa amani JPM.

Kwa sasa shughuli mbalimbali zimerejea Taifa likiwa na uongozi mpya wa Rais Samia Suluhu Hassan anayehimiza kazi iendelee ili kuijenga nchi yetu.

Hata kwa upande wa michezo kazi zinaendelea na pamoja na yote juzi Ijumaa tumeshuhudia shughuli nzito ikifanywa na mabondia wa nchini sambamba na pambano la Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly na Simba mchezo uliomalizika kwa Simba kulala bao 1-0 mbele ya wenyeji wao Al Ahly ya Misri.

Kwa upande wa masumbwi ilishuhudiwa Twaha Kiduku akiibeba vyema Bendera ya Taifa baada ya kumshinda kwa pointi Mcongo, Tshibangu Kayembe ‘Bebe Rico’ kwenye pambano lisilo la ubingwa la raundi nane.

Kwa upande wa michezo ya Ligi Kuu ambayo imerejea tangu Alhamisi iliyopita, zilishuhudiwa mechi kadhaa zikipigwa na Mbeya City iliumana na Kagera Sugar mchezo uliomalizika suluhu, huku Ihefu ikiilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC.

Related SHAURI LA MWAKALEBELA PICHA PANA Yanayotokea Simba, Namungo sababu ni hii tu Faida za Chama, Miquissone kutamba AfrikaJuzi ijumaa Biashara United ililazimishwa sare ya 1-1 na Polisi Tanzania, JKT Tanzania ikiifunga Mwadui FC 3-1 na Azam FC ikishinda nyumbani mabao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, kabla ya jana kupigwa mechi nyingine za ligi hiyo na Tanzania Prisons itaikaribisha Dodoma Jiji, Gwambina Itaikaribisha Coastal Union huku vinara wa ligi, Yanga itaikaribisha KMC.

Kwa maoni yetu kama wadau wa michezo, tunaamini kuendelea kwa kazi kama Rais Samia anavyohimiza, ni pamoja na matokeo chanya kwenye viwanja vya michezo.

Maandalizi kwa kila timu na hata wanamichezo yatasaidia kulibeba Taifa kwenye michezo ikiwemo pia michango ya wahisani na wadau wa michezo kwenye kuhakikisha hawamwangushi Rais Samia kwenye shughuli za michezo.

Tumeshuhudia kasi ya Wekundu wa Msimbazi, Simba kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na Namungo ambayo imesaliwa na michezo miwili ilionyesha taswira nzuri kwa soka letu baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tunahimiza kasi ya michezo izidi kukua kwani ni moja ya shughuli zinazoleta umoja na amani kwenye Taifa letu kwa kuunganisha watu na kuleta burudani.

Ushindani wa Ligi Kuu uliokuwepo tangu mwanzo uendelee huku sintofahamu zote zikimalizwa ikiwamo ya Yanga na Shirikisho la Soka nchini ambazo zimepewa Jumatatu ya wiki ijayo kukaa na kumalizana.

Tunaamini michezo itaendelea kwa kasi yake na kuwapa Watanzania ikiwamo kwa timu za Taifa zinazopshiriki michuano mbalimbali.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz