Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hivi ndivyo utalii wa matibabu utakavyoinufaishsa Tanzania

B5cb0d77162a0f19e409e832a744abb2 Hivi ndivyo utalii wa matibabu utakavyoinufaishsa Tanzania

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

TUNAENDELEA na makala haya yanayoangazia namna uwekezaji mkubwa unaofanyika kwenye sekta ya tiba Tanzania, unavyoonesha kwamba muda si mrefu Tanzania itakuwa kitovu cha utalii wa matibabu Afrika.

Tukaona kwamba kutokana na gharama kubwa za matibabu katika mataifa yaliyoendelea sambamba na muda mrefu wa kusubiri, nchi inavyoboresha mfumo wake wa tiba kama inavyofanya Tanzania itasababisha wageni wengi kuja kutibiwa Tanzania. India ni moja ya mfao mzuri.

Tumeshaona namna kanda zote nchini zilivyosheheni hospitali za kanda zinazotoa tiba murua zikiwemo za kibingwa na ukweli kwamba sasa hivi huduma nyingi za tiba ambazo tulikuwa tunazifuata nje ya nchi zinapatikana hapa hapa Tanzania.

Hali kadhalika tuliona kwamba, mbali na hospotali hizi kuwa na vifaa vya kisasa, pia zina watalaamu wa kitanzania wanaotoa huduma za kibingwa.

Jana tuliona namna ambavyo mambo kama upandakizaji wa figo unavyofanyika sasa kwa ufanisi hapa Tanzania, matibabu ya mfumo wa juu na kati wa chakula (Gastroenterology) na kwamba upandikizaji wa uroto (bone marrow transplant) pia unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Tulimaliza kwa uangalia namna Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) zinavyoendelea kuwa kitovu cha taina katika eneo hili la Afrika Mashariki na Kati.

Tanzania katika kuhakikisha inatimiza azma ya kuwa nchi ya viwanda na kujitosheleza kwa bidhaa ndani ya nchi imedhamiria kuwekeza kwenye uzalishaji wa ndani ambapo katika miaka takribani sita, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dk John Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuanzisha viwanda vya dawa, vifaa tiba na vitendanishi.

Katika muda mfupi Tanzania itakuwa na viwanda visivyopungua 30 baada ya wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuanzisha viwanda vya dawa na vifaa tiba ambapo baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na M-Pharmaceuticals Ltd, Zinga Pharmaceuticals Ltd kilicho eneo la Zinga Bagamoyo, Vista Pharmaceutical Ltd, Kairuki Pharmaceuticals Ltd, Bahari Pharmaceuticals Ltd vilivyojengwa eneo la Zegereni mjini Kibaha pamoja na viwanda vingine katika mikoa mingine.

Utalii wa matibabu unapelekea moja kwa moja kukuza uchumu wa nchi kupitia mapato yanayopatikana kupitia utalii na sekta zingine zinazoshabihiana.

Nchi nyingi zimekuwa zikiweka mazingira mazuri ya utalii wa matibabu kwa ajili ya kukuza na kuchochea uchumi wa nchi zao. Mfano wakati wa mdororo wa wa kiuchumi wa mwaka 1997 kwa Bara Asia na 2008 kwa dunia, nchi nyingi za Asia na Mashariki ya Mbali ziliboresha mazingira ya Utalii wa Matibabu na kupelekea kuwa chanzo kikuu cha fedha za kigeni.

Ukichukulia nchi kama ya Thailand iliweza kuongeza mapato yake kutoka dola za Marekani milioni 340 kwa mwaka 2010 hadi kufikia dola milioni 622 katika mwaka 2013 ikiwa na ukuaji wa zaidi ya asilimia ishirini hivyo kuchangia kwa asilimia 0.16 ya GDP katika mwaka 2013.

Watalii hawa wa matibabu wataongeza mapato moja kwa moja kupitia ununuzi wa vyakula, malazi pamoja na utalii wa ndani. Hivyo basi, utalii wa matibabu haunufaishi sekta ya afya peke yake bali unakuza uchumi kwa wafanyabiashara wadogo, mahoteli, usafiri na pamoja na miundombinu.

Utalii wa matibabu utasaidia sana kuongezeka kwa fursa za ajira katika sekta ya afya na isiyokuwa ya afya. Mwaka 2007 utalii wa matibabu ulitengeneza jumla ya ajira 20,000 ambapo kati yake ajira 13,000 zilikuwa zinatokana na sekta isiyohusiana na afya.

Kupitia utalii huu, vituo vya kutolea huduma vitakavyohusika na utalii wa matibabu vitaweza kuongeza maslahi kwa watumishi wake hivyo itasaidia kupunguza utofauti wa mishahara ya ndani na nje ya nchi. Hii itafanya wataalamu wengi walio nje nchi kuamua kurudi kulitumikia taifa lao.

Utalii huu wa matibabu utasaidia sana kuvutia madaktari bingwa ambao kwa sasa wanafanya kazi katika nchi mbalimbali kurudi kulitumikia taifa lao. Hii ni kwa sababu kwanza wanakuwa na fursa ya kufanya kazi katika vituo vingi vilivyo ndani ya nchi lakini pia itavutia sana hawa wataalamu kurdi au kutofikiria kwenda nje kwani watakuwa na uhakika wa maslahi yanayoendana na mazingira bora ya kazi zao.

