Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

JARIDA LA WANAWAKE: Mwanzo wa kupata viongozi wanawake ni sasa

Jarida La Wanawake (2) JARIDA LA WANAWAKE: Mwanzo wa kupata viongozi wanawake ni sasa

Mon, 21 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Kuzinduliwa kwa uandikishaji huo ni mwanzo wa Watanzania wote kujiandikisha na kupata kitambulisho kwa ajili ya kupiga kura ya maoni ya Katiba Pendekezwa pamoja na Uchaguzi Mkuu.

Katika kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kuafanyika Oktoba kupata Rais, Wabunge na madiwani, sasa ndiyo harakati zimeanza kwani hakuna muujiza katika kupiga kura ikiwa hujajiandikisha katika daftari hilo la kudumu.

Nasema hivyo kutokana na ukweli kuwa ikiwa wanawake tumedhamiria kuhakikisha katika uchaguzi huo wanapatikana viongozi wengi wanawake, basi ni vema tuanze sasa kwa kuhakikisha wote wenye sifa ya kujiandikisha katika Daftari hilo wanafanya hivyo.

Bila kujiandikisha wakati uandikishaji utakapofika mkoani kwako, utakuwa umepoteza nafasi yako ya kupiga kura kuchagua viongozi na kwa kuzingatia kuwa wapigakura wengi ni wanawake, na ni vema kujitokeza sasa na katika Uchaguzi Mkuu kupigia kura wanawake wenye uwezo wa kuongoza.

Kutokana na umuhimu huo ni vema wanawake tujipange katika shughuli zetu na kuhakikisha tunajiandikisha na kutunza kitambulisho hicho ambacho baada ya uchaguzi, kitasaidia katika masuala mbalimbali.

Ni dhahiri kuwa katika kuelekea Uchaguzi Mkuu, ni vema kuzingatia masuala ya kijinsia kwa kuhakikisha wanawake wengi zaidi wanaingia katika ngazi ya uamuzi ili kupunguza changamoto za unyanyasaji wa kijinsia.

Columnist: habarileo.co.tz