Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kwanini mechi hizi zimepelekwa Tanga?

Wallace Karia Bila Vijana Rais wa TFF, Wallace Karia

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Nasikia Tanga ukilipa Nauli, haiendi Bure. Kuna Soka na Mapenzi. Sawa. Nimekubali ndugu zangu lakini ndiyo kila Siku Matukio Makubwa yapelekwe Tanga?

Tanga ndiyo Mkoa anakotoka Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ndugu, Wallace Karia. Kuna ubaya akipeleka mashindano Mkoani kwao? Jibu ni hapana. Mpira unapaswa kuchezwa kila kona ya nchi yetu. Kuna ubaya matukio mengi makubwa yakifululiza kupelekwa Tanga? Jibu ni ndiyo. Italeta hisia za Upendeleo.

Jibu ni ndiyo kwa maana Tanzania ina mikoa zaidi ya 20. Nimeona taarifa ya TFF ambayo imethibitisha Mechi tatu za Ngao ya Jamii mwaka huu kufanyika Tanga. Sina tatizo na Tanga. Sina Tatizo na TFF. Sina tatizo na Wallace Karia. Nina tatizo na matukio Makubwa ya Soka mengi kufanyika Tanga mfululizo.

Hivi Karibuni tumeshuhudia Fainai ya Azam Sports Federation Cup baina ya Yanga vs Azam FC ikichezwa Mkoani Tanga. Hivi karibuni tumeshuhudia Tuzo za TFF zikifanyika pia Mkoani Tanga na hivi karibuni, tutashudia Simba SC, Yanga SC, Azam FC na Singida Fontein Gate FC zikishiriki michuano ya Ngao ya Jamii Mkoani Tanga.

Hapa ndipo shida yangu inapoanzia. Kuna maneno ya mtaani nayasikia kuwa ukilipa Nauli kwenda Tanga, haiendi Bure. Mpira utapata na mapenzi utapata! Kama hii ndiyo sababu ya msingi, basi tuendele tu kula Mtori maana nyama tutazikita chini.

Ni sawa TFF kupeleka matukio matatu makubwa ya Soka nchini mfululizo mkoani Tanga? Naomba maoni yako kwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Unapopeleka matukio makubwa matatu ya Soka mfululizo mkoani Tanga, unawapa watu sababu ya kukujadili. Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma ni mikoa minne ambayo kwenye Miundombinu ya Soka la hapa kwetu imekamilika zaidi kuliko Tanga.

Ni mikoa yenye uwezo wa kupokea Wageni bila tatizo lolote. Kuanzia Barabara, Hoteli, sehemu za Starehe n.k. Ni tofuati sana na Tanga. Tanga ni Mkoa mzuri na una heshima lakini sio mahali pa kupeleka matukio makubwa kila siku na kibaya zaidi ni mfululizo. Labda kwa sababu mtaani kuna maneno nayasikia kuwa ukilipa Nauli kwenye Tanga, haiendi Bure.

Mpira utapata na Mapenzi utapata! Bado sioni kama ni wazo zuri kutoka kwa TFF ambayo Kiongozi wake mkuu ni mtu wa Tanga. Naunga mkono hoja ya Uongozi wa Wallace Karia ya kutuka mpira uchezwe kote sio Dar es Salaam tu. Naunga mkono, lakini sio Tanga kila siku. Kupeleka Tanga matukio makubwa ya Kimpira nchini tena mfululizo, haikubaliki. Ni dalili za upendeleo ambazo hazina mpango wowote.

Sina tatizo na Tanga. Sina tatizo na TFF. Sina tatizo na Karia. Nina tatizo na kupeleka matukio matatu makubwa ya Soka mfululizo mkoani Tanga.Ni sawa TFF kupeleka matukio matatu makubwa ya Soka nchini mfululizo mkoani Tanga? Naomba maoni yako kwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Hivi karibuni tuliona fainali ya Kombe la FA ikipigwa Kigoma. Lilikuwa wazo jema kabisa. Tulishuhudia Fainali nyingine ikipigwa Sumbawanga, ni jambo la heri sana. Lakini Sumbawanga ingerudiwa mara tatu mfululizo, isingekuwa sawa. Watu wangehoji tu. Kigoma ingekuwa mfululizo, isingekuwa sawa.

Tanga ni mkoa mzuri lakini bado kuna tabu sana kwenye kuhudumia Mashabiki wa Simba na Yanga ambao ndiyo wengi zaidi Nchini. Bado miundombinu ya Tanga sio rafiki sana. Mahali pa kulala ni shida. Chukula pia changamoto. Watu wa mpira wakisafiri wanakwenda kula Starehe. Klabu za Usiku na mambo mengine, bado Tanga sio rafiki. Labda kama yale maneno ya mtaani ya kufata Soka na mapenzi ndiyo sababu ya msingi, tofauti na hapo Tanga sio mahali pa kupeleka matukio mengi mfululizo kama wanavyofanya TFF.

Kuna muda nawaza bila hata kupata Majibu. Ingekuwaje kama Simba na Yanga wangekutana kwenye Fainali ya FA msimu uliopita? Najua mechi ingechezwa lakini mashabiki wangeishije? Sina hakika. Najua fainali ya Simba na Yanga imewahi kuchezwa Kigoma lakini kumbuka, Kigoma ni mbali sana kutoka yaliko Makao makuu ya Klabu hizi mbili ukilinganisha na Tanga. Hapa ni karibu sana. Ni rahisi watu wengi sana kusafiri. Ni sawa TFF kupeleka matukio matatu makubwa ya Soka nchini mfululizo mkoani Tanga? Naomba maoni yako kwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba yangu ya simu hapo juu.

Ukitaka kuwa Nchi mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia, ni lazima ufikie vigezo vilivyowekwa na Shirikisho la Soka Duniani FIFA. Ukitaka kuwa mwenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika, ni lazima ufikie vigezo vilivyowekwa na Shirikisho la Soka Afrika, CAF. Nadhani TFF wanapaswa kujifunza hapa.

Michuano mikubwa yenye kugusa watu wengi, haiendi tu popote. Wale Waingereza pale UK tunaowafuata kwa mambo mengi, sio Wajinga fainali zote kuzipeleka Wembley Stadium. Kama uwanja wetu wa Mkapa unahitaji marekebisho, basi isiwe Tanga kila siku. Kuna Dodoma na Arusha ambako miundombinu inaruhusu kupokea Wageni wengi. Ni mikoa ambayo wana uzoefu mkubwa wa kutoa huduma kwa watu wengi kwa pamoja. Rais wa TFF na Uongozi wake wanatakiwa kuukwepa mtego wa upendeleo.

Kupeleka matukio matatu ya Soka mfululizo, kunaleta maswali mengi. Qatar walikuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia mwaka jana, watu watapiga kelele kama Matukio mangine ya Soka mfululizo yatapelekwa huko Uarabuni. Unajua kwa nini? Kiukweli Qatar haikuwa rafiki sana kwa mashabiki.

Ni kwa sababu tu watu wanapenda mpira. Ingekuwa ni Brazil au Nchi nyingi za Ulaya, watu wanatamani Kombe la Dunia lifanyika hata kila mwezi. Again, sina tatizo na Tanga. Sina tatizo na TFF. Sina tatizo na Karia. Nina tatizo na Tanga kupewa uwenyeji wa matukio makubwa ya Soka mfululizo. Karia anatoka Tanga, huo ni mtego.

Columnist: Mwanaspoti