Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Fahamu hili: Huu ndio mmea unaopatikana Tanzania tu!

Mpugu Puguuu (600 X 354) Fahamu hili: Huu ndio mmea unaopatikana Tanzania tu!

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MMEA ujulikanao kama mpugupugu uliopo katika Msitu wa Hifadhi ya Mazingira Asilia Pugu Kazimzumbwi, Wilaya ya Kisarawe, mkoani Pwani upo hatarini kupotea.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Fendey Mashimba amesema hayo alipozungumza baada ya Umoja wa Uhifadhi wa Mazingira wa Kimataifa (IUCN), kufanya tathmini na kuuweka mti huo katika kundi la mimea adimu iliyo katika hatari ya kutoweka duniani.

“Hii ni aina ya mimea ambayo inapatikana katika eneo hilo tu la Pugu, kwa kitaalamu tunaita ni mimea ambayo haipatikani sehemu nyingine yoyote duniani, hata hapa Tanzania nje ya eneo hilo la Pugu Kazimzumbwi,” amesema.

Columnist: www.tanzaniaweb.live