Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Klabu ziache wachezaji wao mapema

Jonas Mkude 12 Jonas Mkude ameachwa na Simba

Tue, 27 Jun 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Usajili wa Ligi Kuu Bara pamoja na ligi nyingine unatarajiwa kufunguliwa Julai 1 kwa timu zote kuhakikisha kuwa zinaziba mapengo kwenye vikosi vyao.

Huu ni usajili mkubwa ambao timu nyingi huutumia vizuri kuhakikisha kuwa kila kitu kinaenda sawa, lakini ndiyo kipindi ambacho wachezaji wengi hupatikana sokoni tofauti na usajili ule wa Januari.

Tuyari tumeona timu kadhaa zimeacha wachezaji wao, Simba, Yanga, Azam, Coastal Union pamoja na Namungo ndiyo kati ya zile ambazo zimeonekana kutangaza wachezaji wao wengi sana iliyowaacha ili kuweza kusajili wengine ambao watakuja kuchukua nafasi zao.

Kuacha wachezaji siyo jambo geni kwetu au duniani kwa ujumla bali kinachoonekana msimu huu ni mfumo mzuri wa kuwaacha kwa kuwatangaza kwa mashabiki kwa kichwa cha habari cha Thank You.

Hii imeonekana kuwateka sana mashabiki wa soka Tanzania nzima na unaonekana kuwa ni mfumo mzuri kama utaendelezwa kwa miaka kadhaa mbele.

Lakini pamoja na hayo, tunapenda kuzishauri timu nyingine ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara pamoja na Championship kutangaza wachezaji wao wanaowaacha mapema ili kuwapa nafasi ya kutafuta timu nyingine.

Ni jambo zuri kama watatangazwa mapema, kwanza wao watapata timu za kuchezea kama bado wanataka kucheza, lakini klabu waliyotoka nayo itakuwa na nafasi nzuri ya kuhakikisha kuwa inaziba pengo lake mapema.

Tumekuwa tukiona wachezaji wanatangazwa kuachwa mwishoni kabisa mwa usajili na wakati wanatafuta timu wanakuta usajili umefungwa, hii siyo sawa, watangazwe sasa ili waendeleze vipaji vyao.

Tumeona Erasto Nyoni muda mchache tu baada ya kutangazwa kuachwa na Simba amechukuliwa na Namungo, lakini angeachwa siku ya mwisho angeweza kukosa nafasi hiyo hata kama anakipaji.

Pamoja na hayo ukweli unabakia palepale kwamba soka ni mchezo unaochezwa kwa miaka michache katika ubora sawa na michezo mingine kwani haiendani na umri hivyo kila kitu kinapaswa kufanyika kwa umakini na kwa usahihi.

Columnist: Mwanaspoti