Kwa nchi nyingi duniani, utalii wa matibabu unafanyika katika vituo vya huduma vya binafsi na vituo vya umma ambavyo vinakuwa vimeweka maeneo maalumu/binafsi kwa ajili ya wagonjwa wa nje.

Ili kuweza kuwavutia wageni kuja kupata matibabu vituo vingi vya afya vimewekeza katika kupandisha hadhi vituo vyake, kuboresha miundombinu ya vituo, kununua vifaa vya matibabu vya kisasa pamoja na kuvutia wataalamu zaidi kuja kufanya kazi katika vituo vyao.

Lazima tutambue kwamba sekta ya utalii wa matibabu ni sekta iliyo na mashindano makubwa kwa sababu inaingiza fedha nyingi za kigeni. Hivyo, basi ili kuweza kuvutia watalii wa matibabu tunatakiwa kuendelea kuwekeza katika teknolojia katika vituo vya kutolea huduma.

Watalii wa matibabu wengi huvutiwa na nchi zilizo na vituo bora na zinazotoa huduma za matibabu zilizo katika kiwango cha juu (world class healthcare facilities). Watoa huduma wanashauriwa kuwekeza katika teknolojia na uboreshaji wa huduma za matibabu kwa kuwa na vifaa tiba vya kisasa vya upasuaji na matibabu mengine mbalimbali ili kuvutia watalii wengi nchini.

Kwa kuwa watalii wa matibabu watahitaji matibabu kwenye ngazi ya hospitali za Kikanda na Kitaifa ambazo tayari upatikanaji wa huduma unaendana na viwango vya kimataifa basi ni sharti vituo hivyo viendelee kuwekeza katika teknolojia ili viweze kuendana na matakwa ya kimataifa.

Mfano hospitali hizo zinapaswa kuwa na mifumo mizuri ya mitandao ya kijamii ambayo inapatikana wakati wote, kuwe na taarifa za kutosha za matibabu yanayofanyika katika kila hospitali husika na kwa nini wanaona mtalii wa matibabu atanufaika na matibabu hayo.

Aidha, hospitali hizi kubwa za kikanda na kitaifa zinapaswa kuwa na umahiri katika maeneo machache (area of specialization) ambayo zitahudumia watalii wa matibabu kwa ufanisi mkubwa.

Mfano ilivyo kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyojikita na matibabu ya moyo, Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili iliyojikita katika matibabu ya mifupa, mishipa ya fahamu na ubongo na Taasisi ya Saratani Ocean Road iliyojikita na matibabu ya saratani.

Hospitali ya Muhimbili inaweza ikajikita kwenye baadhi ya matibabu kama ya upandikizaji wa figo na upandikizaji wa uroto na hospitali zingine zikajielekeza katika eneo ambalo linaweza kuwa na ushawishi mkubwa kwa watalii wa matibabu waache kwenda kwingine na badala yake waje Tanzania.

Kitu kingine muhimu ni kwa bima za ndani ya nchi kama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuanza mchakato wa kuingia ubia na makubaliano na baadhi ya bima za afya za kimataifa ili kuwapa nafasi wagonjwa wa nchi hizo kusafiri na kuja kutibiwa Tanzania.

Kuna nchi nyingi gharama za matibabu ni kubwa sana kwa hiyo pindi watakapoona gharama ni za chini na zilizo na ubora watamiminika na kuja kupata matibabu nchini Tanzania. Kwa mfano nchi ya Singapore imeruhusu wanufaika wa bima za afya kwenda kupata matibabu nchini Thailand kwa kuwa gharama kubwa za matibabu nchini Singapore ni kubwa zaidi ya zile za Thailand.

Pia kuna haja ya kufikiria ujenzi wa hoteli jirani na hospitali za kutolea huduma kwa sababu nyingi mfano kuna baadhi ya watalii wa matibabu huwa ni wagonjwa sana hivyo hawahitaji kusafiri umbali mrefu kwenda hospitalini.

Kwa kuwa hospitali nyingi zina wodi za wagonjwa wa kawaida na kukosa wodi maalumu za binafsi (private/VIP wards) basi zinashauriwa kutafuta vyanzo vya fedha ili kujenga wodi maalumu kwa ajiri ya hawa wageni.

Baadhi ya nchi hujenga hoteli maalumu jirani na hospitali hizo kwa ajiri ya watalii wa matibabu ambapo wanakuwa na uwezo wa kupata huduma zote kama wako wodini.

Kwa Tanzania, vituo vya kutolea huduma vinaweza kuingia ubia na/au makubaliano na Bima za Afya kama NHIF ili kuwawezesha kujenga hoteli zitakazosaidia kupokea watalii wa matibabu.

Wodi binafsi/ hoteli hizo zinatakiwa kuwa za kisasa zinazokuwa na mifumo yote ya mitandao kama internet, CCTV Camera na mawasiliano mengine ili kumfanya mgeni kujisikia kama yuko nyumbani kwake.

Mwandishi wa mkala haya ambaye ni Ofisa Mwandamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ni msomaji wa gazeti hili.

Columnist: www.habarileo.co.tz