Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kila mmoja ajilinde na kuwalinda wenzake

05f9f7e2f2de54f22eeb920b93d3d06c.jpeg Kila mmoja ajilinde na kuwalinda wenzake

Thu, 18 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TANZANIA si kisiwa kisichofikika; bali nchi inayohusiana na mataifa mengine kwa nyanja mbalimbali zikiwamo za kibiashara na hata kuingilia kwa namna mbalimbali.

Hili lilikuwapo siku za nyuma hata kabla ugonjwa wa Covid-19 haujaingia nchini mwaka jana, ingawa haukudumu; ukaondoka mapema kutokana na ushirikiano wa Watanzania katika kuomba huruma wa Mungu na kufuata malekezo ya wataalamu wa afya na viongozi wa serikali.

Tuendelee kumshukuru Mungu na hata viongozi wetu wa kada mbalimbali wakiwamo wa serikali, dini na watalaamu wa afya kwa juhudi walizofanya kuhamasisha Watanzania kumuomba Mungu huku wakichukua tahadhari hali iliyowezesha ugonjwa huo ‘kuikimbia’ Tanzania.

Hali ilikuwa hivyo kwa Tanzania mwaka jana, wakati Shirika la Afya Duniani (WHO) likiwa limeutangaza ugonjwa huo unaosababishwa na virusi vya corona kuwa ni janga la kimataifa kutokana na namna unavyoambukiza kwa haraka na kuua idadi kubwa ya watu kwa muda mfupi.

Hadi jana kwa mujibu wa takwimu, zaidi ya watu milioni 121.29 wameambukizwa virusi hivyo na zaidi ya watu milioni 2.68, wamepoteza maisha.

Kutokana na juhudi zilizofanywa na Watanzania, ugonjwa huu mwaka jana ‘uliambulia’ maisha ya Watanzania 21, licha ya watu 509 kuambukizwa nchini.

Katika hili, juhudi za serikali na wataalamu wake hazina budi kupongezwa kwa dhati sambamba na wote walioomba kwa dhati huruma wa Mungu na hali ikatulia hadi sasa.

Takwimu za jana zinabainisha kuwa, kwa saa 24 watu 23,874 walikuwa wameambukizwa corona huku waliofariki dunia wakifikia 610 duniani kote. Hii inaonesha kuwa, bado hali ni tete duniani.

Kwa msingi huo, yapo mambo mawili makubwa yanayonifanya niseme: “Kila mmoja ajilinde ili kuwalinda wenzake.”

Kwanza, kama nilivyosema awali, Tanzania si Kisiwa, licha ya kuwa bado ipo salama dhidi ya janga la corona, juhudi tulizofanya mwaka jana hata kuushinda ugonjwa huu lazima tuendelee ‘kuzikumbatia.”

Kadhalika, yapo magonjwa mengine yanayohusika na mfumo wa hewa ambayo nayo, lazima Watanzania tuunganishe nguvu kuhakikisha kuwa, tunayashinda na ‘kuyafukuza’ ili sisi wenyewe tuwe salama na kisha tuwalinde wenzetu.

Yote haya tutafanikiwa kuyamudu endapo kwanza, tutaendelea kumwita Mungu bila kukoma kwa imani na matebndo yetu.

Katika matendo, ni kuendelea kusikia maelekezo ya viongozi na wataalamu wa afya kuhusu namna ya kuepuka magonjwa hayo ikiwa ni pamoja kuepuka misongamano na mikusanyiko isiyo ya lazima.

Watu waendeleze utamaduni safi wa kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka au kutumia vitakasa mikono na inapobidi, kuvaa barakoa.

Ile kasumba ya kushikana mikono katika misiba au kukumbatiana hovyo hovyo, ni vema iendelee kuepukwa kwa kuwa magonjwa ya mfumo wa hewa ‘hayana adabu.’

Ndio maana ninasema, kila mmoja akijilinda kwa kutekeleza maagizo na maelekezo ya serikali na wataa;lamu wa afya, atakuwa anatimiza wajibu wa kujilinda na kulinda haki na wajibu wake wa kulinda wenzake.

Columnist: www.habarileo.co.tz