Kijamii

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Lifestyle

SIL

MenuKijamiiMaoni
Articles

Dunia ya Soka haina cha kumdai Thiago Silva

Thiago Silva Career Thiago Silva

Tue, 31 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

September 22 mwaka jana, Wabrazil wawili walisherekea birthday zao. Mmoja alitimiza miaka 38 na mwingine alitimiza miaka 46. Beki mmoja kisiki sana na mshambuliaji hatari wa kizazi chake!

Yule mshambuliaji akiwa mtu aliyebarikiwa kipaji kikubwa sana ametwaa tuzo nyingi binafsi ikiwemo tuzo ya mwanasoka bora wa dunia.

Bahati njema pia, alikuwa sehemu ya kizazi cha dhahabu cha Brazil kilichotwaa world cup 2002. Hata 1994 alikuwepo kikosini lakini hakupata nafasi. Kumbuka Romario na Bebeto waliongoza safu ya ushambuliaji.

Hiyo ni bahati njema lakini bahati mbaya ni kwamba hakucheza soka la ushindani kwa muda mrefu. Akiwa na miaka 31 tu tayari alikuwa nyumbani Brazil akimalizia soka lake.

Hata kipindi alichokuwa moto sana, majeraha yalimsumbua na hakuonekana uwanjani kama alivohitajika. Inasemekana alikuwa na mambo mengi nje ya uwanja.

Huyo ni Ronaldo de Lima ambaye birthday yake imerekodiwa kuwa September 18 japo alizaliwa September 22 sawa na Thiago Silva ijapokuwa Thiago ni mdogo!

Hii ni safari ya pili ya Silva Ulaya baada ya ile ya kwanza kukwama. Aliposhindwa kutoboa katika kikosi cha Porto aliamua kurudi nyumbani Brazil na kuanza upya.

Alirejea Ulaya tena akiwa kijana wa miaka 25 kujiunga na AC Milan. Tangu hapo hajawahi kurudi nyuma tena. Amesonga mbele siku zote.

Katika umri wa miaka 38 bado anacheza soka la ushindani Ulaya tena kwa kiwango kikubwa katika klabu kubwa. Bado mwili una nguvu ya kukimbizana vijana wadogo wa miaka 21.

Tofauti na yule Ronaldo halisi, yeye hajashinda sana tuzo binafsi lakini hajawadhulumu mashabiki kwa kupotea mapema. Fikiria, miaka 38 bado anacheza Ulaya.

Bila shaka ndie beki bora wa kati kwa sasa duniani (mtazamo wangu). Kama utabisha basi naamini katika 'tatu bora' yako yupo. Wapo wachezaji wachache sana Wanaoweza kuwa bora duniani hadi katika umri wake.

Bila shaka Chelsea watampa mwaka mwingine wa mkataba ukizingatia kwamba walpata bure kutoka PSG. Kwa hiki anachokifanya nadhani Chelsea wanaweza kuwa waungwana wakamrudisha Ufaransa na kumsajili upya, walau kwa paundi 50 milioni.

Columnist: www.tanzaniaweb.live