Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

HISIA ZANGU: Luis Miquissone anauzwa, hatujui tu dau lake

Luis Miqusson Pic Data HISIA ZANGU: Luis Miquissone anauzwa, hatujui tu dau lake

Tue, 2 Mar 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

KWAMBA Mmakonde wa Simba, Luis Miquissone hauzwi sio kweli. Wakati fulani tajiri wa Simba alikaririwa akidai kwamba Miquissone na wachezaji muhimu klabuni hawatauzwa kwa sababu Simba inasaka mafanikio katika soka la Afrika kwa sasa. Wakati mwingine unakutana na mashabiki wa Simba ambao wanatamba mitaani wakidai kwamba Miquissone hauzwi kwa sababu jambo hilo litadhoofisha timu. Wanaamini kwamba Simba haistahili kuwauza Miquissone wala Clatous Chama.

Kiwango cha Miquissone katika pambano dhidi ya Al Ahly kimewaacha mashabiki wa Simba na hofu kwamba muda wowote kuanzia sasa wababe hao wanaweza kuweka dau la kumtaka Miquissone mezani. Binafsi nahisi uwezekano huu upo. Kama si kwa Al Ahly wenyewe basi hata kwa miamba mingine ya soka kutoka Afrika Kaskazini.

Wanaoamini kwamba Simba haiwezi kumuuza Miquissone wanajidanganya tu. Simba inaweza kumuuza Miquissone hata wakati huu michuano ya Afrika ikiendelea. Tatizo letu tumezowea usajili wa bure au wa pesa kidogo. Umaskini unaathiri akili zetu.

Kama Al Ahly wakija kwa Miquissone hawatakuja na pesa yetu ya kitoto tuliyozoea. Watakuja na pesa ambayo hatujazoea na viongozi wote wa Simba wataonekana wajinga kwa kushindwa kumruhusu Miquissone aondoke zake. Watakuja na pesa kamili ambayo haitaacha maswali. Kwa umri wake wa miaka 25 Al Ahly wanaweza kuweka mezani dau linaloanzia Dola 1.5 milioni. Kwao ni pesa ya kawaida lakini kwetu sisi ni pesa ya ajabu. Hakuna mchezaji aliyewahi kuuzwa wala kununuliwa kwa nusu tu ya hizo pesa. Unazikataaje?

Columnist: mwanaspoti.co.tz