Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kidume Mansour wa Manchester City kufuru tupu

Sheikh Masour.jpeg Kidume Mansour wa Manchester City kufuru tupu

Tue, 27 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Mbali ya Nasser Al Khelaifi kuna tajiri mwingine ambaye anasumbua sana vigogo barani Ulaya ambaye ni huyu Sheikh Mansour ambaye anamwaga pesa vile anavyojisikia kuhakikisha mastaa wote bora anawapata kwenye kikosi chake cha Manchester City.

Hivi karibuni alimsajili Erling Haaland aliyekuwa anatakiwa na vigogo wengi barani na anahusishwa pia kuwahitaji Kylian Mbappe na Jude Bellingham wanaomezewa mate pia na vigogo wengine wakubwa barani Ulaya, lakini je? Jamaa anatoa wapi jeuri hiyo? Twende sawa hapa.

ANAPIGAJE PESA

Jina lake kamili ni Mansour bin Zayed Al Nahyan. Jamaa anapata pesa kupitia kampuni yake ya Mubadala Investment Company ambayo inajihusisha na uchakataji wa mafuta na faida yake kwa mwaka hufikia hadi Dola 1 bilioni.

Kupitia kampuni hii jamaa amekuwa mmoja kati ya wajumbe wa kamati ya mamlaka ya mafuta ya Petroli wa Falme za Kiarabu na mwaka 2007 aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa mamlaka ya uwekezaji wa Falme za Kiarabu ya Emirates Investment Authority.

Mansour pia ana asilimia 32 ya hisa kwenye kampuni ya Kimarekani ya Virgin Galactic, pia ana hisa za asilimia 9.1 katika kampuni ya Daimler ambayo ndio kampuni mama ya utengenezaji wa magari ya Kijerumani ya Marcedes Benz Group na alinunua hisa hizo Machi 2009 kwa kutumia Dola 2.7 bilioni.

Achana na hiyo jamaa pia anamiliki kampuni ya Abu Dhabi Media Investment Corporation (ADMIC), ambayo inamiliki media mbalimbali za televisheni na magazeti.

Jumla ya utajiri wake unakadiriwa kufikia Dola 40 bilioni na anatajwa kuwa binadamu wa pili tajiri zaidi huko UAE sambamba na mashariki ya kati kwa ujumla.

Pia ni mwanasiasa, ambaye anashikilia wadhifa wa Waziri Mkuu wa UAE tangu mwaka 2009 na kupitia hapa pia anakunja pesa za kutosha.

Kwa makadirio kutoka vyanzo mbalimbali ni kwamba fundi huyu anakunja kiasi kisichopungua Dola 250 milioni kwa mwezi.

USAFIRI

Kwenye upande wa magari yapo ya kutosha tena yenye thamani kubwa ikiwa pamoja na Bugatti Veyrons, Ferarri 599XX, McLaren MC12, Ferrari F40, Mercedes CLK GTR, Mercedes G63 AMG, Range Rover na Lamborghini Reventon, yote hayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya Dola 30 milioni.

Jamaa anamiliki boti yenye thamani ya Dola 600 milioni ambayo inatajwa kuwa moja kati ya boti ghali zaidi duniani, ndani ya boti hiyo kuna huduma zote muhimu za kijamii.

Anamiliki pia ndege aina ya Boeing lakini hadi sasa bado haijajulikana ni aina gani ingawa vyanzo vinadai huenda ikawa kati ya Boeing 747, 767, au 787.

MSAADA KWA JAMII

Jamaa amekuwa akisaidia jamii kumpitia taasisi yake ya Khalifa bin Zayed Al Nahyan Foundation ambayo imekuwa ikitoa misaada ya kimasomo, matibabu na kusaidia nchi mbali mbali maskini kwenye majanga.

MJENGO

Anakaa kwenye makazi ambayo ameandaliwa na serikali kwa wadhifa wake wa Waziri Mkuu huko Abu Dhabi tangu mwaka 2009, hivyo hadi sasa bado haijajulikana hasa mijengo anayomiliki binafasi.

MAISHA BINAFSI

Mwaka 1995 alimuoa Sheikha Alia bint Mohammed bin Butti Al Hamed ambaye alibahatika kuzaa naye mtoto mmoja wa kiume aitwaye Zayed. Mansoor pia mwaka 2005, alimuoa Manal bint Mohammed bin Rashid Al Maktoum ambaye ni mtoto wa kiongozi wa Dubai Mohammed bin Rashid Al Maktoum, amezaa naye watoto watano, Fatima (2006), Mohammed (2007), Hamdan (2011), Latifa (2014) na Rashid (2017).

Columnist: Mwanaspoti