Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Leo ni siku nyingine ya kuionesha dunia tunavyompenda Magufuli

2030b7d8359f1fcadc66e731dc82563f.png Leo ni siku nyingine ya kuionesha dunia tunavyompenda Magufuli

Mon, 22 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

LEO wana Dodoma wana kila sababu ya kufurika kuonesha dunia jinsi Watanzania wanavyosikitika kuondokewa na kiongozi wao shupavu, mzalendo na kipenzi chao, Dk John Magufuli. Dodoma ukiwa ni kitovu cha Tanzania, mshikamano mtakaouonesha leo utakuwa ni mnyororo wa kuendelea kuzima kejeli za wachimvi ambao wanadhani sisi hatujui lulu yetu nini.

Nyie ambao mnatengeneza historia kamili ya mji huu ambao kwa sasa unabadilika na kuwa maarufu kutokana na kuwa sehemu ya siasa na kutunga sheria na kitovu cha elimu, hakika mna kila sababu ya kuionesha dunia nini maana ya kuwa Mtanzania.

Mwaka 1973 Dodoma ilipochaguliwa kuwa makao makuu ya serikali, ilielezwa eneo hilo kuwa kitovu cha juhudi za kujenga ujamaa na mshikamano nchini Tanzania na leo tena uwakilishi umekaa kwenye kuonesha dunia ‘Sisi ni watanzania.

’ Ingawa ni kweli kuwa wazo la kufanya Dodoma kuwa Makao Makuu lilifikiriwa tangu mwaka 1915 na wakoloni wa Kijerumani likarejewa wakati wa uhuru aliyetekeleza kwa vitendo wazo hilo ni Dk John Magufuli.

Ndio, ni baada ya Februari 1966 Mbunge wa Musoma Mjini wakati huo Joseph Nyerere kuwasilisha bungeni muswada binafsi, ambapo alibainisha kuwa Dar es Salaam inahudumia sehemu ndogo ya nchi na kupendekeza makao makuu ya serikali kuwa Dodoma ili kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali.

Sote tunajua kwamba hoja hiyo iliendelea kulala katika makabrasha hadi pale mwaka 1972 shauri hilo lilipopelekwa Kamati Kuu ya TANU mkoa wa Mwanza ambako kwa kauli moja walisema makao makuu ya TANU yawe Dodoma, lakini pia ikapendekezwa kuwa makao makuu ya serikali nayo yahamie huko.

Pamoja na kauli hizo aliyewezesha serikali kuhamia Dodoma ni Dk John Magufuli ambaye alifanyakazi hiyo kwa weledi , moyo safi na wenye kutia moyo sana na sasa tunaona mabadiliko.

Mabadiliko makubwa yanayoendelea kutokea katika mkoa wa Dodoma hasa kwenye mji wenyewe kwa sasa, kuhusiana na masuala ya ustawi wa jamii kunafanya mji huu ambao kwa miaka mingi umekuwa ukizungumzwa kama mji muhimu wa Tanzania, kujiweka katika ramani ya moja ya miji inayopendwa na watu kuishi na kufanyia kazi.

Hivyo unapoangalia historia ya Mkoa wa Dodoma tangu wakati wa ukoloni mpaka sasa utabaini kuwa Dodoma ina kila sababu ya kusimama kwa saa zaidi saa 12 kutoa salamu za Tanzania kwa mwanamageuzi huyo mpendwa.

Historia inaonyesha nguvu ya Dodoma na leo lazima dunia nzima ijue kwamba hii ni Tanzania na kama Tanzania wananchi wake hawaogopi kuonesha hisia zao za kweli kuhusu kiongozi wao mpendwa.

Watanzania wanampenda Magufuli kwa kuwawezesha kuwa na heshima duniani, wanampenda kwa kuhakikisha kwamba kodi ya serikali inafanyakazi iliyokusudiwa na kubwa zaidi utajiri wa Tanzania kutumika kwa ajili ya Watanzania wenyewe na hasa wanyonge na wasiokuwa na uwezo ili kuwapatia huduma muhimu kama vile elimu na matibabu na kuwaongezea uwezo wa mitaji.

Shime Wana-Dodoma leo ndio siku yetu. Mungu ametoa Mungu na Mungu ametwaa jina la bwana lihimidiwe. Amina.

Columnist: www.habarileo.co.tz