Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

GLORIA ANDERSON Anayeamini ujuzi kuwatoa vijana

A156191f918140b77043642eb4b0f9f9.png GLORIA ANDERSON Anayeamini ujuzi kuwatoa vijana

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WANAWAKE wamekuwa ni chachu kubwa ya maendeleo katika jamii hasa katika kuendeleza elimu, utamaduni, siasa na uchumi.

Tanzania sasa inajivunia kuwa na Rais Mwanamke, Samia Suluhu Hassan ambaye ameanza kazi kwa kutema cheche na kuonesha mwelekeo makini wa uchumi, pia wapo wanawake walioanzisha harakati mbalimbali katika sekta tofauti tofauti ikiwemo sekta ya elimu ambayo ni msingi wa maendeleo.

Wanawake wengine wamekuwa chachu katika sekta mbalimbali na mmojawapo ni Gloria Anderson aliye mstari wa mbele kusaidia uimarishwaji wa sekta ya elimu ambayo kimsingi sekta hiyo ni nguzo muhimu katika mustakabali wa nchi.

Grolia ni nani?

Grolia ni kati ya watu ambao wanapokutana na jambo huakikisha wanalipambania ili kujua kiini cha tatizo na kulitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Mwanadada huyu ni mwanzilishi wa Shirika linalohamasisha umuhimu wa kuwa na mfumo wa elimu unaoweza kuunganisha nadharia na ujuzi kuanzia chini kabisa kwenye mfumo wa elimu (TEDI).

Gloria ni mhitimu wa Shahada ya Masoko na Biashara aliyotunukiwa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2013 na kisha kupata Shahada ya Uzamili kwenye Utawala wa Masoko mwaka 2017.

Alianzisha shirika hilo baada ya kufanya utafiti wake uliokuwa sehemu ya masomo yake ya shahada hiyo ya pili. Utafiti ulilenga “kubaini wahitimu wanasema nini kuhusiana na suala la ajira au kujiajiri. ”

Aliwahoji vijana 100 wahitimu wa vyuo vikuu kati ya mwaka 2015 hadi 2017 waliopata matokeo kati ya GPA ya 3.5 hadi tano na alibainisha kuwa kati yao asilimia 34 walikuwa kwenye ajira rasmi huku asilimia 66 wakiwa hawajaajiriwa wala kujiajiri, hapo ndipo aliamua kutafuta suluhu ya matatizo hayo.

Anasema utafiti huo ulimpatia picha kuwa kuna changamoto kwenye sera ya elimu kwani haimuwezeshi kijana kujiajiri hivyo akaanzisha TEDI mwaka 2017 na ndani ya miaka mitatu imeshawawezesha vijana wengi kujiajiri na kuajiriwa huku akiendeleza mafunzo ya mbinu za kupata ajira na za kujiajiri, mafunzo ambayo wataalamu wake wanayatoa vyuoni na shuleni.

“Sera ya elimu ya hapa nchini haimwandai kijana kujiajiri, inapaswa iwe kwenye vitendo zaidi badala ya nadharia yaani inashangaza kuona kuwa kuna wahitimu ambao wamefaulu kwa ngazi ya juu lakini hata kuandika mpango wa biashara hawawezi,” anasema.

Kwa mujibu wa GloryTEDI imeanza kwa kuwafikia wanafunzi vyuo vikuu na tayari Chuo Kikuu Mzumbe, tawi la Dar es Salaam,

Chuo cha Biashara Dar es Salaam, Chuo cha Uhasibu Tanzania(TIA) na wanapatiwa elimu ya fedha kwa njia ya kidigitali, fedha, uongozi, ujasiriamali na mengineo mengi, pia TEDI inawafikia wanafunzi wa shule za msingi na sekondari.

Gloria anasema pia zimeanzishwa klabu za TEDI katika shule za msingi za Kisamvule wilayani Mkuranga na Chalinze A wilayani Kisarawe kwa upande wa sekondari ni katika shule za sekondari za Tabata Kimanga na Chalinze.

Kwa mujibu wa Gloria bado anaendelea na jitihada za kusaidia maendeleo ya elimu kwa jinsia zote kwani anaamini ili mafanikio ya nchi yapatikane ni lazima iwepo sera ya elimu bora inayowapatia wasaha wote kufanikiwa.

Lengo la Grolia kupitia TEDI ni kuhakikisha hata mwanafunzi anayemaliza darasa la saba akiambiwa kuanzisha biashara awe na wazo la kuanzia na tena hata akipewa mtaji aweze kuifanya biashara husika kwa ufanisi zaidi.

Anaongeza kuwa licha ya kuamini kwenye elimu ya darasani anasema kuwa huwa anakerwa kuona watu wengi wakiwemo wazazi na walezi wakilazimisha watoto wao kusoma kwa kufuata tu dhana kuwa lazima mtoto afike Chuo Kikuu ndiyo afanikiwe.

