Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kwenda Qatar sio bahati, kunahitaji maandalizi

Qatar World Cup 3269040 Kwenda Qatar sio bahati, kunahitaji maandalizi

Sun, 14 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

HAKIKA wiki imekuwa chungu sana kwa mashabiki kutokana na mambo yaliyoikumba Tanzania kwenye mechi yao ya Kundi J. Mapema mashabiki walielekeza macho na masikio kwenye ya mechi ya Taifa Stars kutaka kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2022 zitakazofanyikia Qatar.

Stars ilikuwa ikikutana na DR Congo katika mchezo wa kundi lake na kwa bahati mbaya timu hiyo ilipasuka kwa mabao 3-0 nyumbani, huku wapinzani wao kwenye kundi hilo Benin usiku wake ikapata ushindi nyumbani kwa mabao 2-0 dhidi ya Madagascar.

Mashabiki walikuwa na kiu ya kufuatilia mechi hizo kutokana na mazingira waliyokuwa nayo Stars katika kundi lao na kusababisha wadau wa soka nchini na nje ya nchi kuwa na imani kubwa kwa timu yao itafanya vema katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar.

Kwa kiasi kikubwa imani hiyo ilijengwa baada ya Stars kupata ushindi ugenini dhidi ya Benin katika mechi iliyorejesha imani kubwa na kuona kuwa inawezekana kupata matokeo chanya katika mechi mbili zilizosalia ambazo ni ya nyumbani dhidi ya DR Congo na ile ya mwisho dhidi ya Madagascar itakayochezwa kesho Jumapili jijini Antananarivo, Madagascar.

Kwa kawaida mashabiki hawatakiwi kulaumiwa kwa kuwa na imani kubwa na timu yao kwa kuwa ni haki yao ya msingi na hasa pale timu hiyo inapokuwa imeweza kuthibitisha ubora wake katika baadhi ya mechi kama tulivyoona timu yetu ilivyotengeneza imani hiyo kwa kupata sare dhidi ya Wakongo katika mechi ya kwanza kisha kupata ushindi katika mechi nyingine ya ugenini dhidi ya Benin.

Ikumbukwe mechi hizi ni za kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani na kama kawaida Afrika itawakilishwa na timu tano kati ya 54 ambazo ni wanachama wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Hivyo kwa matokeo ya mechi nne zilizopita zilizoifanya Stars kuongoza msimamo wa Kundi J ikiwa na pointi 7 sawa na Benin na kutofautiana uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa ulifanya mashabiki kuamini safari ya Qatar ilikuwa bado kidogo.

Kwa matokeo ya mechi za juzi imemaanisha safari ya Tanzania imefikia mwisho na Benin na DR Congo ndio waliobaki katika kuwania nafasi moja ya kundi hilo, kwani Benin ipo kileleni na pointi 10 na DR Congo ikiwa na nane, kama Wakongo watashinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya vinara hao wanaenda, Benin ikipata sare tu nayo inaenda.

Awali msimamo ulivyokuwa uliwajengea wadau wengi wa soka matamanio ya kiwango cha juu cha kutaka kuona timu yetu ikifanya vema na kupata nafasi hiyo ya kuiwakilisha Afrika katika fainali za Qatar.

Imani hiyo ya Watanzania juu ya timu yao ilipotezwa juzi baada ya kipigo cha Wakongo katika mchezo ambao karibu wadau wengi kama sio wote walioufuatia mchezo huo hawakutarajia matokeo kama hayo yangeweza kupatikana Kwa Mkapa.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza Stars kufungwa bao la mapema zaidi, dakika ya sita tu, lakini ilikuwa ni mechi ambayo timu yetu ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao na kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa huku Kongo wakionekana kucheza taratibu.

Kipindi cha pili ndio kiliwashangaza wengi baada ya DR Congo kufunga mara mbili na kufanya matokeo kuwa 3-0 huku mashabiki wakionekana kukasirika na kuanza kuondoka uwanjani kabla mchezo kumalizika kutokana na matarajio waliyokuwa nayo kutokufikiwa.

Baada ya mchezo huo maoni mengi yalitolewa na wadau huku kila mtu akiwa na mtazamo wake juu ya nini kilichopelekea Stars sio tu kupoteza mchezo bali kufungwa mabao 3-0.

Mijadala iliendelea ikijikita kwa wachezaji huku kila mtu akiwa na mtazamo tofauti juu ya kikosi kilichopangwa na Kocha Kim Poulsen na wengine wakisema kama nafasi zilizotengenezwa zingetumika ipasavyo, basi timu ingeibuka na ushindi wa mabao zaidi ya saba.

Wapo wanaoamini nafasi nyingi za mabao zilizopotezwa katika kipindi cha kwanza, zilichangiwa kuwavuruga kisaikolojia wachezaji.

Hivyo, pamoja na wadau kuainisha sababu mbalimbali wanazoona ndio zilisababisha timu yetu ya Taifa kupoteza mchezo huo, lakini kikubwa tunachotakiwa kujifunza pale yanapotokea matukio kama haya ni kuwa siku zote licha ya kuwepo kwa bahati lakini siku zote ‘Bahati hupatikana pale panapokuwa na maandalizi ya kukutana na bahati hiyo” (‘Luck is what happens when preparation meets opportunity.’’)

Hivyo, hata kama tulikuwa na matarajio ya kupata matokeo na kuvuka kwenye Kundi J tukiwa viongozi na kuingia kwenye hatua ya mwisho ya 10 Bora na hatimaye kwenda hatua ya fainali tunatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Mpango wa angalau wa miaka mitano utakaorahisisha kazi hata pale panapotokea mabadiliko ya benchi ya ufundi na kusababisha kuwa na mwendelezo tofauti.

Ila kwa sasa kila kocha anapoingia huwa na mipango yake ya muda mfupi na kusababisha kukosa mwendelezo ndio sababu ya Kim kuonekana kutumia wachezaji wengi aliowahi kuwafundisha kutokanana imani aliyokuwa nayo kwao kwa muda aliowafundisha.

Pia lazima tukumbuke kuwa timu yetu ilicheza na timu bora tukilinganisha na yetu.

Wametuzidi sana wale.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz