Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kwa nini Yanga na Simba tu? kuna jambo

Kibu D Simba na Yanga zinalalamikiwa kupewa upendeleo na waamuzi

Fri, 3 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022 imemaliza mzunguko wa saba wiki hii kwa mechi kati ya Simba na Geita Gold.

Lakini wakati tunakwenda kuianza raundi ya nane, kauna malalamiko mengi juu ya waamuzi katika hizo raundi saba zilizopita.

Na wingi wa tuhuma hizo inazihusisha vigogo katika soka la nchi hii, Simba SC na Yanga.

Mambo ya kutumwa hayana ushahidi na hatuwezi kudhibitisha juu ya hayo, makosa ya kibinadamu yanatokea kwa Yanga SC na Simba SC jambo linalotufanya tuanze kuwaza nje ya makosa ya kibinadamu.

Huenda kamati ya waamuzi haipo huru inaingiliwa maamuzi na kamati ya mashindano pamoja na Bodi ya Ligi.

Pia tatizo lingine linatokana utaratibu wa kuwapata waamuzi tofauti na zamani ilikuwa lazima mwamuzi achezeshe mechi 45 katika madaraja tofauti hii ingeweza kuwasaidia kwa sababu kwenye madaraja hayo wangeweza kuwasaidia kwenye matukio ambayo wangekutana nayo kwenye ligi kuliko kuwaleta moja kwa moja kwenye ligi.

Columnist: www.tanzaniaweb.live