Gloria anasema mtoto anaweza kusoma chuo cha ufundi kisha akapata ujuzi na kuja kuwa mtu mwenye msaada zaidi wakati wa utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda kwa kuwa anakuwa na ujuzi ambao unaweza kuchangia uzalishaji wa moja kwa moja.

“Simaanishi kuwa wanaosoma hadi vyuo vikuu wanakosea, hapana ila nina amini kuwa kama kijana akiwa na ujuzi kwanza wa ngazi ya vyuo vya kati na kisha akasoma na kumaliza akaanza na kazi, nakwambia hata akija kujiunga na vyuo vikuu akimaliza anakuwa na uwezo mkubwa sana…sasa sera ya elimu iweke mfumo utakaolazimisha misha elimu ya vyuo vikuu iwe ya kivitendo tendo zaidi, kama ilivyo elimu ya a kati ili wanaotoka vyuo vikuu wawe awe na uwezo unaoendana na ngazi azi ya elimu husika,” anasema.

Tedi inafanya kazi na vijana zaidi ya 15 wakiwepo waajiriwa na wanaojitolea kupata ujuzi wa aina mbalimbali. Vijana hao wanafanya kazi katika masuala ya uhasibu, utengenezaji na uendeshaji wa mitandao ya kijamii, utayarishaji wa dokumentari na upigaji wa picha.

Wazo la TEDI lilipotokea

Mwaka 2018, Gloria alienda nchini Croatia kwenye kongamano la vijana lililoshirikisha vijana kutoka nchi mbalimbali duniani, wakati huo alikuwa kwenye shirika liitwalo Tycen ambalo amekuwa akijihusisha nalo kwa muda mrefu tangu akiwa anasoma.

Akiwa nchini humo alikutana na raia wa Kenya aliyekuwa akifanya kazi katika mradi mmoja ambao wamiliki wake walikuwa wakitafuta Mtanzania wa kushirikiana naye.

Mwaka huo wa 2018 wakati anakutana na wazo hilo ilikuwa ni mwaka mmoja tangu afanye utafiti wake kuhusiana na wahitimu na ajira, hivyo aliona kuwa akianzisha shirika ataifanyia kazi vizuri zaidi.

Akiwa anaendelea kuzungumza na kijana huyo Mkenya kuhusiana na kufanya kazi hiyo, hapo likaja pia wazo la yeye kwa nini asiwe na mradi wa kusaidia vijana.

Muda huo alikuwa akifanya kazi na shirika la Tycen ambalo alikuwa nalo tangu akiwa anasoma lakini muda huo huo pia alikuwa ametoka kufanya kazi katika Kampuni ya Multichoice alikodumu kwa miaka minne kuanzia 2014 hadi 2017, hivyo wakati akihudhuria mkutano huo ilikuwa ni mwaka mmoja tangu atoke Multichoice.

Gloria anasema kuwa ulikuwa ni kama mwito wa kuambiwa kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya kwa vijana yaani kuwawezesha kujiajiri na kwa kuwa alikuwa ameshaacha kazi aliona wazo linalofika mbele yake ni kuja kuwa mkombozi kwa vijana.

Leo hii ikiwa ni miaka takribani mitatu tangu kuanzisha TEDI anaona mwelekeo wake ni thabiti kwa kusaidia vijana kupata ajira pamoja na kusaidia kuimarisha sera ya elimu.

Gloria amesoma hapa hapa nchini kuanzia elimu ya msingi hadi chuo kikuu. Elimu ya msingi alipata katika Shule ya Msingi Kijenge, kisha kuanza elimu ya sekondari kwa ngazi ya kidato cha kwanza hadi cha nne kuanzia mwaka 2004 hadi 2007.

Mwaka 2008 hadi 2010 akaendelea na kidato cha tano na sita na miaka yote akiwa anasoma sekondari

alikuwa akijihusisha na shughuli za mashirika mbalimbali kama vile Tycen, Support for International Change(SIC) na Team Youth Leadership.

Gloria anampenda mwanasiasa, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Asharose Migiro. Anampenda kwa sababu mtazamomtazam wake ni mwanamama mwenye uthubuthubutu, lakini pia ana imani kubwa na Rais Samia Suluhu Hassan hasa kutokana na kile alichodai kuwa Gloria ameonesha njia kubwa na yenye matumaini.

Mwanadada huyu anamalizia kwa kusema mbali na shughuli zake hizo, mambo mengine anayopenda ni kujiendeleza kimaisha na kikazi, vile vile anapenda kuwa na marafiki wa aina mbalimbali hasa ambao wanakuwa na mtazamo chanya na wenye lengo la kuendelezana kimaisha kwa kupatiana mawazo endelevu.

Columnist: www.habarileo.co.tz