Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Kaseja amelala usingizi wa peke yake

Kaseja Juma To Kaseja amelala usingizi wa peke yake

Sat, 29 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama mungu angenichukua mapema basi nisingeweza leo kuwasimulia mambo haya makuu katika ulimwengu soka katika dunia yenye watu takribani bilion 8.5 ni ngumu sana binadamu wote kuwa sawa ni ngumu sana kila mtu anakuwa na mlango wake wa kuingilia duniani na kuondokea hii ni kama Ibada.

Nayasema haya huku nikiitazama picha ya Juma kaseja kwenye vitabu vyangu vya kumbukumbu bahati nzuri vinanieleza mambo yake mema mengi aliyotutendea kwenye Ulimwengu huu hususani katika football yetu hii.

Bado nawaza huku moyo wangu ukimiminika damu nzito yenye asili ya mnyama simba nikikumbuka maisha ya kijana huyu aliyefanya makubwa na jezi ya Simba sports club lakini natamani isiwe kweli nayoyasikia kwenye ngome ya sikio langu.

Nimetazama kwenye vitabu vya Kumbukumbu vya Moro United, Mtibwa Sugar, Simba Sport club, Kuala Lumper Malasia (Yanga) bado sikumaliza nikaingia kwenye vitabu vya Mbeya City nikafika mbali zaidi nikaingia mpaka kwenye kabati la Watoza Ushuru wa Kinondoni hapo ndipo nilipokubali tuache muda uamue unachotaka.

Nipo naendelea kusoma vitabu vyako ulivyooandika na kutuachia kwenye vilabu vyote hivi huku nikiwa na hudhuni tele moyoni sawa Juma nenda nafasi hii finyu niliyoipata ya kuandika mema yako nahisi haitoshi hata kidogo nitaandika wakati mwingine.

Pengine hata macho yangu hayawezi kusadiki kweli ninayoisikia machozi yananitoka mithili ya mtoto mchanga pengine ni maumivu nikikumbuka moments zote nilizokuwa nikimtazama Juma K Juma akiwa langoni mwake mikono yangu inasita kuandika miguu yangu inatetemeka kwa hofu nashindwa hata kusimama mithili ya mtu mwenye degedege.

Pengine nashindwa kukubaliana na ukweli halisi kwamba Tanzania One Juma Kaseja amelala usingizi mzito katika chumba cha peke yake huko nyumbani kwake huku akiota ndoto ndefu ya safari ya maisha yake ya football mpaka mwisho wake.

Pengine yeye ndiye mwenye huzuni kuliko sisi sote kwa sababu pale atakapoamka na kugundua kuwa hayupo nasi katika soka la ushindani pengine ataumia sana.

Juma amelala Juma ametuacha peke yetu natamani rafiki zake wakina Amri Kiemba, Boniphace Pawasa, Ulimboka Mwakingwe, Shadrack Msajigwa, Nadir Haroub 'Canavaro' watusimulie habari zake njema.

Natamani mikono mitakatifu ya Edo Kumwembe kuona ikiandika makala ndefu zenye kuwakumbusha vijana kuwa Juma alikuwa ni mtu wa namna gani moyo unaniuma sana moyo unaniuma sana Juma kuachana na soka la ushindani pengine huyu ni role model wa vijana wengi kwenye hii soka yetu.

Baada ya kusikia kuwa Juma K Juma ameachana na soka la ushindani kwa takribani miaka 22 akicheza kwa mafanikio makubwa sana, kipa Juma Kaseja hatimaye amefanya maamuzi magumu kwa kutangaza kustaafu kucheza soka la ushindani.

Aiseee inaumiza sana lakini mimi ni nani niubishie muda umeandika kitabu cha maisha yako kizazi kwa kizazi kwenye football yetu hakika kitasomwa na vijana wengi wanaofuata nyayo zako.

Nidhamu na kujituma ndiyo ilikuwa msingi wako wa kukufikisha juu kabisa kwenye mafanikio yako nitakukumbuka kila siku nitakuheshimu kila Siku nakutakia kila kheri Tanzania One sisi tunakupenda.

Muda umeamua Juma atuache muda umeamua Kaseja atukimbie Much RESPECT the Living Legend Juma K Juma. We Love you Juma tuanaheshimu mikono yako salama iliyotupa heshima kwenye anga za kimataifa tunakupenda tutakupenda na upendo wetu hautokuwa na kikomo katu katu kwako ❤ Godbless You.

Acha ball itembee Ukinelewa Mimi umelielewa SOKA Imeandaliwa na; Simba Sunderland The Lion.

Columnist: www.tanzaniaweb.live