Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Hii ndio siri ya mafanikio Crotia Kombe la Dunia 2022

Croatia Ntional Team Kikosi cha Timu ya Taifa Croatia

Mon, 12 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Croatia, Bruno Petkovic amesema utimamu wa kiakili wa timu hiyo ambao umeiwezesha kushinda mara mbili kwa mikwaju ya penalti kwenye Kombe la Dunia una mizizi mirefu katika harakati za kupigania uhuru wa nchi hiyo.

Petkovic alifunga goli la jioni kabisa kuisawazishia Croatia muda mfupi baada ya Neymar Jr kuitanguliza Brazil katika mchezo wa robo fainali ya kombe la Dunia kabla ya kikosi hicho kinachonolewa na Zlatko Dalic kushinda kwenye matuta.

"Nadhani moja ya sababu ya ari hii ya ushindi ni kwasababu sisi ni Nchi ndogo.Ingawa kama wachezaji sisi ni vijana, tunajua jinsi nchi yetu ilivyoundwa na kupata uhuru miaka ya 1990. Tumejifunza haya kutoka kwa wazazi wetu. Tumejifunza kupambana, kufanya kazi kwa bidii na tunafahamu bila hivyo hufiki popote," ameongeza Bruno Petkovic (28)

Baadhi ya wachezaji wakongwe kwenye katika timu wa ufahamu mkubwa juu ya mzozo wa Balkan katika miaka ya 1990. Kiungo mkongwe Luka Modric aliishi maisha ya kutangatanga ikiwemo kuishi kama mtumwa kwa miaka 7 akiwa kijana mdogo.

Mlinzi Dejan Lovren akiwa na umri wa miaka mitatu yeye na familia yake walilazimika kuondoka nyumbani kwao kukimbia vita vilivyoua takribani 100,000 na kutimkia Ujerumani.

Croatia ilipata Uhuru mnamo 1995, baba yake Luka Modric alipigani vita huku Babu yake kwa jina Luka akiuawa na waasi kutoka Serbia. Croatia ilishiriki kombe la Dunia kwa mara ya kwanza kama Taifa huru mnamo 1998 kabla ya kutolewa na Mabingwa wa mwaka huo Ufaransa kwenye hatua ya nusu fainali.

Ufaransa walizima ndoto za Croatia kutwaa kombe hilo kwa mara nyingine mnamo 2018 walipokutana fainali kwa ushindi wa 4-2.

Nchi hiyo ambayo ina takribani raia milioni 4 tu imetinga nusu fainali kwa mara nyingine ambapo mbele yake yupo Messi na Argentina kabla ya kumvaa mmoja kati ya Ufaransa au Morocco kwenye fainali.

Columnist: www.tanzaniaweb.live