Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hongera shule za Serikali kwa ufaulu mzuri kidato cha sita

MSONDE NECTA 2 Hongera shule za Serikali kwa ufaulu mzuri kidato cha sita

Sun, 23 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

JUZI Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta) lilitangaza matokeo ya kidato cha sita mwaka huu yakionesha shule za Serikali zikifanya vizuri katika ufaulu ambapo kati ya shule 10 bora, nane ni za Serikali.

Katika matokeo hayo yaliotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde, mjini Zanzibar, ufaulu kwa ujumla umepanda kwa asimilia 0.03 kutoka asilimia 98.32 mwaka 2019 hadi asilimia 98.35 mwaka huu huku wasichana waking’ara zaidi kwa asilimia 0.89 zaidi ya wavulana.

Kufuatia matokeo hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa, ufaulu huo na kufanya vizuri kwa shule za serikali ni matokeo ya uwekezaji uliofanywa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitano.

Ni ukweli usiopingika kuwa, maboresho yaliofanywa na Serikali yaliyotumia zaidi ya Sh bilioni 588 kwa shule kongwe 73 nchini na nyingine 13 zinazoendelea kukarabatiwa na uwekezaji wa zaidi ya Sh trilioni 1.09 kugharimia mpango wa elimu bila malipo, umezaa matunda haya ya ufaulu.

Matokeo haya yameleta furaha kwa wazazi na Watanzania wote kwani pamoja na uwepo wa janga la ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (Covid-19) uliosababisha shule na vyuo kwa zaidi ya miezi mitatu nchini, wanafunzi hawa wa kidato cha sita na walimu wao, wamewafuta watu machozi.

Ikiwa kwa miaka mitano shule za Serikali zilizozoeleka kushika mikia au kufanya vibaya miaka ya nyuma zimeonesha matunda haya, basi ni wazi kuwa tukiipa Serikali miaka michache ijayo, kutakuwa hakuna tofauti kubwa kati ya ubora wa elimu inayotolewa katika shule za watu binafsi, taasisi za dini na zile za Serikali.

Hali hii pia itarejesha imani kwa shule za Serikali ambazo wengi wasingetamani watoto wao wasome huko kutokana na changamoto ya mazingira duni na yasio rafiki ya kujifunzia, lakini sasa zinageuka kuwa kimbilio lenye uhakika wa ufaulu mzuri hata kuliko shule binafsi kunakolipwa mamilioni ya pesa.

Kazi imebaki kwetu Watanzania kuunga mkono juhudi hizi za Serikali ili kutengeneza kizazi bora cha sasa na cha baadae kwani hakuna asiyefahamu kwamba, elimu ndio ufunguo wa maisha na ili tupate mafanikio ya kiuchumi, tunahitaji.

Columnist: habarileo.co.tz