Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Guardiola anapoamua kurithisha starehe na mateso kwenye soka kwa wajukuu wa Cruyff

Pep With Arteta.jpeg Guardiola anapoamua kurithisha starehe na mateso kwenye soka kwa wajukuu wa Cruyff

Mon, 23 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Mziki wa Hip Hop nchini,Stamina aliwahi kuimba wimbo alioupa jina la 'Like Father Like Son' akimaanisha vile alivyo Baba ndivyo atakavyokuwa Mtoto.Wengine wakasema Mtoto wa nyoka Ni nyoka.Hawa wote walipita kwenye lugha yenye maana Moja katika mifano tofauti.

Huku kwenye Mchezo wetu pendwa wa Mpira wa miguu imejitokeza familia Moja inayojulikana kwa jina la Total Football na Wengine wakajiongeza kidogo kwa kujiita Familia ya Soka la Tik Taka.Lakini zote zinatokea kwenye familia ya Mpira pasi (Haijalishi Ni pasi fupi fupi na za haraka au pasi fupi fupi huku mwendo ukiwa wa Kawaida).Yaani timu inakuwa inaumiliki Mpira mda mwingi kwenye zile dakika za Mchezo.

Hizi Ni familia mbili ambazo zina-share Baba Mmoja.Zimetoka kwa Baba Mmoja aitwae Sir Hendrick Johannes Cruijff maarufu kwa jina la Johan Cryuff.Ni Kama vile Juma na Mwajuma au John na Yohana.

Huyu Johan Cryuff ndiye Baba wa hiyo familia ambayo ndani ya familia yake alizaliwa Pep Guardiola Kisha KUPITIA Pep wakazaliwa kina Mikel Arteta,Xavi Hernandez na Erik ten Hag.

Vinasaba (DNA) alivyonavyo Johan Cryuff ndivyo vinapatikana kwa Pep Guardiola amemrithisha Xavi Hernandez wa Barca,Eric ten Hag wa Ajax na Mikel ARTETA wa Arsenal.

Style yao (Falasafa) soka la Makocha hawa ambao wamepita kwenye mikono salama ya Genius wa Mpira,Pep Guardiola inafanana kwa asilimia kubwa.Wote wanapenda kuufanya Mpira kwao uonekane kama starehe.Mchezaji afurahie kucheza soka huku Mpinzani akiuona Mpira ni mchezo mgumu.

Pep na Eric ten Hag walikutana wote wakiwa Bayern Munich ambapo Pep alikuwa Kocha wa Kikosi Cha Kwanza Cha Bayern huku Hag akiwa Kocha wa Kikosi Cha Pili.Xavi Hernandez alifundishwa na Pep huku Arteta akiwa amekutana na Pep Kama Msaidizi wake pale Man City kabla ya Arteta kutua Arsenal.

Wote hawa wanapenda timu zao zicheze Mpira wa pasi,Mpira wa kuvutia (TOTAL FOOTBALL ambayo iliasisiwa na Johan Cryuff).Wanataka timu zao ziwe Zina shinda na tena zishinde huku zikiwa zimecheza soka safu.Ukiangalia hata ki-mbinu na ki-ufundi wanafanana sana.

Mfano Mwalimu wao Pep Guardiola Yeye huwa anamfanya Riyad Mahrez Kama Isolated Player (Mchezaji aliyetengwa pale timu inapokuwa haina Mpira ).Timu ikishapata tu Mpira Basi Space ya Kwanza kuifikiria Ni ile aliyopo Mahrez.

Mahrez akishaupata Mpira (Hata asipokuwa na Mpira tu ilimradi Mpira uwe unamilikiwa na City) Basi ataanza kuingia ndani kwenye Left Half space Kisha ile space aliyoiacha (Mahrez) inakuwa covered na Wingback/Fullback wa upande huo.

Arteta yeye huwa anamfanya Bukayo Saka Kama isolated Player pale timu inaposhambuliwa ili pale tu ipatapo Mpira yeye ndio huangaliwa zaidi.Mfumo mzima wa timu umetengenezwa kwaajili yake kuwa akipata Mpira iwe rahisi kutengeneza move ya kwenda mbele.

Hiki Ndicho anachokifanya Xavi kwa Dembele pale Barcelona (Angalia mechi dhidi ya Real Madrid).Na pia Ndicho Erik ten Hag amekifanya kwa Antony pale Ajax.

Master Xavi Hernandez,Mikel ARTETA pamoja na Erik ten HAG wote Ni wazuri kwenye kuvumbua na kuendeleza vipaji vya Wachezaji hasa makinda Kama ilivyo kwa Mwalimu wao Pep.Mfano Arteta kwa Emiry Smith Rowe,Odegaard,Aaron Ramslade pamoja na Bukayo Saka.Xavi Hernandez kwa kuendeleza na kukuza viwango vya Wachezaji mfano DembelePedri,Gavi,Ferran Torres nk.

Juzi Xavi Hernandez alikuwa anamtesa Babu Carlo Ancelotti pale Santiago Bernabeu.Don Carlo alipigwa Goli nne bila huku akiishia kutafuta Big G tu.Ni Kama vile ambavyo Pep alimfanya aliyekuwa Kocha wa Manchester United,Sir Alex Ferguson pale Wembley kwenye Fainali ya UEFA Mwaka 2011.

Ukienda kule Uholanzi,Eric Ten Hag amekuwa Kama Daktari dhidi ya Wagonjwa.Kila weekend anagawa dozi atakavyo.Kwake kushinda Goli 3+ kwa mechi moja imekuwa Kawaida Kwake.Hivi ndivyo Mikel Arteta anachokifanyia kazi pale kwa Malkia Elizabeth.

Wazee wetu walipata Manyanyaso kutoka kwa Johan Cryuff,Sisi tunayapata Kutoka Pep Guardiola na watoto zetu watayaonja Kutoka kwa Xavi,Arteta na ten Hag.Mateso yanaendelea.TUJIANDAE.

Columnist: www.tanzaniaweb.live