Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

HISIA ZANGU: Mkude anavyoimarisha kikosi cha Uganda

101680 Mkude+pic HISIA ZANGU: Mkude anavyoimarisha kikosi cha Uganda

Wed, 17 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Edo KumwembeMore by this Author MMOJA kati ya wachezaji bora uwanjani pambano la Ijumaa usiku kati ya As Vita dhidi ya Simba pale Kinshasa alikuwa Taddeo Lwanga. Alicheza vizuri sana na kutimiza majukumu yake. Ilituacha mdomo wazi hasa ukizingatia kwamba katika michuano ya kombe la mapinduzi wiki chache zilizopita hakuwa fiti kiasi hiki.

Taddeo alicheza katika nafasi ya staa wetu wa Tanzania, Jonas Mkude ambaye alisimamishwa kwa matatizo ya utovu wa nidhamu. Simba haikupata matatizo yoyote katika nafasi hiyo na waliondoka na ushindi muhimu ugenini. Inasemwa kwamba wachezaji wenyewe wa Simba hawataki Mkude acheze kwa sasa.

Mchezo wa mpira wa miguu unakwenda kasi kama ambavyo maisha yetu yanavyokwenda. Ghafla nafasi ya Mkude huyu Taddeo ameitendea haki. Kabla hata Taddeo hajafika tayari Simba waliiibabua Platinum ya Zimbabwe bila ya Mkude.

Kuna madhara ya aina mbili wakati mchezaji kama Mkude anapokuwa hachezi katika kikosi cha Simba. Hii nchi haina wachezaji wengi mastaa wanaocheza nje. Tunawategemea akina Mbwana Samatta, Simon Msuva, Thomas Ulimwengu waje waungane na mastaa wanaocheza timu kubwa nchini kwa ajili ya kutengeneza kikosi kizuri cha timu ya taifa.

Majuzi kocha wa zamani wa timu ya Taifa, Ettiene Ndayiragije alibebeshwa lawama zisizo zake katika uteuzi wa timu ya taifa. Achilia mbali kumuacha, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ ambaye wengi hatukuhafiki, ukweli ni kwamba wengine walistahili kuachwa kwa sababu hawapati nafasi katika vikosi vya timu kubwa.

Columnist: mwanaspoti.co.tz