Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

FAHAMU: Jinsi Waziri Mkuu anavyopatikana leo, Spika na barua ya JPM

Istockphoto 657943988 170667a FAHAMU: Jinsi Waziri Mkuu anavyopatikana leo, Spika na barua ya JPM

Thu, 12 Nov 2020 Chanzo: millardayo.com

Leo Novemba 12, 2020, katika Mkutano wa tatu wa Bunge la 12, Waziri Mkuu wa Serikali itakayoongoza 2020 hadi 2025 atafahamika rasmi kwa mchakato unakuwa kama ifuatavyo.

Spika wa Bunge atapokea barua kutoka kwa Rais yenye jina la mteule wa nafasi hiyo, atasoma ujumbe uliomo ambao utakuwa umeambatana na jina la Waziri Mkuu aliyeteuliwa na Rais.

Kisha Spika ataahirisha Bunge kwa dakika 45 ili kuwapa nafasi wabunge kutafakari uteuzi huo kisha kumthibitisha.

Rais Magufuli amesema ana uwanda mpana wa kuchagua mawaziri kutokana na kuwa na wabunge wengi wa CCM tofauti na muhula ulipita.

Via JF

HOTUBA YA MWINYI ILIYOGUSA HISIA ZA WAZANZIBAR “NITATUMBUA, NITAPAMBANA NAO, HII VITA”

Columnist: millardayo.com