Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Garikubwa: Simba ilinituma kwa mganga

Gari Kubwa Mganga Garikubwa: Simba ilinituma kwa mganga

Fri, 17 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Jana tuliona jinsi ambavyo Gari Kubwa alivyokuwa akielezea maisha yake kwenye kikosi cha Simba na Yanga na jinsi alivyopata mafanikio akiwa na timu hizo, leo anaendelea kuzungumzia mambo mengi lakini akifunguka jinsi alivyokwenda kwa Mganga, lakini mwisho anawashauri Simba na Yanga kwenye michuano ya kimataifa inayoendelea...

NI SIMBA DAMDAM

Garikubwa anaweka wazi kuwa akiwa mtoto aliipenda sana Simba akieleza kuwa siku moja akiwa na watoto wenzake wakicheza, mpira ulienda karibu na mbwa aliyekuwa amefugwa na wote waliogopa.

“Kwahiyo nikajisogeza taratibu nikauchukua ule mpira nikaurudisha uwanjani tukaendelea na mchezo kuanzia hapo wakasema mimi Simba nikafurahi ila baada ya kukua nikaweka ushabiki pembeni nikafanya kazi,î anasema mkongwe huyo anayejivuani kuacha alama nzuri kwenye soka.

“Majimaji FC niliipa ubingwa Kombe la Muungano mwaka 1998 na kushiriki klabu bingwa kwa mara ya kwanza, Yanga tukatwaa ubingwa klabu bingwa Mashariki 1992, Simba nikaipa ubingwa wa Kombe Hedex,” anasema staa huyo.

Hivi karibuni Simba ilifanya uchaguzi wao mkuu ambao anadai anatamani angewania nafasi ya kuiongoza klabu hiyo.

“Changamoto ilikuwa nauli kwa sababu kutoka hapa kijijini hadi ufike Dar es Salaam na kurudi ni gharama kubwa lakini nilitamani sana nikagombee nafasi ya mjumbe kwa mojawapo wa timu hizo kwenye chaguzi zao,” anasema

ALIVYOIKACHA SIMBA

Unaambiwa wakati akikipiga Ushirika, beki huyo aliwindwa sana na miamba ya soka, Yanga na Simba lakini mwisho aliamua kujiunga Yanga kutokana kitita cha pesa alichowekewa kulinganisha na watani zao.

Anasema wakati wa usajili mwishoni mwa miaka 1992 alipokea Sh 200,000 kutoka kwa kigogo na Mwenyekiti wa Simba, Priva Matema na kupanga kumuweka kambi nzuri, lakini Abbas Gulamali alicheza rafu na kumbeba juu juu.

“Wawili hao walikuwa na ushawishi mkubwa kuanzia Stars na hizo Simba na Yanga, nilianza kupokea Sh 200,000 kutoka kwa Matema lakini Gulamali aliniwekea Sh 800,000 sasa jiulize enzi hizo ningefanyaje,”

Anaongeza katika makubaliano yao ilikuwa ni kupewa Sh 1.5 ambapo pesa hiyo ndio ulivunja rekodi kwenye soka kuungana na Jonas Lunyamila kuwa wachezaji wawili nchini kuchukua pesa ndefu.

MAISHA YA MTAANI

Anasema muda mwingine hukosa hata msaada wa kifedha hata Sh 100 ya kunywa maji kwani wengi huamini ni mtu mkubwa mwenye kipato japokuwa uhalisia wake ni tofauti na wanavyojua.

“Utakuta sehemu za mkusanyiko watu wananiogopa lakini hata hivyo, nimeishi sana nje ya Kyela kwahiyo kupata watu wa karibu zaidi inakuwa ngumu, ila nashukuru watu ninao wengi,” anasema.

TUKIO KUBWA

Anaeleza tukio ambalo hatalisahau ni kipindi akicheza Simba wakiwa mazoezini alidondokea mpira ambao ulimsababishia madhara makubwa hadi kustaafu soka mwaka 2004.

“Nilikaa hospitali kwa miezi tisa nikifanyiwa upasuaji na ndio ikawa mwisho wangu kucheza mpira uwanjani hadi leo nipo hapa kijijini nashukuru naendelea vizuri,” anasema Martin.

ATINGA KWA MGANGA

Anasema wakati anatua Simba aliikuta ikiwa na wakati mgumu kwani haikufanya vizuri na tatizo lilikuwa kwa uongozi ambao walimdhulumu mganga wakati wa mechi zao za kimataifa.

Anabainisha kuwa akiwa nahodha alipewa jukumu la kwenda kwa mganga huyo na kukabidhiwa Sh 500,000.

“Nilienda nikamkuta akachukua ile pesa akaisambaza ndani akafukua sebuleni kulikuwa na chupa ya maji akaifungua kama shampeni akasema tayari mizimu imekubali nendeni na tangu hapo Simba ikaanza kufanya vizuri,” anasema Martin.

HISTORIA YAKE

Majina yake halisi ni Willy Martin Mwandola mzaliwa wa Kyela katika miaka ya 1969 na ni mtoto wa tatu kwa baba na wa tano kwa mama, alisoma Shule ya Msingi Lubaga wilayani humo.

Alianza kucheza soka akiwa darasa la sita katika timu ya Boma iliyokuwa Ligi ya Mkoa wa Mbeya na alipomaliza elimu ya msingi mwaka 1988 alichukuliwa na aliyekuwa Kocha Mkuu wa Ushirika Moshi iliyokuwa Ligi Kuu, Dan Koroso.

Ushirika aliitumikia tangu 1988 hadi 1991 kabla ya kutua Yanga hadi 1995 kisha kujiunga na Majimaji hadi 2000 na kumalizia Simba alipostaafu rasmi 2004 huku Taifa Stars akiichezea miaka sita mfululizo tangu akiwa Ushirika.

UBINGWA NA MASTAA BARA

Anasema kwa misimu mitatu mfululizo Yanga imekuwa bora na imeitangaza zaidi Tanzania kwenye medani za soka, akisema hata msimu huu wanaweza kutetea taji na kwamba kupanda kwa kiwango cha ligi Afrika, Yanga pia wanahusika.

“Kuhusu ubingwa w wa msimu huu, Yanga inaweza ila iwe makini na Simba nyuma siyo mdogo maana wamesajili vizuri sasa hivi, nafurahia namna timu hizi zinavyopambana kuitangaza nchi kwenye soka la nje.

“Kuhusu wachezaji ninaowaona bora ni Henock Inonga na Yanick Bangala ila usajili wa Saido Ntibazonkiza pale Simba umeleta kitu cha tofauti yule Clatous Chama ni wa kawaida,” anasema beki huyo.

MAKUNDI CAF

Simba na Yanga ndizo zinawakilisha nchi kimataifa, ambapo wekundu wapo Ligi ya Mabingwa Afrika, huku watani zao wakipeperusha bendera upande wa Kombe la Shirikisho.

Timu hizo zilianza vibaya michuano hiyo ambapo zikicheza ugenini Simba ililala bao 1-0 dhidi ya Horoya, ilhali Yanga ikifa 2-0 mbele ya US Monastir.

Simba itakuwa tena Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam Jumamosi kuikaribisha Raja Casablanca, huku Yanga ikishuka uwanjani hapohapo Jumapili kuipokea TP Mazembe.

“Lazima watumie nafasi kufunga mabao ya mapema ili kuwatoa mchezoni wapinzani, hizi ni timu kubwa kwa rekodi zao, Simba na Yanga inaweza kushinda kama itaweka mipango sawa.”

Columnist: Mwanaspoti