Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Krismasi imepita salama,bado Mwaka Mpya

931838504f52d4e347c307355d04f30e Krismasi imepita salama,bado Mwaka Mpya

Sun, 3 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BAADA ya sikukuku ya Krismasi kupita salama, sasa zimebaki sherehe ya kuupokea Mwaka Mpya wa 2021.

Sherehe ya Mwaka Mpya ni moja ya matukio makubwa duniani, yanayosherehekewa na watu wote kwa mitindo tofauti lakini inayofanana, mfano urushaji wa fataki, magari kupiga honi na watu kucheza ngoma. Baadhi huimba na kukikimbia mitaani na wengine huwa kwenye nyumba za ibada.

Haya yote hufanyika katika kuonesha furaha ya kuumaliza mwaka uliopita salama na matarajio ya mwaka mpya, kwamba Mwenyezi Mungu atafanikisha mipango mbalimbali.

Pamoja na haya yote, wapo wengine kupitia sherehe hizo za mwaka mpya hususani katika mkesha wake, hupanga kufanya ujambazi, wizi, ukabaji na kuendesha magari hovyo.

Matukio hayo ya uhalifu huwa na madhara kwa watu mbalimbali, ambapo baadhi huuawa au kujeruhiwa, kutiwa hasara na umaskini kwa kuibiwa mali zao na madhara mengine mbalimbali.

Hivyo basi, kama Krismasi ilivyopita salama, naamini vyombo vya dola hususani Jeshi la Polisi limejipanga vyema katika kuhakikisha hakuna uhalifu utakaofanyika katika sherehe za kuupokea Mwaka Mpya wa 2021 katika usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa wiki hii.

Natambua ni wajibu wa kila raia kutunza amani na utulivu katika kipindi chote cha sherehe za mwaka mpya, lakini pia ni vyema Polisi waimarishe ulinzi kila kona ya nchi na katika mikusanyiko ya watu, ili kuhakikisha wahalifu hawapati nafasi ya kutekeleza uhalifu wao kwa raia wema.

Wananchi wanahitaji kufurahia Mwaka Mpya kwa amani na utulivu, bila purukushani za vibaka, wezi, majambazi au uhalifu wa aina yotote ile, kwani hayo yanaweza kuondoa ladha nzuri ya Mwaka Mpya wa 2021.

Kwenye baadhi ya miji ambako kuna fukwe za Bahari ya Hindi au fukwe za ziwa mfano Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika na Ziwa Nyasa, watu hupenda kwenda kubarizi na wengine kuogelea kusherehekea Mwaka Mpya. Hivyo, basi ni vyema maeneo hayo nayo, ulinzi uimarishwe ili wananchi wafurahie Mwaka Mpya bila bughudha yoyote ya uhalifu.

Ndiyo maana nimesema baada ya Krismasi kupita salama, sasa zimebaki sherehe za kuupokea Mwaka Mpya wa 2021.

Hivyo basi, Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wananchi, wana wajibu wa kutunza amani na usalama ili hatimaye Mwaka Mpya upokewe kwa amani na utulivu.

Columnist: habarileo.co.tz