Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

JICHO LA MWEWE: Mapokezi ya wakubwa mikoani na hatima ya ya 'Leeds' wetu

Mwewe Pic Data Mapokezi ya wakubwa mikoani na hatima ya ya 'Leeds' wetu

Tue, 1 Feb 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Maisha yanahama na mbwembwe zake. Siku hizi imezuka fasheni ambayo zamani haikuwepo. Wakubwa wa soka letu wamekuwa wakipokewa kwa mbwembwe nyingi wanapokwenda mikoani. Zamani wakubwa walikuwa wanaingia kimya kimya.

Labda kwa sababu walikuwa wanaingia na mabasi, lakini siku hizi wakubwa wetu Simba na Yanga huwa wanaingia mikoani kwa ndege. Umati wa mashabiki unawasubiri wakubwa wetu. Wengine wanajipanga barabarani.

Zamani hali kama hii ilikuwa inatokea pale tu wakubwa wakichukua taji nje ya nchi au nje ya mkoa. Kama vile Yanga walivyotwaa taji la Afrika Mashariki na kati pale Kampala Uganda mwaka 1993. Kama vile Simba walipoitoa Zamalek na kusonga mbele katika michuano mabingwa wa Afrika mwaka 2003 pale Cairo Misri.

Siku hizi watu wa mikoani wamechangamka. Wanashindana kuwapokea wakubwa wetu. Nini hatima yetu? Unajiuliza, majuzi Yanga walikwenda Mwanza kucheza dhidi ya Mbao katika michuano ya FA wakapokewa kwa mbwembwe zote. Huu ni mkoa ambao hauna timu ya Ligi Kuu. Bahati mbaya au nzuri sidhani kama wenyewe wanajali.

Kama ilivyokuwa zamani ndivyo tunavyorithisha vizazi vyetu. Nchi nzima imegawanyika kuwa Simba na Yanga, basi. Hata watoto wadogo wa mikoani nao wameingia katika mkumbo wa kufuata hisia za baba na mama zao. Hakuna anayetaka kuwa shabiki wa Prisons wala Mbeya City wala Geita Gold. Ni mwendo wa Simba na Yanga tu.

Nini matokeo yake? klabu zao zinakosa hamasa ya mashabiki wa nyumbani. Mashabiki ni roho. Simba na Yanga zinasonga mbele kwa sababu ya hamasa za mashabiki. Mikoani hatuna timu za namna hii. Labda kidogo Tanga ambako wamebakia mashabiki wachache wa asili wa Coastal Union na African Sports.

Lakini zaidi klabu hizi zinakosa pesa. Zinashindwa kujiendesha kwa sababu hazina mashabiki wala wanachama wanaojitolea kuziendesha klabu hizi. Bahati mbaya zaidi hata uwanjani mashabiki hawaendi. Siku pekee ambayo Mbao inaweza kupata mashabiki ni pale inapocheza na Yanga. Watajitokeza mashabiki waTATIZO

Siku hizi mashabiki hawaendi katika mechi za mikoani kwa sababu wanaangalia Simba na Yanga katika televisheni.

Columnist: www.mwanaspoti.co.tz