Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

KIBANDA UMIZA: Jamaa ashindwa kuendelea na mechi kisa msiba wa JPM

Kibanda 1 Pic Data KIBANDA UMIZA: Jamaa ashindwa kuendelea na mechi kisa msiba wa JPM

Thu, 25 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

ILIKUWA Machi, 17, 2021 wakati tunatazama mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea dhidi ya Atletico Madrid, jaama mmoja aliyekuwa nyuma yangu ghafla alipaza sauti yake.

Jamaa huyo alisikika akisema kwa sauti kwamba aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati, Dkt John Joseph Pombe Magufuli amefariki Dunia.

Mzee mmoja wa makamo aliyekaa pembeni yake akamwambia; “Nahisi wewe hii hali ya hewa ya nje umeichoka, endelea tu kuropoka kama huna akili vizuri, shauri yako”

Jamaa aliyeambiwa maneno hayo akamgeukia yule mzee na kumuonyesha video ya Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mama Samia Suluhu akitangaza kifo cha mpendwa wetu Hayati Magufuli.

Mzee yule ghafla alipoteza nuru usoni bila ya kuongea neno akasimama na kuanza kutoka nje.

Mwanaspoti ilipata picha yake wakati anatoka nje, ambaye ni huyo aliyevaa fulana yenye mistari mistari.

Muda ambao anasimama kutoka nje kuna jamaa aliyeketi mbele naye aliwaonyeshea baadhi ya watu video ambao ndio hao unaoona wamesimama kwenye picha, kila mtu akizungumza la kwake.

Baada ya muda ni kama watu walipoteza hamu ya kuangalia mpira kwani wengi walitoka nje na tuliobakia ndani tulikuwa wachache sana. Ameenda Jembe.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz