Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kwanini watu wamepunguza kuzaa duniani?

A Kwanini watu wamepunguza kuzaa duniani?

Wed, 15 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Dunia haijajitayarisha kuwa na idadi ndogo ya watoto wanaozaliwa ambayo itakuwa na athari hata katika jamii, watafiti wanasema.

Kupungua kwa kiwango cha kuzaliana kuna maanisha kwamba karibu kila nchi inaweza kuwa na idadi ndogo ya watu kufikia mwisho wa karne hii.

Na mataifa 23 - ikiwemo Uhispania na Japani - yanatarajia kuwa idadi jumla ya watu itapungua kwa nusu kufikia 2100. Kipi kinachoendelea?

Kiwango cha kuzaliana - wastani wa idadi ya watoto ambayo mwanamke anazaa pia nayo inapungua.

Ikiwa idadi hiyo itapugua chini ya takriban kiwango cha 2.1, idadi ya watu itaanza kupungua.

Mwaka 1950, wanawake walikuwa wanapata wastani wa watoto 4.7 katika kipindi cha maisha yao.

Watafiti katika moja ya Taasisi ya Afya huko Washington, wameonesha kwamba kiwango cha kuzaliana duniani kilipungua kwa karibu nusu hadi 2.4 mwaka 2017 na utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Lancet, unakadiria kwamba kiwango cha kuzaliana kitapungua hadi chini 1.7 kufikia 2100.

Matokeo yake ni kwamba watafiti wanatarajia kuwa idadi ya watu duniani kuwa katika kilele chake cha watu bilioni 9.7 karibu mwaka 2064, kabla ya kupungua hadi bilioni 8.8 kufikia mwisho wa karne.

"Hi ni jambo kubwa; maeneo mengi duniani sasa yanakugeukia kupungua kwa idadi ya watu kwa hiari," mtafiti Profesa Christopher Murray amezungumza na BBC.

"Najua ni vigumu kukubali hili na kutambua kwamba ni jambo kubwa; ni jambo la kipekee, itabidi jamii zipangwe upya." Kwa nini viwango vya kuzaliana vinapungua?

Hakuna uhusiano wowote na idadi ya shahawa au yale mambo ya kawaida yanayokuja akili wakati wa mjadala wa uwezo wa kuzaliana.

Badala yake hili linachangiwa na wanawake wengi kupata elimu na kufanyakazi, pamoja na upatikanaji wa njia za upangaji uzazi, na kufanya wanawake wengi sasa kuamua tu kupata watoto kidogo kwa hiari yao. Kwa njia nyingi, kupungua kwa kiwango cha kuzaliana ni mafanikio. Nchi gani zitaathirika zaidi? Baby and granddad

Chanzo cha picha, Getty Images

Idadi ya watu nchini Japani inakadiriwa kupungua kutoka kilele chake cha watu milioni 128 mwaka 2017 hadi chini ya milioni 53 kufikia mwisho wa karne.

Italia inatarajiwa kushuhudia kupungua kwa kuzaliana kiwango sawa na hicho kutoka milioni 61 hadi milioni 28 kwa kipindi sawa na cha Japani.

Kuna nchi 23 - ambazo ni pamoja na Uhispani, Ureno, Thailand na Korea Kusini - ambazo zinatarajiwa kwamba kiwango chao cha kuzaliana pia kitapugua kwa zaidi ya nusu.

"Hicho ni kiwango kikubwa sana cha kupungua kwa kuzaliana," Profesa Christopher Murray amesema.

Sasa hivi, China ndio taifa lenye idadi kubwa ya watu duniani na inatarajiwa kufikia kilele chake cha watu bilioni 1.4 miaka minne ijayo kabla ya kupungua kwa karibu nusu hadi milioni 732 kufikia 2100. India itachukua nafasi yake.

Uingereza inatarajiwa kufikia kilele chake cha watu milioni 75 mwaka 2063 na kupungua hadi kufikia watu milioni 71 kufikia 2100.

Hata hivyo hili litakuwa tatizo la dunia nzima ambapo nchi 183 kati ya 195 kiwango chao cha kuzaliana kitakuwa chini ya kinachotakikana ili idadi ya watu isipungue au kuongezeka. Kwanini hili ni tatizo?

Unaweza kufikiria kwamba hii ni hatua nzuri. Idadi ndogo ya watu itapunguza uzalishaji wa hewa chafuzi pamoja na ukataji wa miti.

"Hilo litakuwa kweli isipokuwa tu kwa nchi zenye idadi kubwa ya wazee kuliko wenye umri mdogo na athari zingine pia zitatokea," amesema Profesa Murray. Utafiti huo unakadiria:

Idadi ya watoto chini ya miaka mitano itapugua kutoka milioni 681 mwaka 2017 hadi milioni 401 mwaka 2100.

Idadi ya wenye zaidi ya umri wa miaka 80 itaongezeka kutoka milioni 141 mwaka 2017 hadi milioni 866, mwaka 2100.

Profesa Murray ameongeza: "Hili pia litaleta mabadiliko katika jamii. Linanifanya kuwa na wasiwasi kwasababu nina msichana wa umri wa miaka 8 na kile ninachojiuliza ni je dunia itakuwa vipi."

Nani atakayelipa kodi katika dunia ambayo wengi ni wazee? Je ni nani atakayelipia huduma za matibabu kwa wazee? Je ni nani atakayetunza wazee? Na je bado watu watakuwa wanaweza kustaafu kazini umri ukishatimia?

"Tunahitaji kuwa na njia mbadala stahiki," Profesa Murray amesema.

WHO yaonya hali ya watoto ya siku zijazo 'Nataka watoto wangu wajivunie kuwa weusi’

Je kuna suluhisho?

Nchi zikiwezo Uingereza, zimetumia uhamiaji kuimarisha idadi yao ya watu na pia kutoa fidia kwa kupungua kwa kiwango cha kuzaliana.

Hatahivyo, hili halitakuwa suluhisho pale idadi ya watu ya karibu kila nchi itakapokuwa inapungua.

"Tutaingia kipindi ambapo itakuwa ni chaguo la nchi kufungua mipaka yake au la, kwa ushindani wa wahamiaji kwasababu watu watakuwa hawatoshi," Profesa Murray anasema.

Baadhi ya nchi zimejitahidi kuimarisha sera zao kama vile likizo kwa kina mama wanapojifungua pamoja na kwa waume wake zao wanapopata watoto, pesa za matunzo ya watoto zinazotolewa na serikali, vichocheo vya kifedha na haki zaidi kwa wafanyakazi lakini bado jibu la moja kwa moja halijapatikana.

Sweden imeongeza kiwago chake cha kuzaliana kutoka 1.7 hadi 1.9 lakini nchi zingine ambazo zimekuwa zikijitahidi kupunguza idadi ya kuzaliana zimekuwa na wakati mgumu. Singapore bado ina kiwango cha kuzaliana cha karibia 1.3.

Profesa Murray anasema: "Naona wengine wakichukulia suala hili kama mzaha; hawafikirii kwamba linaweza kuwa kweli, wanafikiri wanawake watafanya maamuzi ya kupata watoto zaidi tu.

"Ikiwa suluhisho haiwezi kupatikana bila shaka hatimae spishi hii itatoeka, lakini hilo ni karne kadhaa ijazo." Vipi kuhusu Afrika? watoto

Chanzo cha picha, AFP

Idadi ya watu katika jangwa la Sahara inatarajiwa kuongezeka hadi kufikia zaidi ya bilioni 3 kufikia 2100.

Na utafiti unaonesha kwamba Nigeria itakuwa nchi ya pili yenye idadi kubwa ya watu duniani ikiwa na watu milioni 791.

Professa Murray amesema: "Kutakuwa na watu wengi wenye asili ya Afrika katika nchi nyingi zaidi.

"Pia changamoto za ubaguzi wa rangi duniani zitakuwa zinakosolewa zaidi kama idadi kubwa ya raia wenye asili ya Afrika itakuwa katika nchi nyingi zaidi." Kwanini kiwango cha kuzaliana ni 2.1?

Unaweza kufikiria kwamba kiwango hicho kinastahili kuwa 2.0 - yaani wazazi wawili kuwa na watoto wawili, ili idadi iendelee kukua kwa kiwango hicho hicho.

Lakini hata pakiwa na huduma bora za afya, sio watoto wote watakaokuwa hai hadi ukubwa wao.

Mataifa yenye idadi kubwa ya vifo vya watoto pia inahitaji kiwango cha juu cha kuzaliana. Watafiti wanasema nini?

Profesa Ibrahim Abubakar, kutoka Chuo cha London (UCL), amesema: "Ikiwa makadirio hayo yatakuwa sahihi hata kwa nusu tu, uhamiaji utakuwa jambo la lazima kwa mataifa yote na wala hakutakuwa na namna nyengine.

"Kufanikiwa, siasa za dunia zinahitaji kufikiriwa upya.

Columnist: www.tanzaniaweb.live