Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kupanda na kushuka kwa AS Vita Club

Vita Club 4ke7tto85d7p1w10k0tl7r3ty AS Vita Club

Sat, 23 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ijumaa timu Ya Association Sportive Vita Club kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Kongo imeondoshwa katika Michuano ya kombe la Shirikisho, binafsi sijashangaa sana kutokana na timu hiyo kuuza wachezaji wengi nje ya Kongo mpaka kocha mkuu ambaye aliwapatia mafanikio makubwa bwana Ibenge.

Niliwatazama wakicheza fainali ya kombe la shirikisho barani Afrika mwaka 2018 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco pale LeopardVille na wakashinda 3-1 huku wakipoteza taji mbele ya Raja kwa agreggate ya 3-4.

Wachezaji kama Nelson Lukongo, Djuma Shaaban, Muzinga Ngonda, Makwekwe Cupa, Litombo Bangala, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Fabrice Ngoma, Mukoko Batezadio, Makusu Mundele, Enerst Luzolo Sita, Ducapel Moloko, walikuwa sehemu ya kikosi cha mafaniko ambao baada ya fainali ile msimu mmoja baadae walihama kwenda vilabu mbali mbali barani afrika na Ulaya.

Wachezaji kama Goma alikwenda Raja Casablanca, Mukoko na Tusila walikwenda Yanga, Bangala alikwenda FAR Rabbat, Lukombe alikwenda Almeria ya Spain, Muzinga alikwenda Dijon ya Ufaransa na wengine wengi.

Vita klabu wakajaribu tena kujenga timu ambayo ilikuja kubomolewa na Yanga kwa kuwasajili Djuma Shaabani, Ducapel Moloko na Fiston Mayele kalala.

Hawa walikuwa wachezaji tegemeo na ndiyo sababu hata Simba haikuwa ngumu kupata matokeo pale Leopard Ville mwaka Jana kutokana na kuwa Vita club ilikuta imeporomoka mno.

Wanayo kazi kubwa ya kujenga timu na wanahali mbaya ya kiuchumi hivyo wataendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya kimataifa

Columnist: www.tanzaniaweb.live