Hapo juzi Kajala na Paula wamezindua duka jipya na kubwa lenye hadhi ya Mall. Thamani ya duka hilo ni kubwa sana, sidhani kama kuna msanii au staa yeyote mwenye duka kama lile.
Swali la kujiuliza, Paula hana biashara, Kajala hana biashara, hela wametoa wapi? Huitaji kuumiza kichwa, Marioo ndiye ametoa hela ya mtaji kwa Paula kitu ambacho ni hatari sana.
Yuko wapi Harmonize baada ya kuhonga Range? Yuko wapi Rayvanny? Kinacholeta maswali mengi ni je, Marioo kwao wote wana uwezo? Kwa nini asiwainue ndugu zake, wana ukoo ili hata siku moja wamkumbuke?
Marioo kwanini hataki kujifunza kwa Diamond? Diamond kainua ndugu zake karibia wote, mpaka marafiki zake lakini pia anawekeza.
Leo Marioo anachukua pesa yote aliyoitolea jasho anagawa afu badaye atakuja kuachwa vibaya. Ni suala la mda.
Vipi kwa maoni yako, unadhani alichokifanya ni sahihi?