Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KWAKO KASHASHA: Tofauti ya makipa Metacha na Shikhalo ni hii tu!

Faruk Pic Data KWAKO KASHASHA: Tofauti ya makipa Metacha na Shikhalo ni hii tu!

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

TIMU ya soka kwa kawaida inakuwa na wachezaji wengi na inafanya kazi kama unit lakini ili iwe timu iliyokamilika kisheria kucheza mechi inakuwa na idara tatu

Idara ya ulinzi inayojumuisha kipa, idara ya kiungo na idara ya ushambuliaji ambazo zikiungana pamoja na kila moja ikatimiza majukumu yake, timu inakuwa na nafasi ya kushinda.

Kwa misingi hiyo tunawaona makipa wa Yanga kuanzia 2019/202 wako watatu ambao ni Faruk Shikhalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili, lakini Metacha na Shikhalo ndio wamekuwa wakitumika mara kwa mara

Siku zote wachezaji katika timu yoyote ile hawawezi kufanana. Lakini wana criteria (vigezo) zao zinazowafanya waweze kuchezea timu kama Yanga.

Lakini pamoja na Shikhalo na Metacha kuwepo katika Yanga wanaachana katika mambo mbalimbali. Kila mmoja ana udhaifu na ubora wake.

Metacha ana sporting personality (haiba ya kimichezo) kwa maana ya umbile lake. Ni mrefu na amejengeka. Metacha ni mchezaji mwenye umbile la walinda milango, mrefu na anaonekana kuwa na nguvu.

Kingine Metacha ni mtulivu na mpole. Lakini pia ana moderate footwork (mpangilio wa kimchezo). Matumizi ya miguu ni ya kiwango cha kawaida. Makipa kisheria wanaruhusiwa kutumia viungo vyote kwa kuangalia ni mahali gani alikuwa anaokoa mpira.

Sasa Metacha kwenye miguu sio mzuri kwani kuna nyakati kipa anatakiwa kutumia miguu yake kuokoa mpira, kuanzisha mchezo sasa Metacha hapo ana changamoto.

Pamoja na kazi nzuri anayofanya kuna wakati anaperform chini, ana-drop kiwango chake. Anaweza kucheza vizuri, lakini kuna wakati anacheza ovyo

Wakati mwingine Metacha licha ya kuaminiwa amekuwa ni slow reactor. Ni mchezaji ambaye anachelewa kufanya maamuzi. Kuna wakati anaweza kufungwa bao ambalo hutegemei kama atafungwa.

Ni mzuri kwenye distribution (usambazaji) hasa katika masafa ya karibu lakini huwa sio mzuri sana katika kupiga mipira inayokwenda masafa ya mbali.

Kuna mazingira Metacha anakuwa sio aggressive (mkali) hasa katika mipira ya juu, huku akiwa na umbo linalomwezesha. Kuna wakati unatakiwa kuwa aggressive lakini yeye huwa anakuwa mpole pindi anapokuwa uwanja.

Mara moja moja huwa anashindwa kucheza krosi lakini mara nyingi huwa anajitahidi kufanya hivyo.

Shikhalo ni mfupi kwa Metacha, lakini huwa mchezaji anayetamani kufanya vitu vikubwa lakini pia ni mzuri katika footwork. Katika matumizi ya miguu yuko sawasawa.

Ni mtu anayeweza kufanya directing kwa mabeki na kuwakumbusha majukumu yao na yeye anaongoza kwa vitendo.

Ni mzuri kwenye one against one. Mara nyingi anawaokoa Yanga katika baadhi ya mechi ambazo anakutana na washambuliaji wanaobakia naye ana kwa ana pindi wanaposhambuliwa.

Pia ni mzuri kwenye kusave mipira ya penalti. Nadhani ubingwa wa Yanga kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi, mchango wa Shikhalo ni mkubwa sana.

Shikhalo pia yuko quick katika kufanya reaction lakini pia ni kipa mzuri katika kusambaza mipira. Hapaniki na ana exposure (ufahamu). Akiwa under pressure (chini ya shinikizo) ni mzuri lakini ana tabia ya kucheza mipira ya pembeni.

Mahali ambayo wote hawa wawili wanafanana ni kwenye kukamata mipira lakini pia ni wachezaji wanaoonekana wanapenda kazi yao, wana passion

Kwa hiyo kitabia Metacha na Shikhalo hawana vituko na huwezi kusikia sijui Shikhalo na Metacha wamefanya nini na badala yake wana utulivu, ni wachezaji waungwana na wastaarabu

Vijana ambao wanafanya kazi yao kwa kufikiria mbali lakini lingine nawaoana wao kwa wao wana ushirikiano, waungwa na wanapenda umoja.

Ni wachezaji ambao hawana mambo mengi, watulivu na wana nidhamu na ni sehemu moja ya umoja ndani ya Yanga. Wote ni makipa wazuri lakini nani atumike na nani asitumike ni suala la mwalimu.

Kwa hiyo ni vijana ambao wanastahili kabisa kuwemo ndani ya Yanga kutokana na maisha yao ya ndani na nje ya uwanja.

Imeandikwa na Alex Kashasha

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz