Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Ganesh Kumar mkali wa kuchora picha kwa kutumia mdomo

Ganesh Kumar Drawer Ganesh Kumar mkali wa kuchora picha kwa kutumia mdomo

Fri, 7 Apr 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Yapo mambo ukiambiwa, ukisoma au kusikia habari zake huwezi kuamini na hata ukiyaona utapata abu kuamini na kusema ni kiini macho (umetekwa na ushirikina). Lakini dunia yetu hii ina maajabu mengi katika kila fani na hii pia ipo katka sanaa.

Kwa kawaida panapozungmziwa habari za kuchora picha.iwe kwa kalamu, chaki, kiiti, brashi au kitu chochote chengine moja kwa moja huwa tunajua huyo mchoraji ataonyesha utaalamu wake kwa kutumia mikono yake.

Katika miaka ya karibuni wamechomoza wachoraji waliouonyesha ulimwengu maajabu makubwa. Kwanza walichomoza watu wanaochora kwa kutumia miguu na hii zaidi ni kule India.

Badaye wakachmoza wasanii wanaochora kwa mdomo na hii zaidi ilitokana sio kwa kupenda kufanya hivyo, lakini kutokana na hali yao ya kiafya kwa vile mikono na miguu imepooza, haina hisia na haiwezi hata kutikisika, seuze kushika kalamu.

Kwa kawaida, wengi tunaona matumizi ya mdomo ni kwa ajili ya kusema, kula, kunywa au kuonyesha ishara mbali mbali, kama ya kuchukia jambo, kwa kutegeame mdomo unavyowekwa.

Lakini binadamu kajaaliwa na Mola wake maarifa ambayo anaweza kutumia kiungo chake cha mwili na kuweza kufanya mambo ambayo ukiyaona au kuhadthiwa utashangaa kwa vile sio ya kawaida.

Kwa mfano, unapozungumzia kazi ya uchoraji kinachofahamika haraka ni kwa msanii kutumia mikono yake , iwe kwa kalamu, chaki, brashi au kitu chochote chengine kuonyesha ustadi wake katika fani hii ambayo inahitaji utulivu mkubwa.

Tumeona wapo watu ambao hawana mikono na badala yake wamekuwa wakitumia miguu kuchora picha ambazo watu wengi wenye mikono hawawezi kuzichora vizuri kama huyu aliyetumia vidole vya miguu yake.

Lakini ukiiachilia matumizi ya miguu kuchora picha siku hizi zipo picha nyingi ziliovutia maelfu kwa uzuri wa aina yake ambazo huchorwa kwa mdodo kutokana na watu wanaofanya hivyo kutokuwa na mikono.

Picha hizi siku hizi hugobaniwa kwenye minada na watu wenye uwezo mzuri wa kifedha au makampuni makubwa kwa sababu kuzimiliki pivha za aina hio limekuwa jambo la kujivunia.

Wengi wa wasanii stadi wa picha zinazochorwa kwa kutumia mdomo wapo India ambapo pia wapo wachoraji mahiri wanaotumia vidole vya miguu yao kuchora na kuandika.

Kuchomoza kwa wahoraji wa picha kwa kutumia mdomo kulipeleka kuundwa kwa jumuiya za watu hawa, wanaume na wanawake, katika nchi mbali mbali.

Hivi sasa wapo wachoraji wa aina hii wanaojulikana wanaofikia 1,000 katika nchi karibu 80.

Mara myimgi hutumiwa kutengeneza kadi sherehe za siku ya kuzaliwa, harusi, Idi na Krismasi, mwaka mpya au kalenda na wanaowapenda sana ni makampuni ya kimataifa.

Wana siasa, hasa India na na nchi za Bara la Asia, huwatumia kutengeneza mabango wakati wa kampeni za uchaguzi au zile za mada maalum ya kisiasa ili kuungwa mkono na umma.

Hivi sasa wasanii wanaochora kwa miguu na midomo wameunda chama chao kimataifa kijulikanacho kama The Association of Mouth and Foot Painting Artists of the World (AMFPA). Mnamo Septemba 5 ya kila mwaka huadhimisha Siku ya Wasanii wanaochora au kupiga ala za muziki kwa kutumia mguu na mdomo.

Unapoangalia picha zikichorwa kwa msanii kutumia brashi iliyowekwa mdomoni utashangaa na kupigwa na butaa. Kama hujamuona alipoichora hutaamini kwamba ulitumika mdomo kutokana na uzuri wake.

Miongoni mwa wachoraji mahiri wa kutumia mdomo duniani kuchora picha na kuandika ni Ganesh Kumar wa India ambaye sasa ana miaka 54.

Kumar alizaliwa katika mji mdogo wa Kannur uliopo jimbo la Kerala, India. Akiwa na umri wa mwaka mmoja tu alipata ugonjwa wa polio (kupooza) miguu, lakini alionyesha ukakamavu tokea akiwa na miaka mitatu kwa kuanza kwa shida kuchora kwenye mchanga.

Mikono yake ilikuwa haitaki, lakini aliilazimisha kuchora, ijapokuwa kwa tabu. Kwa bahati mbaya baadaye maradhi hayo yaliendelea na mikono kupooza na hapo ndipo alipoanza kutumia mdomo kuchora picha huku akiwa amekaa kwenye kiti alipokuwa na miaka minane.

Hakujaaliwa kwenda shule,lakini alijifunza nyumbani kwa msaada wa ndugu na marafiki kusoma na kuandika.

Hadi hivi sasa Kumar ameshachora picha zaidi ya 3,200, zikiwezo za anamu la Mungu wa Kihindi zinazoonekanda katika nyumba nyingi za ibada za Wahindiu na nyengine ziliotumika kwa kalenda na kadi za aina mbali mbali.

Ameshinda zawadi nono katika maonyesho mengi ya wachoraji ya watu wanaotumia miguu na mdomo na kwenda nchi nyingi za Ulaya, Marekani na Bara la Asia kushiriki mashindano ya kimataifa ya wachoraji wanaotumia mmdomo na miguu yatayofanyika tarehe 21 Septemba, mwaka huu

Columnist: Mwanaspoti