Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kiduku, katumia raundi 10 kushinda mikanda miwili

Kiduku Tye Bondia Twaha Kiduku akitangazwa mshindi

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Lilikuwa ni pambano la jasho, mashabiki walilazimika kusubiri uamuzi wa majaji kujua nani atavikwa ubingwa wa mabara wa UBO na ule wa PST baada ya dakika 30 kuisha. Ilikuwa ni Twaha 'Kiduku' Kassim tena, safari hii akiondoka na mataji mawili kwa mpigo, licha ya matokeo ya pointi kuwakwaza baadhi ya mashabiki wake, wengine wakiamini kama angekuwa na tageti, angemaliza pambano mapema. Mwenyewe alikiri kucheza na bondia mwenye kiwango bora, mwenye nguvu ambaye ilihitaji akili ya ziada kumpiga. "Alikuwa na nguvu, spidi na anayejua kujipanga vyema, ilihitaji mbinu zaidi kucheza naye, lakini kikubwa naishukuru menejimenti yangu, chini ya meneja, Ibrahim Nyange kwa maandalizi nimeshinda," alisema bondia huyo. Kocha wake, Pawa Ilanda alisema mpinzani huyo wa Kiduku (Iago Kiziria raia wa Georgia), hakuhitaji kucheza naye kwa haraka. Japo raundi ya tatu na ya tano, mashabiki wa Kiduku walitamani amalize pambano kwa TKO au KO baada ya kumweka kwenye tageti mpinzani wake na kuanza kumshambulia, bondia huyo namba moja kwenye uzani wa supermiddle nchini, alimpa nafasi ya kujipanda Iago na kurudi mchezoni. Kocha Ilanda alisema aina ya bondia waliyecheza naye, Kiduku hakupaswa kuwa na haraka ya kulazimisha matokeo. "Ilikuwa ni ngumu kumshambulia moja kwa moja, Iago ni bondia mwenye nguvu, ukicheza naye kwa kulazimisha unaweza kukutana na ngumi nzito ikakukalisha, ndio sababu nilitaka acheze boxing, tulimjenga kwenye foot work. "Kuna wakati ana fight (pambana) kuna wakati anacheza boxing na wakati ana score," alisema. Majaji wote walimpa ushindi wa pointi Kiduku aliyecheza nyumbani mjini Morogoro, majaji wawili wakitoa pointi 98-92 na mmoja pointi 97-93. Pambano lilivyokuwa Kwenye ukumbi wa Tanzanite, Kiduku alipanda ulingoni saa 5:52 usiku akitanguliwa na msanii, Afande Sele aliyeimba wimbo wa watu Pori akishangiliwa na mamia ya mashabiki ukumbini hapo, kabla ya kupigwa nyimbo za taifa la Georgia na Tanzania. Refarii, Anthony Rutha alianzisha pambano saa 6:06 usiku na Iago ndiye alianzisha mashambulizi kwa ngumi ya kudokoa ya mkono wa kushoto. Kiduku alijibu mashambulizi kwa ngumi ya kushoto iliyompata sawa Iago na kisha akaachia nyingine ya upper cut, huku mpinzani wake akijaribu kumpiga ngumi nyingi za tumbo kujaribu kumkata pumzi. Raundi ya pili, Kiduku alionyesha staili ya kuzungusha ngumi ya mkono wa kushoto kana kwamba anarusha kombeo, ili kumweka kwenye tageti mpinzani wake ingawa walipokezana kushambuliana kama ilivyokuwa raundi ya nne na sita. Raundi ya saba kama Kiduku angecheza kwa spidi, huenda angemaliza pambano hilo baada ya kumshambulia mfululizo mpinzani wake, lakini akampa nafasi ya kuvuta pumzi kabla ya kengele ya kumalizika kwa raundi hiyo kugongwa. Raundi ya nane Kiduku aliianza kwa kasi, lakini mpinzani wake alikomaa na kuanza kutumia mbinu ya kumkumbatia ili kupumzika huku akijibu mapigo na raundi ya tisa huku ile ya 10 nusura Kiduku aende chini kutokana na ulingo kuteleza, lakini alikuwa fiti.

Columnist: Dar24